Ni kama akili zenu nyote, wewe pamoja naorodha hiyo iliyokupa 'like'; akili zenu zimeganda mahali fulani na kamwe hamuwezi kuziondoa kwenye mgando huo.Mkataba una shida gani?
Kama hadi wakati huu bado unauliza swali hilo, ina maana huamini kuwa hiyo 'IGA' ni mkataba.
Lakini pamoja na tunapokubaliana juu ya hilo, kuwa ni "Makubaliano", bado hamuoni ubovu uliomo kwenye hayo makubaliano!
Kinachotakiwa sasa, labda elekezeni akili zenu kwenye kuwaeleza wananchi wa nchi hii, kwamba "Makubaliano" hayo hayana uhusiano wowote na "Mikataba" itakayoingiwa.
Hapo mtakuwa na kazi ya kuwaambia wananchi kuwa makubaliano ya IGA yawepo au yasiwepo, haiathiri chochote katika mikataba hiyo ya HGA.
Kwa hiyo, nwasihi sasa, muelekeze akili zenu katika kuifuta IGA, ila tuendelee na HGA.
Nimeona mahali fulani ume'ni'quote', sijakusoma huko, nitakutafutia muda, maanake najua utakuwa umeacha takataka kama hizi unazoeneza kila mahali. Kwa hiyo vuta subira juu ya hilo.