Rais Samia: Sensa haitauliza kuhusu Dini ya mtu

Rais Samia: Sensa haitauliza kuhusu Dini ya mtu

Kwani umewahi kusikia chuo cha sensa popote? Hili ni jambo la kukubaliana tu
Sensa ni takwimu za idadi ya watu ndugu, inaangalia vitu kama ukuaji wake, umri, kipato n.k
Uchukuaji na uchambuzi wa takwimu ni taaluma, hata vyuoni kuna kozi hizo
 
Sensa ni takwimu za idadi ya watu ndugu, inaangalia vitu kama ukuaji wake, umri, kipato n.k
Uchukuaji na uchambuzi wa takwimu ni taaluma, hata vyuoni kuna kozi hizo
Tofautisha taaluma ya upolisi na mambo ya takwimu
Tatizo nyie ndio chanzo cha mateso yetu,
Kufelisha watoto wetu shule,
Kupeana kazi ki idini,
Kufisidi mali ya umma,
Na mengi yapo Ila tuyaache yasidishe uchungu na maumivu
Kama unaamini mko wengi si mtumie uwingi wenu kupindua matokea?
 
No, no, no
Tunataka kuhesabiwa kwa dini zetu, tujuane tu, hii itasaidia katika mgawanyo wa mambo mengi tu,
Wakati ni sasa,
Unyonge na uonevu uishe
Acha upuuzi,, unataka idadi? Wambieni kanisani kwenu mhesabiane ..
 
Rais Samia Suluhu Hassana ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa huku akisema suala jipya lililoongezwa ni swali kuhusu anuani za makazi.

Amesema hakutakuwa na swali la kuhusu dini ya mtu kwa kuwa suala hilo lilishakataliwa tangu enzi za Rais Julius Nyerere, hivyo hakutakuwa na swali la namna hiyo.

Rais ameyasema hayo akiongea na wanawake Zanzibar.

Hata swali la ukabila halitakiwi kuwepo. Muhimu ni kujua idadi ya watanzania.
 
So what??? Hii lugha umeletewa, ongea lugha yako
Unataka niongee lugha yangu uku wewe unataka tuige mambo ya nchi zingine yasiyo na faida hapa kwetu.maana mambo ya nigeria,somalia yanatuhusu nini sisi.Mara ngapi tumesikia vikundi vya kidini vikigombana na serikali kwenye baadhi ya hizo nchi zako ulizozitaja.kwahiyo unataka nasisi tuwe wajinga kama hao.
 
Kwa nini Wakristo ndio huwa wanapinga kwa nguvu zote hili suala? Wanaogopa nini? Nini kilichojificha hawataki kijulikane?
Kilichojificha ni ujinga wako uliouleta hadharani wakuwahusisha wakristo na jambo lisilowahusu.Ni kiongozi gani wakikristo aliyepinga hilo swala wakati linaratibiwa na serikali.Kwahiyo na huyu rais wasasa aliyekataa huo ujinga naye ni mkristo?
 
Hawa CCM sijui Nyerere wanamuonaje na kumchukuliaje, Nyerere alikuwa ni binadamu na alikuwa na madhaifu sana, Nyerere hakuwa mkweli kuna siku alisema angemuwahi Rais wa 2010 akiwa hai.

Suali la dini ni suali zuri katika nchi kujua watu wako wala halina mtafaruku wowote ni figure tu kama nchi unajua Tanzania kwa mfano kuna waislamu kiasi gani na wakiristo kiasi gaini labda ambao hawana dini ni kiasi gani kujua mahitaji vile vile katika shughuli za maendeleo.

Hili suali nchi nyingi wanauliza, hata katika CV lakini mafomu mingi ya online lipo hili suali lina umuhimu katika mahitaji na sio kuwagawa watu.

Lakini ukija kwa wanaokataa sijui tuseme ni hofu au kitu gani sijuI au ndio hizo fikira za Nyerere labda wanaogopa waislamu kuonekana ni wengi kuliko wakiristo maana aslimia 99% wanaopinga suali hili la dini ni wakristo, hawa watu wana hofu sana kujiona wako kidogo.

Nadhani kuna watu hawatakubali kuhesabiwa kama hili suali halipo
Kwa akili finyu kama hizi sababu ulizo orodhesha , nafikiri ndio maana wameamuwa waondoe hicho kipengele
 
Hili suali nchi nyingi wanauliza, hata katika CV lakini mafomu mingi ya online lipo hili suali lina umuhimu katika mahitaji na sio kuwagawa watu.
Hizo CV zenu mnazojaza marital status, na Religion .. ndio maana zinawanyima kazi vijana, katika kampuni zinazojielewi ni mifumo ya uandishi wa cv wa kizamani sana ..

