Rais Samia: Sisi tunalumbana kuhusu Bandari, wenzetu wanatumia fursa

Rais Samia: Sisi tunalumbana kuhusu Bandari, wenzetu wanatumia fursa

🤣🤣🤣na watu wa kyerwa mmeongea eeh,sisi mbeya tushamtanguliza mwakabusi na nshala🙏
 
Huo udhaifu wa kikatiba uliopo ambao anaweza kuutumia kunyima wananchi uhuru wa kuongea ni upi?

Ni sehemu ipi ya katiba ambapo huo udhaifu upo?

Udhaifu pekee uliopo ni wa sisi wananchi kuwa ni waoga katika kulinda na kutetea haki zetu.
Katiba inamruhusu kufanya kosa lolote muda wowote na hatashitakiwa wala kuhojiwa na chombo chochote.
 
Mh Rais,

Kitu kikubwa sana ulichoshinda pamoja na changamoto zilizojitokeza ni kuruhusu mjadala juu ya mkataba wa DP World. Huu ni uhuru wa kikatiba lakini tunajua upo udhaifu wa kikatiba ambao ukiamua kuutumia kikamilifu tusingepata uhuru wa kiwango hiki.

Kwahili lazima tukusifu kukubali mawe yanayorushwa kila kona kwako ingawa baadhi ya wasaidizi wako ni kama wamefikia ukomo wa uvumilivu na badala kukazana na hoja sasa wameamua kutumia njia zisizo salama.

Lakini mkuu wetu kwanini vitisho kwa wanaohoji juu ya mkataba wa Dp world?

Kwanini kukamatwa kwa akina Mdude Nyangali?

Kuacha mjadala kushika hatamu na kuamua hatma ya taifa ni kitu cha pekee umefanya na usiruhusu machawa kuvuruga jambo hili jema sana kwako.

Hii ni sauti ya kiungwana kutoka Kaisho, Kyerwa! Asante sana Mh Rais!
Kama yaliyofanyika Mbeya hayana baraka zake, haitapita wiki, utasikia RPC wa Mbeya amehamishiwa makao makuu. Ukiona kimya, ujue Rais amebariki.
 
Katiba inamruhusu kufanya kosa lolote muda wowote na hatashitakiwa wala kuhojiwa na chombo chochote.
Weka hapa hiyo sehemu ya katiba inayomruhusu kufanya hivyo.

Huu ndo ubwege na ujuha ninaouzungumzia hapa!!

Mtu hana hiyo haki ya kufanya yote hayo lakini mpo mnaoamini anaweza akafanya hivyo!!
 
Kama yaliyofanyika Mbeya hayana baraka zake, haitapita wiki, utasikia RPC wa Mbeya amehamishiwa makao makuu. Ukiona kimya, ujue Rais amebariki.
Asiruhusu lolote limtokee Mdude! Tuna imani nae mkuu wetu.
 
Mdude amekatwa kumbe?
ec6b22d7830731dfb288ab339b6bb6f7.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujue kwanza kisa cha kukamatwa maada mdude historia yake tunaijua
Kama ndio vile basi tuache
Hana kosa lolote lakini huu mwanya unaweza kutumika vibaya dhidi yake.
 
Hana kosa lolote lakini huu mwanya unaweza kutumika vibaya dhidi yake.

Inawezekana hana kosa ila anasaidia mambo ya kitaifa
Sio wote wanaokamatwa na Polisi ni wahalifu
Wengine wanakuwa kwenye kuwasaidia polisi, wengine wanakuwa wamesaidiwa kuwa salama
 
Samia ni kweli kabisa anastahili pongezi lakini anatakiwa kuwapiga STOP mapolisi waache harassment dhidi ya critics wake.
 
Samia ni kweli kabisa anastahili pongezi lakini anatakiwa kuwapiga STOP mapolisi waache harassment dhidi ya critics wake.
Hastahili pongezi zozote kwa kuacha kuibaka katiba!

Kumpa pongezi Samia ni sawa na kumpongeza jambazi ambaye hajakupora mali yako!

Jambazi hastahili pongezi yoyote ile kwa kuacha kuwa jambazi.

Ni akili gani hizo mlizonazo nyinyi????
 
Amekamatwa na tunaomba aachiwe haraka!
Kwa nini kakamatwa na si wewe, mimi au ndugu zetu wengine? Tujue chanzo cha kukamatwa then tuanze kujadili. #Yote kwa yote nakupongeza kutambua uvumilivu mkubwa wa Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu dhidi ya wakosoaji. Basi tuutumie uhuru vizuri.🙏🙏🙏
 
Hastahili pongezi zozote kwa kuacha kuibaka katiba!

Kumpa pongezi Samia ni sawa na kumpongeza jambazi ambaye hajakupora mali yako!

Jambazi hastahili pongezi yoyote ile kwa kuacha kuwa jambazi.

Ni akili gani hizo mlizonazo nyinyi????
Sema, jambazi baadaye likuvamia na kuiba na kuua ndio utajua jambazi ni mtu mbaya.
 
Sasa lijitu libaya likiacha kufanya ubaya wake ndo linastahilli pongezi?
Serikali kazi yake ni kutetea maslahi ya nchi Ila sasa hivi genge, kundi dogo la familia zao na washkaji zao wanatetea maslahi yao. Rushwa. Wamepewa 10% walipo kuwa Dubai.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule Ikulu jijini Dar es Es Salaam leo tarehe 14 Julai, 2023

RAIS SAMIA: SISI TUNALUMBANA KUHUSU BANDARI, WENZETU WANATUMIA FURSA
Rais wa Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati wa kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es es Salaam, leo Julai 14, 2023 ambapo amesisitiza kuhusu kutumia fursa za kupata maendeleo pindi zinapopatikana.

RAIS SAMIA: KILA MABADILIKO YANA UGUMU WAKE
Rais wa Samia Suluhu Hassan anasema “Mkiwa na nia safi na ya kujenga Nchi msiogope kuja na mawazo ya kubadilisha mwekeleo wa Nchi, kila mabadiliko yana ugumu wake, hakuna mabadiliko marahisi.”

Ameongeza “Watu wakizoea kushoto ukiwaambia geuka kulia watalalamika, msiogope kuna na madiliko ya uelekeo wa Nchi yetu.”

Hatuna Rais Tanganyika.
 
Tuna genge la wahuni, likiongozwa na Rais kilaza, wamezamilia kuuza nchi. Kuingia Mikataba ya hovyo.
 
Rais akumbuke ya mwaka 2019 waziri wa uchukuzi Dr. Isack Kamwelwe na mkurugenzi wa TCAA mwanasheria Hamza Johari walipiga vita sana wawekezaji toka nje.

Huyu mwanasheria Hamza Johari na yule Dr. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe walivuruga sekta binafsi ya ndege fastjet 2019 - 2020 kwa kuapa kuwaondoa FastJet

Sasa mwaka 2023 tena mwanasheria Hamza Johari na Prof. Makame Mnyaa Mbawara wanataka kuvuruga bandari zetu kwa kujidai wanaipenda sekta binafsi itaweza ....

TOKA MAKTABA :

December 19, 2018
Dar es Salaam, Tanzania

Waziri ashangilia matatizo ya Fastjet

Waziri Isaack Kamwelwe aliibua sakata la Fastjet mbele ya Rais Magufuli “…kuna mfanyabiashara mmoja anayejulikana kwa jina la Fastjet...juzi alitusumbua…alitubip…tumempigia…”

Source : Azam TV
 
Back
Top Bottom