Rais Samia: Serikali imempatia Mzee Mwinyi zawadi ya gari aina ya Benz ya chini

Hivi mnajua wale wageni wa SADC zile gari zote ziliagizwa mpya 0km na kuwachukua airport na kuwarudisha baada ya hapo zililala tu.inawezekana kampa moja kati ya zile.
Ushahidi? Acha uzushi kutetea ujinga wako
 
Naona zile bilioni 1.2 kwa mwezi za "matumizi binafsi ya Rais" enzi za Mwendazake zimeanza kufanyiwa kazi pia katika awamu hii, hakika CCM ni ile ile.
ni 80mln bana acha kutia watu moto[emoji16]
 
Wewe ni dogg sana, Mwinyi anastahili zaidi ya hiyo Benz, benz zenyewe zimejaa Ikulu kwanini asipewe moja mtu muhimu kama huyu?
 

Subiri kwanza Mkuu ni mapema
 
huzijui benz mzee,au unadhani ni compressor ile[emoji23][emoji23].
 
Umejuaje kama ni jipya?
Huenda amepewa gari kuukuu
 
Afadhali mama amesema “serikali imetoa …”, angekuwa ni yule jamaa ungesikia “mimi nimempa….”
kwani mama si ndio serikali!!!au wewe unaweza kupinga???
 
Una akili kijana
 
Jambo jema ,Sana kutoa ni moyo japo sijajua ametoa mfukoni au ni kwa niaba ya wananchi?

But all ni all mama wenda ana moyo mzuri kufika mwakani mama SSH binafsi nitafuata taratibu nitakuja kukusalimia hapo CHAMWINO, Sasa isije fika mda then ulishabadilika Kama mwendazake, nishindwe kunywa soda maana tumeyaona na tutayasimulia wajukuu ya mwendazake , lakin pia ajengewe sanam ili kipindi hicho wajukuu wetu wawapo wanasimuliwa Basi wafanye na tour
 
Ni haki yake Mzee mwinyi kama rais mstaafu kuhudumiwa na serikali mpaka mwisho wa uhai wake.unashangaa benzi ya mil450: je unajua bei ya vx v8 new model?
 
Majuzi hapa Magufuli kamjengea Mzee Mwinyi bonge la "Hekalu"

Leo Samia anatoa Zawadi ya Benz la Mamilioni

Hivi haya Mambo ndo yanatatua shida na kero za wananchi au?

Mwinyi ana pensheni ya Mamilioni ya fedha, Mwanae ni rais, watoto wake ni wabunge, Hivi bado anahitaji Mihela yote hiyo kodi za wananchi masikini kwa ajili ya mavituvitu kama hayo?

Naona tumeanza kutumia fedha za wananchi kama pesa za familia. Mambo ya ajabu sana haya!
 
Kuna Rummors kuwa Maza ni Mtoto wa Mzee Mwinyi.
Kamzawadia Babaye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…