Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Karibu kila Rais kuanzia Mzee Mwinyi aliljikuta akilazimika kuzoea kufanya kazi huku akiisikia sauti ya mtangulizi wake ikiongelea namna anavyoendesha nchi. Huu umekuwa ni mtihani mzito wa kuirithi ofisi nzito ya urais.
Mzee Mwinyi anaikumbuka hotuba ya Mwalimu Nyerere mwezi March 1995 pale Kilimanjaro Hotel namna ilivyompiga vijembe uongozi wake, Alikuja kuijibu hotuba ile japokuwa majibu yake hayakuwa na ushawishi kwa waliyoyasikiliza kulinganisha na madhara ya hotuba yenyewe. Mwalimu Alikuwa na kipaji cha kuongea na kupendwa.
Mzee Mwinyi akiwa ikulu hakumsimanga Mkapa wala kumuonyesha kwamba sehemu fulani anakosea na sehemu fulani angechukua njia nyingine ingekuwa ni heri zaidi kwa uongozi wake. Hakukuwa na sauti ya pembeni yenye kushauri mamlaka yake na wakati mwingine ukiyakwaza.
Mwinyi alistaafu siasa za kujiingiza moja kwa moja mara nyingi akionekana katika shughuli za matembezi ya hisani akiimarisha afya yake na mpaka anafikisha miaka 96 ni matokeo ya faida za kutembea kila mtu anapopata wasaa wa kufanya hivyo.
Utaratibu wa rais mstaafu kuwa mshauri asiye rasmi umeendelea kutumika haswa kwa kuzingatia bahati ya kitaifa tuliyonayo ya kuachiana madaraka pasipo matumizi ya mitutu ya bunduki.
Rais Samia ndani ya mwaka mmoja na nusu ukiwa amiri jeshi mkuu umeshaona madhara ya utaratibu huu usio rasmi wa rais kutakiwa kupelekeshwa na mtangulizi wake na hulka hiyo ikiambatana na ile mbaya zaidi ya kutaka watu wa huyo mstaafu ndio wawe na sauti juu ya yote unayoyafanya.
Rais wangu SSH umeamini sasa kuwa anayekuchekea sio kuwa ndiye mwenye moyo mzuri kwako. Simama na Mungu wa mbinguni kwa vitendo katika muda wote wa miaka mitatu iliyobaki ya awamu yako. Fanya kazi kwa kutanguliza busara za kimungu zinazotafutwa kwa njia ya ibada kila unapoamka asubuhi.
Watu wako wa karibu wamekusikilizisha hicho walichokirekodi na kama ninakuona ukiwa huamini moyo wako kwamba uliowachukulia kama ni watu wako wa karibu wangeweza kupanga mipango mibaya dhidi yako wewe.
Simama na Mungu wa mbinguni, ndio ameipanga safari yako mpaka muda huu ulipofika, hao wanaokupigia makofi na kukupamba sio wa kuwaamini, ishi nao kimachale sana. Wanaweza wasiwe walevi wa pombe za kidunia kwa maana ya mivinyo na bia za aina mbalimbali lakini haya maisha mafupi na fahari zake zote ni vitu wanavyoviabudu tangu wakiwa wanasiasa vijana wakilelewa na wastaafu mahayati wa CCM.
Epuka hizi harakati za kinamama,kujitambulisha na jinsia moja tu, epuka haya mambo ya uchifu. Simamia utekelezaji wa ilani uliyoinadi kwa wananchi ukiwa na hayati JPM. Pima kwa kina kila unachokisikia kutoka kwa hao hao walioingizwa katika vyeo mbalimbali nyeti ndani ya mwaka mmoja tangu aliyekuwa bosi wako alipofariki dunia.
Wenye nia njema ya kuiona TZ ikistawi miaka na miaka pasipo ulazima wa matumizi ya mitutu ya bunduki daima tunapopiga magoti makanisani na misikitini tunakuombea. Mungu akutie nguvu na akujalie busara za kufanya kila aina ya maamuzi ndani ya wakati wake.