Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Mtu hajui anachokisimamia. Yaani ni bora kunakucha tu.

Huyu ndio anataka 2025 eti apewe kisa yeye mama.

Lumumba mtakosea sana kutupatia hii karata dume.
 
Kwa mujibu wako wewe timu mwenda zake,HUONI U.K,GERMAN,USA ,INDIA WANANCHI WANALALAMA JUU YA BEI YA MAFUTA KWA GALON YAMEPANDA ALMOST MARA MBILI,/PENDA KUJUA PIA MAMBO YA KIMATAIFA.
Mpuuzi wewe mafuta yaliagiza Dec 2021 tukaambiwa nafuu tutaanza kuiona March 2022 badala yake ndiyo yanapaa kabisa
 
Vibali vya machinga vurudishwe tu ila wapangiwe maeneo maalum itasaidia kudhibiti impacts iliyopo, kwani hatuwezi kukwepa tanzania ni sehemu ya dunia.
 
Safi ndio maana namkubali mama,huwa hapepesi macho aki focus jambo lazima akomae nalo ,mtukane,mnune au msengenye ndio kwanza anawapuuza.

Tukutane 2025,,watu mtaumia wee lakini matokeo yatayoishi vizazi na vizazi yataendelea kuwepo.
Uzuri ni kwamba, wenyeviti, madiwani, Wabunge, wote ni wa chama kimoja.

Chadema walituchelewesha sana kupata maendeleo.

Tukae kwa kutulia dawa iingie.
 
Rais yupo sawa kabisa mafuta yamepanda na yanaendelea kupanda. Isiwe maisha yenu yapo kwenye wasapu tu angalieni huko ulimwenguni kuna nini ili msiipe shida sirikali.

Ila nimesikia Mafuta ya Urusi yanapatikana kwa bei chee na wanakufikishia mpaka mlangoni achaneni na Opec, ila ameshusha kwa nchi rafiki tu na kama haittoshi kuanzia kesho 31/03/2022, Urusi haitapokea dola au pound katika biashara ya kimataifa watapokea rubo kama sijakosea.
 
Uzuri ni kwamba,wenyeviti, madiwani, Wabunge,wote Ni wa chama kimoja.

Chadema walituchelewesha Sana kupata maendeleo.
Tukae kwa kutulia dawa iingie.
Hata wangekuwa vyama tofauti, so long as pesa inakusanywa na matokeo wanayaona hakuna shida, unune au ukunje ndita lazima ugharamie maendeleo.
 
Ilivyoondolewa mlimsifu raisi, kaibakisha mnamsifu
[emoji23][emoji23][emoji23]
In fact mimi niliwahi kupinga toka mwanzo Rais alipoanzaga kuondoa au kufuta tozo ya miamala ya simu kwa sababu tayari ilishakuwepo kwenye bajeti na isitoshe hicho chanzo kulikuwa specific kwenye afya, barabara,maji na elimu.

Unapoondoa manake unaharibu mipango ya serikali.

Kuhusu tozo ya mafuta,kwanza nilishangaa how comes uondoe tozo ya sh.100 ulivyosema ni ya Mfuko wa Tarura? Unaondoa wakati tayari umekomit miradi na wakandarasi wako site,utawalioaje kama sio kuwasababishia umaskini kwa sababu ya Madeni?

Hapo kwenye mafuta kuna Kodi za kuondoka kama tasac,TBS ,ewura na takataka zingine ila sio kuondoa pesa ya maendeleo.
 
Hawana ubunifu wa kupata mapato wanachojua ni kutegemea kodi tu kwa kuwaumiza wananchi tu
 
Kwa mujibu wako wewe timu mwenda zake,HUONI U.K,GERMAN,USA ,INDIA WANANCHI WANALALAMA JUU YA BEI YA MAFUTA KWA GALON YAMEPANDA ALMOST MARA MBILI,/PENDA KUJUA PIA MAMBO YA KIMATAIFA.
Ila mlienda UAE mwaka jana November, mkasema mafuta yataaanza kushuka Bei January mwaka huu.

Lakini hayakushuka. Sasa si mlikua mnaongopa?
 
Duuh!
Mi-5 tena 🙄 Hadi akili zikae sawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…