Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Tajiri ataendelea kutajirika na maskini tutaendelea kusaga meno kwa uchungu.

Hali ni mbaya hakuna bidhaa inayoshikika kwenye bei.
 
Kama nawaona ewura wakija kuruka hewani na mkeka mpya, wapi kaguo........ila mama hii 100 inaihenyesha serikali wakati wamebambikiza matozo kwanye miamala ya simu na hadi wameweka VAT kwenye miamala ya kwenye mabenki.

Yaani unamtoza VAT mtu anayetoa pesa kwenye akaunti yake ya akiba ili akanunue bidhaa na huduma ambazo vilevile atakatwa VAT.........mama itabidi afikirie kutoa fursa kwa wengine nao wajaribu bahati yao come 2025.​
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe...
Niliandika hapa kuwa muda si mrefu tutaambiwa vita ya Ukraine na Urusi ndio imeleta huu mfumuko ,utadhani huu mfumuko ndio umeanza juzi, Bongo pana mizaha mingi sana.
 
Mama anakosea kutamka wazi kwenye hotuba zake kwamba vitu vitapanda kisa vita vya Ukraine na Urusi, hii wafanya biashara wanatembea nao na wataongeza gharama maradufu ili kujipatia faida kubwa.

Mama swala hili la mafuta angefanya kama hajaliona, wafanya biashara wangelalamika tu, then anakaa nao mezani mnapangiana bei atleast kutakuwa na ongezeko la bei ambalo ni uniform kwa wafanyabiashara wote.Lakini hii ya kutamka kwenye hutuba zake "vitu vitapanda bei sababu ya vita......." wafanyabiashara wanatambaa nayo na kila mtu atakuwa na bei yake.

So ndugu zangu tutafute baiskeli.
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe...
Kusema kwamba kuondoa shs 100/ tayari ilikuwa kwenye budget ya mwaka; kwani ya misaada kama ya TZS 1.3tr zilikuwepo kwenye budget?

Wakati fulani ni jukumu la serikali na hata Bunge kuingilia kati hizi tuzo na hasa nyakati kama hizi vita. Kusema kwamba ikitokea vita kati nchi moja na nyingine bus mzigo wa kubeba impact ya vita hivyo, budi aubebe mwananchi, nadhani serikali nayo inabidi iwajibike.

Tuangalie mfano wa bei za mafuta kwenye nchi ambazo ni land- locked countries, mfano Malawi, Uganda, Zambia, ni bei za petrolium products zipo chini. Ni dhamira tu ya serikali hizo na mabunge yao
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe...
Duu, huyu rais kiboko aisee.
 
Tatizo ni moja tu, rais Samia S Hassan hana uchungu na wananchi hata kidogo,anazungumza akiwa mkavuu, kama anasema " mtakoma mwaka huu".

JPM , kwenye ishu kama hizi angezungumza kwa uchungu sana mpaka machozi yanakaribia kutoka. Halafu angechukua hatua ambazo wananchi tunaona kweli hapa tuna kiongozi.

Mama kama anatutupia tu mizigo tupambane nayo, haumizi kichwa,anaagiza tu wenye mamlaka sekta fulani waangalie na kuchukua hatua,kitu ambacho JPM angefanya mwenyewe kuhakikisha maamuzi sahihi yanafanywa na kwa wakati.

JPM alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, lakini hii nafasi ya kuongoza nchi ilimfaa na kum fit ipasavyo.

Hakika tulipoteza kiongozi thabiti.
Huyu wa sasa simpendi kabisa hata kumuona.
 
Back
Top Bottom