Rais Samia: Nilipoingia ofisini tu Mufti alinijia na furushi la migogoro ya mali za BAKWATA, ila tatizo wamelitengeneza wenyewe

Hivi Kuna wakati wakatoliki walimpelekea Nyerere migogoro au Mimi ndio sielewi.serikali ijitenge na dini la sivyo watakuja waumini wa dini zote huko ikulu

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
Modest...
Soma kitabu, "Development and Religion in Tanzania," (1981) cha Jan P van Bergen kinaeleza mikutano ya Nyerere na viongozi wa Kanisa Katoliki Ikulu.

Mimi hujizuia sana kuandika haya lau kama nayajua mengi.

Lakini kwa kuwa hukuwa unayajua hayo nimekupa rejea hiyo ili uijue nchi yetu na matatizo yake.

Kitabu hiki kilikuwa kinauzwa Cathedral Bookshop lakini kwa unyeti wa yaliyokuwa ndani ya kitabu hicho kimya kimya kiliondolewa sokoni kisiuzwe.

Hiki kitabu kilikuwa maarufu sana kwa Waislam katika miaka ya 1980.

Taarifa hizo zilizokuwa katika kitabu hicho ziliandikwa katika kitabu cha Prof. Njozi, "Mwembechai Killings..." (2002)na serikali ya Rais Mkapa ikapiga marufuku kitabu hicho.

Kuitaka serikali ijitenge na dini kwa maana yake kwa Tanzania ni kulitaka Kanisa likae nje ya serikali.

Huu ni muhali mkubwa kwani Kanisa limehodhi uendeshaji wa nchi kwa asilimia 80:20.

Hii ni kama vile Waislam hawapo.

Hili la waumini wa dini zote halipo Tanzania.

Dini kubwa zenye maslahi na serikali ni Uislam na Ukristo.

Waislam maslahi yao katika serikali ni historia yao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wakristo maslahi yao ni kuwa ndiyo walioshika madaraka ya kuendesha nchi toka uhuru upatikane mwaka wa 1961 hadi hivi sasa.

Vipi leo utawataka waachie madaraka haya?

Busara ni walioshika madaraka yote ya serikali wawe tayari kuona na wengine wanapata fursa walizopata wao za elimu nk na wanaingi serikalini bila wao kuwa pingamizi.

 
Ile chang'ombe karibia nusu vimeuzwa viwanja vya waislamu .ila wahusika ni hao hao viongozi wanaoneana aibu.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Shehe mkuu anajua fika hizo mali zimeuzwa kihalali na wenzake waliomtangulia, kwa hiyo anatafuta huruma ili Mh Rais apore haki za wengine wapewe wao, kwa kuwa Rais anayo mamlaka ya kufanya hivyo ili awafurahishe wao, hiyo nia yao mbaya Rais kaishtukia kaikwepa.
 
Yaani
Kuna mahali niliwahi kwenda nikawaambia jamaa nataka.ninunue eneo including msikiti wakakubali.
[/QUOTE Yaani wewe jamaa huwa sikupendi skabisaa. Wakati Mwendazake anatuhujumu wewe ilikuwa ukifurahia sana
 
johnthebaptist umesikia maneno hayo?
 
BAKWATA ni serikali au ni waislamu ?
Tatizo mnapokwepa kuwajibishana na kulazimisha kuonekana mnaonewa ndio shida inapoanzia.
Pokeeni changamoto zenu zishughulikieni itasaidia kuliko kulazimisha kila siku.
 
Mufti alibugi kweli kumpelekea Sa100 kesi za aina hii, mama anayaogopa sana mafisadi...sanasana angeyaomba YAMPISHE halafu shughuli ingekuwa imeisha!.
Mufti alijua kwa kuwa ni mwislamu mwenzake basi atashughulikia mgogoro vizuri.
 
johnthebaptist umesikia maneno hayo?
Kinyungu,
Katika miaka ya 1970 Rashid Mfaume Kawawa alimwambia Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa endapo iko siku watataka kuuza nyumba hiyo basi wawauzie TANU kwani hiyo nyumba imebeba historia kubwa ya Mwalimu Nyerere na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Shkamoo Mzee Moh'd, hili umeliandika kwa bahati mbaya au kwa kumaanisha? Au ni madaraka yapi tunayoyazungumzia?
Ndg,kuna changamoto kubwa sana. Nakumbuka kipindi cha Magufuli palikua na kelele nyingi sana kuhusu wale masheikh walio selo. Imani ya wengi ni kuwa wanaonewa sababu ya dini. Ukiwauliza hao masheikh walikamatwa kipindi gani wanatafuta sababu mpya. Ni ngumu sana kuwaelewa
 
BAKWATA ni serikali au ni waislamu ?
Tatizo mnapokwepa kuwajibishana na kulazimisha kuonekana mnaonewa ndio shida inapoanzia.
Pokeeni changamoto zenu zishughulikieni itasaidia kuliko kulazimisha kila siku.
Dingi...
Kuna haya maneno ambayo siyaelewi vyema: ''mnapokwepa kuwajibishana na kulazimisha mnaonewa.''

Sijui unaposema kwa kujumuisha ''mnapokwepa...'' sijui unawakusudia nani hao?
Nani amuwajibishe nani?

Naamini huwakusudii Waislam kuwaingilia BAKWATA katika taasisi yao.

Ama kuhusu ''changamoto,'' Waislam baada ya kuvunjwa kwa EAMWS walipokea changamoto hiyo kwa mikono miwili na hawakukata tamaa.

Katika utawala wa Julius Nyerere Waislam hawakuruhusiwa kusajili taasisi yeyote ya Kiislam kwa maendeleo yao.

Hata hivyo kulikuwa na harakati za chini kwa chini dhidi ya BAKWATA kupitia Warsha taasisi ya vijana wasomi waliofanya kazi kubwa sana ya kuwaamsha Waislam kujitambua.

Harakati hizi zilizaa matunda kipindi cha utawala wa Rais Mwinyi aliporuhusu Waislam kusajili taasisi huru kwa ajili ya maendeleo yao.

Waislam hawajapata kulazimisha chochote ndiyo maana leo utaona kuna BAKWATA na kuna Shura ya Maimam Tanzania na taasisi nyingi huru nchi nzima.

Hizi hazina ugomvi na BAKWATA kila taasisi inajitahidi kuutumikia Uislam kwa lile wanalolimudu.

Wanaoweza kujenga shule wanajenga, wanaoweza kufungua stesheni za tv na radio wanafanya hivyo nk.

Wanaoweza kuandika vitabu vya kuwaelimisha Waislam wanafanya hivyo nk.
 
Dingi...
Tatizo la kukamatwa Waislam ni tatizo kubwa sana.
Waislam wanakamatwa lakini kesi ikifika mahakamani hakuna ushahidi.
 
Shukuru...
Serikali ya Tanzania mwaka wa 1993 ilitiliana sahihi mkataba na makanisa, mkataba uliokuja kujulikana kama Memorandum of Understanding makubaliano ambayo yalikuwa serikali kuidhinisha elimu, huduma za jamii na afya ziendeshwe na Christian Council of Tanzania (CCT) and Tanzania Episcopal Conference (TEC) kwa kushirikiana na serikali.

Mkataba huu ulitayarishwa kwa siri na Dr. Costa Mahalu, wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na ukatiwa sahihi na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mkataba huu ulitiwa sahihi bila ya kuwashirikisha au kuwafahamisha Waislam.

Ili makubaliano haya yaweze kutekelezeka, serikali ilibidi ifanye marekebisho kifungu 30 cha Education Act No. 25, 1978.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…