Rais Samia: Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa

Rais Samia: Siyo vibaya viongozi wa dini kuwa wanasiasa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 Mjini Morogoro wakati akifungua mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT) aliposema wakati mwingine dini na siasa vinaenda sambamba.

Amesema licha ya kuwa unaweza kutumikia dini na kuwa mwanasiasa, lakini vibaya unapotumia siasa kwenye dini. Amewaomba viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika kudumisha amani na usalama wa nchi uliopo.

Amesema ni nafasi ya viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yakitaifa ikiwemo suala la kuhesabiwa sensa linalotarajia kufanyika mwezi Agosti mwakani.

"Nawasihi viongozi wa dini kuwasihi wananchi kuachana na imani potofu na kushiriki kwenye sensa, suala la sensa lipo hadi kwenye vitabu vya dini na hivyo sio suala geni kwetu," amesema.

Rais Samia pia amewataka viongozi wa dini kote nchini kuhubiri amani, upendo na mshikamano huku wakizidi kuliombea Taifa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Katika risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT), Baba Askofu Dk. Alinikisa Cheyo, ameomba serikali kuondoa kodi ya mapato (Income Tax) kwenye shule na huduma za afya zinazotolewa na taasisi za kidini nchini.

“Tunaiomba Serikali ifikirie kuziondolea Taasisi za kanisa kodi za mapato (income tax) ili taasisi hizo ziweze kujiendesha kwani hazipati faida kubwa na ile faida ndogo inayoipata inatumika kughramia uendeshaji wa huduma hizo,” amesema Askofu Cheyo.

Chanzo: Nipashe
 
Picha anayoitoa Rais hapa ni kwamba kila litakalozungumzwa na viongozi wa dini kwenye kuionya serikali yake atalichukulia kisiasa.

Mfano viongozi wa dini wakisema "Katiba Mpya" kwa Samia hiyo ni propaganda tu ya kisiasa, wakisema tena; "tuheshimu sheria zetu tulizojiwekea" nayo kwake ni kauli ya kisiasa tu.

Simply ametafuta njia rahisi ya kuwafunga midomo viongozi wa dini, mama ameshaanza kuizoea ikulu sasa.
 
Mama anajilika sana na makafiri aisee
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Jamani katiba mpya ndiyo suluhisho.akikubali katiba mpya ndio itakayoleta demokrasia ya kweli nchini.mtake au msitake.
 
Rais Samia amewataka viongozi wa dini kuacha kutumia dini kufanya siasa kwani jambo hilo siyo sawa.

Rais Samia amesema siyo vibaya kwa viongozi wa dini wa kuwa wanasiasa lakini ni jambo baya kwa viongozi wa dini kutumia dini zao kufanya siasa.

Source: ITV habari

Nawasalimu kwa jina la JMT.
 
Jamani katiba mpya ndiyo suluhisho.akikubali katiba mpya ndio itakayoleta demokrasia ya kweli nchini.mtake au msitake.
Yaaani kugsragazwa kwaviongozi waufipani kwenye majimbo ndo iwesababu ya kuwahadaa wananchi eti wanataka katiba mpyaa??
 
"UAMSHO" na Askofu Bagonza ujumbe UMEWAFIKIA.....

#KaziIendelee
 
Akina bagonza hao , kila sku kurelate mafungu ya biblia kujipatia umaarufu kisiasa.....naona mama anaupiga mwingi sana
 
Yeye mwenyewe anajifanya swala 5 huku matendo yake yanakataa
Ulimsikiliza vyema?!!

Amesema kuwa UNAWEZA KUFANYA SIASA KWA IMANI YAKO YA KIDINI MOYONI(mtu binafsi)....

Swala zake 5 hazimuondolei RUNGU LAKE LA KUWASHUGHULIKIA wenye CHOKOCHOKO na WACHOCHEZI.......

#KaziIendelee
 
Akina bagonza hao , kila sku kurelate mafungu ya biblia kujipatia umaarufu kisiasa.....naona mama anaupiga mwingi sana
Bagonza na UAMSHO....

Message sent and delivered....

#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom