Rais Samia: Sasa Tanzania tumeuza (Bandari), wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

Rais Samia: Sasa Tanzania tumeuza (Bandari), wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

Kama hujui hata USA wana mkopo mkubwa huko China unafikiri utasaidika vipi?
Sasa ni sawa sie wenye deficit bajeti mpaka tuombe au tutafute mikopo ni sawa na usa ambaye deni lake limetokana na china kununua treasury bond za federal reserve na mchina anafanya hivyo kimkakati ili aweze kuexport more into usa kwa hiyari yake acha kufananisha na sisi wenye deficit bajeti zetu na watu wenye bajeti za surplus halafu tuende kucompete inakuwa vichekesho ,ni wakati kufungua nchi uwe na mikampuni yenye pato kubwa mara 10 ya nchi ili uchumi uchangamke hayo aliyaona Deng wa china akakaribisha foreign investment leo china ana usd za kutosha kutokana na export kwenda usa kupitia hizo hizo kampuni za usa mwanzoni na sasa za kichina baada ya kupata tech transfer na wanajeuri ya kwenda kununua hizo treasury bond unazowasifia, endelea kulala tu dunia ilishamka toka zamani sasa .
 
Baada ya kupita Cheng'a nyingi , kulia , kushoto, juu, chini , hatimaye wamejitokeza na kuonyesha sababu kuu ya huu ubinafsishaji ni 35% ya hisa watakazo chukua baadhi yetu , kwenye huo mgodi WA bandari. Uwekezaji WA DPA ni kivuli kinachotumika katika ubinafsishaji huo.
 
MKuu hizo 35% anachukua Rais na mawaziri? Weka nyama.
 
Rais Samia akihutubia wakati wa uapisho wa viongozi, akizungumzia kuhusu Wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji ameonesha namna ya kuweza kuzitambua fursa mbalimbali na kuzifanyia kazi kama nchi ili zisipotee.

Akitolea mfano sakata la sasa la fursa ya uwekezaji kwenye bandari zetu amesema haya, nanukuu

Nataka niseme vizuri hili suala la fursa na watu wanavyozitumia. Ndugu zangu wakati sisi tunalumbana bandari yetu apewe nani, iende isiende, ikae, ivue, isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu mmeona wame-jump wamekwenda kulekule, na lile jumba lililowekwa bendera ya Tanzania, limewekwa bendera ya jirani.

Sasa Tanzania tumeuza, wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

Na siku ambayo Bunge letu hapa lilisema kwamba ni ruhusa bandari yetu iendeshwe na Serikali na sekta binafsi, siku ya pili wenzetu wakasema ninyi moja? Sisi zote zilizoko huku ziende private sector na wakakimbilia kwenda kule kwenda kuwahi nafasi. Kama wale wanalumbana, njooni huku.

Sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka.

Nimesema tu nitoe mfano huo kuona changamoto na jinsi ya kupata fursa kuzitumia na kuzifanya zisiponyoke.
Hivi hiyo fursa wanayodai ni fursa gani? Isije ikawa ya kwao kujitajirisha tu.

Mpaka sasa wanayodai hawana mkataba na DPW, kwa maana hiyo hawajui ni kiasi na kiwango gani DPW wako taarifa kuwekeza. Hawajaona hata business proposal yao. Hayo yote ni expectations tu. Ni sawa na kuona mwanamke mzuri unakimbilia kumuoa lakini huna guarantee kuwa anakuzalia watoto.
 
Kunautofauti pia, hao wenzetu jengo limewaka bendera zao tu kuonesha uzarendo wao sisi ilikuwa lilionesha picha ipi?
Unaonekana unapenda sana muziki wa mwambao wewe, Rais wa taifa lolote lile ni nembo na alama ya taifa, kama vipi tuchukue yako tukaweke.
 
Mama asibabaishwe na wapuuza wachache wenye lengo la kumtoa kwenye lengo.
kazi iendelee mbele kwa mbele hakuna kurudi nyuma.
 
Ndio hivyo kwani Cha ajabu ni kipi? Na huna jeuri yeyote kwake
Kuna jambo moja tu ambalo sasa limethibitika rasmi, tofauti na zamani kwa sasa watanzania hawaogopi Tena kutetea na kulinda Mali zao bila kujali vyama vya siasa,dini,kabila Wala propaganda Ila wanaongozwa na uzalendo,mwaka huu mtaelewa tu.
 
