Did you ask why watu walikua kimya na kuridhia?
Perhaps watu walimpenda na kumuamin kias cha kutokua na shaka naye... Ila ukiona watu kinawafurukuta rohon.. ujue bas kuna uwalakin.
Hapo hakuna Cha kumwamini Wala Nini?
Udini TU na ukabila umewajaa watanganyika linapokuja suala la madaraka.
Kila akitokea Rais wa dini ya kiislam watu wanapanua midomo kama Makinda ya Kunguru kumlalamikia na kulaumu kila jambo.
Acheni hizo bhana.
Kuna Watanganyika wanawaza kupata uteuzi TU na sio amani ya kweli na utulivu wa Nchi.
Waacheni Wazanzibari wapumue kidogo mana mnawabana kila kitu kwenye uchumi .
Wazanzibar fursa zao zinazuiwa makusudi na wezi wa bara waliozoea kujilimbikizia Mali Kwa Rushwa. Sasa wanaona Fursa zimepanuka mpaka Zenji.
After all wanaosumbuka na Muungano ni wezi wa Bara na sio wazanzibar. Zanzibari hata kesho ukitaka kuwaachia nchi yao hawana Tabu . Bara wanakuja na visingizio vya usalama sijui na nini.!! Mkoloni alikaa na Wazanzibar Kwa miaka mingi na hapakua na Tatizo kila mmoja akiwa na nchi yake.
Tuwaheshimu Wazanzibar na watu wa Pwani na Waislam kwani ni watu waungwana sana. Kuna watu wa Bara wanaona wao TU ndio wenye sifa za kuongoza lakini wakipata madaraka hakuna unafuu wowote Kwa wananchi zaidi ya wachache kujilimbikizia Mali na kupeana madaraka na Rushwa,ukabila na Udini unaofanyika chichini chini huku wakitumia nguvu kubwa kudhibiti watu wa watu wasilalamike hata Kwa takwimu za wazi.
Mh . Mama Samia Rais wetu chapa Kazi achana na wahuni waliozoea kubebwa na mifumo kandamizi ya Kikoloni na Kifarao.
Watanzania ( Wazanzibari na watanganyika ) Sasa wanapumua kwenye nchi yao.Kwa miaka mingi Wapemba walionewa sana na bahati nzuri ni kwasababu Mwenyezi Mungu amewabariki kwenye biashara zao hawategemei pesa za kukwapua kwenye maofisi ya umma na madili kuendesha maisha yao. Wengi wanafanya biashara zao Kwa haki .
Wazanzibari Wana vitu vingi sana ambavyo kwao vingeweza kuuzwa kama Used huku bara lakini Kwa sababu ya Roho mbaya za watanganyika wanazuia na kuweka Kodi kubwa ili wasiuze.
Kwa Nini wasiweke utaratibu kuwa Kama mfano ni Gari likiwa imenunuliwa na mtu wa Zanzibari Kwa miaka mitano linaruhusiwa kuuzwa Tanganyika Kwa kulipia ushuru wa bandandari na Kodi ya Usajili na sio kama gari inayotoka Japan au Dubai?
Watanganyika wengi kwenye uchumi ni wanafiki sana. Hakuna dalili ya kuwa tupo kwenye nchi Moja.
Na bila kuficha Muungano unawanufaisha wanasiasa na sio uchumi wa nchi. Wale wanaoingia kwenye Bunge la Jamhuri ndio wanaonufaika na Muungano na ndio maana wanafunga midomo yao kupigania Zanzibar na uchumi wa Zanzibar. Wabunge Zaidi ya 50 wanatoka kwenye Eneo lenye ukubwa wa Wilaya ya Serengeti. Hawaoni huruma ya Kodi za nchi maskini Kama Tanzania zaidi ya kuwaza kuongeza majimbo. Mambo ya Msingi ya kuinua uchumi wa ZANZIBAR hawanadili wanajadili madaraka TU na Kupiga makofi ili majimbo yaongezwe na watoto wao wapate nafasi na majimbo ya kupata Ubunge wakale Bata.