Zipo details za muhimu zaidi ,zitakazo changia kumpa mtu kazi,
Same kwenye sensa yapo maswali muhimu zaidi
 
Hili jibu litakuja tukishajua idadi ya waislamu na Nchi itajua mahitaji ya waislamu, kwa mfano waislamu wapewe fursa ya kuanzisha mahkama zao (za kikadhi) kwa ajili ya kutatua changamoto zao na kupata haki zao kwa mujibu wa dini yao ili kuipunguzia Nchi kutatua migogoro ya waislamu ambayo Mahkama za sasa hazina nguvu kisheria na haziko specified.

sijisikii aibu wala fedheha kuanza kuonekana muislamu., unajua shida ni kwamba Wakiristo wao imani yao sijuwi ni kwanini hawajiamini, linapokuja suala lenye maslahi za kidini wao dini yao wanataka wawe kimya ambapo ni tofauti na imani nyengine.
kwani kuanzisha hiyo mahakama ni mpaka mjue mpo wangapi?? we huoni watu wanajaa misikitini na kwenye swala ya Eid?, kama mnataka kuanzisha anzisheni lakini sio kwa sababu ya kutaka kujua mpo wangapi

leo mtaanza tujue tupo wangapi, kesho mtafata tujue idadi ya wasunni, washia au wahamadia, basi msunni aanzishe mahakama yake na nyie mahakama yenu basi vurugu tupu
 
Kwa sababu wakiristo hawashughuliki na dini yao mana hawana uhakika unataka na waislamu pia wawe hivyo? Nchi nyingi duniani zimeangalia mahitaji ya waislamu kwa sababu ndio watu wengi walionao katika nchi yao hakukuwa na namna,

Leo nyerere mchonga meno kawapangia maisha ya baadae na munamuabudu ata akikwambie 2+1 = 5 basi nyoote mtasema ndiooo
issue ni moja tu, jihesabuni. Anzeni kwenye ngazi ya familia mpaka kwenye misikiti na kwa wakristo mkitaka kujihesabu anzeni kwenye vipaimara na ubatizo, ila sisi Tanzania tutakuhesabu kama mwananchi.
 
Hili jibu litakuja tukishajua idadi ya waislamu na Nchi itajua mahitaji ya waislamu, kwa mfano waislamu wapewe fursa ya kuanzisha mahkama zao (za kikadhi) kwa ajili ya kutatua changamoto zao na kupata haki zao kwa mujibu wa dini yao ili kuipunguzia Nchi kutatua migogoro ya waislamu ambayo Mahkama za sasa hazina nguvu kisheria na haziko specified.
Msingi wa haya madai ni kukosa uwezo wa kujiendesha, serikali iliweka wazi, anzisheni hizo mahakama na mzigharamie wenyewe.

Unataka Mfumo wa Sharia uwe sehemu ya utawala wa serikali, reference ikiwa mbona UINGEREZA blah blah, UK wanao ushoga na usagaji pia kwenye taratibu zao, mnaweza ku-rejea hilo?

Mahitaji ya Uislamu yatambuliwe na serikali kwa lipi?

Ni wazi utakuwa ama umewahi kufika nchi za kiarabu kiislamu au hata kusikia lifestyle yao, kama isingekuwa kwa upanga, zaidi ya 50% ya wakazi wa kule wangeachana na Uislamu, achilia mbali kuwa hawana tofauti na ufirauni kabisa.
 
Swali la dini litasaidia kuzaana baada ya wachache kutokubali kupitwa, na wengi kutokubali kukaribiwa, itakuwa'marathon race' kwenye uzazi!
 
Msingi wa haya madai ni kukosa uwezo wa kujiendesha, serikali iliweka wazi, anzisheni hizo mahakama na mzigharamie wenyewe.

Unataka Mfumo wa Sharia uwe sehemu ya utawala wa serikali, reference ikiwa mbona UINGEREZA blah blah, UK wanao ushoga na usagaji pia kwenye taratibu zao, mnaweza ku-rejea hilo?

Mahitaji ya Uislamu yatambuliwe na serikali kwa lipi?

Ni wazi utakuwa ama umewahi kufika nchi za kiarabu kiislamu au hata kusikia lifestyle yao, kama isingekuwa kwa upanga, zaidi ya 50% ya wakazi wa kule wangeachana na Uislamu, achilia mbali kuwa hawana tofauti na ufirauni kabisa.
Jukumu la serikali iliyomadarakani moja ni kutimiza mahitaji ya watu wako kwa vyovyote vile, shida kubwa ni kwamba ikija issue inayowahusu waislamu inaonekana kama ni dharura binafsi n kuonekana kama labda kikundi kidogo cha watu wenye mahitaji hayo na serikali kutaka kujiweka pembeni nayo. huu ni udhaifu mkubwa wa kiutekelezaj kw serikali
 
Ni wazi utakuwa ama umewahi kufika nchi za kiarabu kiislamu au hata kusikia lifestyle yao, kama isingekuwa kwa upanga, zaidi ya 50% ya wakazi wa kule wangeachana na Uislamu, ach
Kwanza uislamu sio uarabu,
Dini hii ni ya wote, kama ambavyo ukristo sio uzungu,
Kwamba upanga ndio umesimamisha dini sio kweli, kwa sababu mafundisho yenyewe yanasema "hakuna kulazimishana katika dini"
Ukiona wanakulazimisha huo sio uislamu,
Jukumu lao ni kukunasihi tu ukitaka uwe usipitaka wanakuombea mungu akuongoze,
Na ukichagua kupotea hiyo ni shauri yako lakini halazimishwi mtu,
Kuhusu ufirauni huo ndio udhaifu wa mwanadamu, kwani sie sio malaika,
Kama ambavyo askofu, padri au shehe anaweza kubaka au kuzini
Kwa hiyo udhaifu ni wa mwanadamu na utukufu ni ALLAH pekee
 
Back
Top Bottom