Sasa kwani Kuna shida? Ukipotosha utashughulikiwa
 
unampangia wewe kama nani?
Wewe unamuuliza huyu Kama Nani kwani wewe Ni Nani mpaka umuulize yeye Ni Nani. Huyu Ni mtanzania ni raia wa kawaida ambaye amezalwa katika ardhi ya tanzania na atafia katika ardhi ya Tanzania. Namie Ni Kama huyo huyo uliyemuuliza ivyo. So wewe ni malaika ama Ni Nani. Ama unaona kisa una kacheo fulani Basi unajua kuwa unatembea juu ya mabega yetu.
We've to defend our Nation by blood,tears and sweat for others.
Najua unatetea tumbo ambalo litaoza muda si mrefu
 
Rais Samia akihutubia wakati wa uapisho wa viongozi, akizungumzia kuhusu Wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji ameonesha namna ya kuweza kuzitambua fursa mbalimbali na kuzifanyia kazi kama nchi ili zisipotee.

Akitolea mfano sakata la sasa la fursa ya uwekezaji kwenye bandari zetu amesema haya, nanukuu

Nataka niseme vizuri hili suala la fursa na watu wanavyozitumia. Ndugu zangu wakati sisi tunalumbana bandari yetu apewe nani, iende isiende, ikae, ivue, isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu mmeona wame-jump wamekwenda kulekule, na lile jumba lililowekwa bendera ya Tanzania, limewekwa bendera ya jirani.

Sasa Tanzania tumeuza, wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?

Na siku ambayo Bunge letu hapa lilisema kwamba ni ruhusa bandari yetu iendeshwe na Serikali na sekta binafsi, siku ya pili wenzetu wakasema ninyi moja? Sisi zote zilizoko huku ziende private sector na wakakimbilia kwenda kule kwenda kuwahi nafasi. Kama wale wanalumbana, njooni huku.

Sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka.

Nimesema tu nitoe mfano huo kuona changamoto na jinsi ya kupata fursa kuzitumia na kuzifanya zisiponyoke.
 
Basi itakua wamepewa rushwa maana mkataba ni mbovu haielezeki.
Tunapoteza muda kwenye ujuzi wa misemo mingi na nahau za jamiiforum wakati mataifa makini hayana muda wa kusubiri sisi tuamke.

Ulishawahi kuiona mikataba mingine kama ule wa bomba la mafuta? Tangu uhuru tumeshakuwa na mikataba mingapi?

Tupunguze siasa.
 
Kwa akili hizi hata mkielimishwa kuhusu vipengele vya mkataba ni kupoteza muda tu. Nilimuelewa sana JPM hakulea vichwa vya aina hii, mikataba mingi aliingia akiwa rais na hakuna hata mmoja tuliojadili kama huu wa bandari.
Hata hasimu wake mkubwa Tundu Lisu anakili wazi kuwa JPM hakuwa na hizo tabia za wizi ndio maana anaaminiwa hakutuingiza kwenye majanga.
 
Hata hasimu wake mkubwa Tundu Lisu anakili wazi kuwa JPM hakuna na hizo tabia za wizi ndio maana anaaminiwa hakutuingiza kwenye majanga.
Unajua hata Tundu lissu ataangalia vipengele kabla ya kusaini IGA. Ni mzalendo.
 
Mama yetu fahamu kuwa terms na conditions za mkataba ni za ajabu sana na ni mendawazimu pekee atazikubali!
Mkataba umekaa kihuni mno na unaonekana wazi kuwa wasaidizi wako kuna kitu wanakuficha. Fuatilia walio nyuma ya huu mkataba utagundua uhuni na ufisadi mtupu ka faida za matumbo yao!
 
Madam president hyo ni biashara tu. Kwa mkataba huo waende tu. Ingawa nikuambie na Kenya unakosema wameenda tayari kimenuka na hoja kubwa ni mkataba kuvunja KATIBA ya KENYA na kuondoa souverainity Yao. Mawakili wetu na wasomi walio tuongoza kuujua mkataba huu wapewe heshima yao.
 
Kwa hiyo tunatoa bandari zetu kwa bendera yetu kupata nafasi ya kupeperushwa kwenye jumba refu tu? Au kwa vile tunakimbizana na jirani badala ya maslahi mapana kwa vizazi vijavyo?

Nasema vizazi vijana maana kwa upande wa maslahi ya taifa tayari viongozi wetu mmetufelisha sana tangu kitambo, tazama leo ni zaidi ya miaka 60 ya uhuru lakin bado tunakimbizana na ukosefu wa maji salama hadi katika makao makuu ya nchi mbali na huko vijijini ambako bado tunakunywa maji pamoja na mifugo
Sizani kama team praise itaelewa
 
Back
Top Bottom