Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Ripoti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ametoa agizo la kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari(TPA) kutokana ubadhirifu mkubwa unaoikumba mamlaka hiyo.

Mkurugenzi mkuu huyo anasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa kina.
Mama ameanza kutufuta machozi siyo bure, anaanza kudhihirisha kauli yake, in raising wa jmt
 
Huku akisimanga awamu zilizopita hadharani kuwa mambo yalofanyika hadi unashangaa kama viongozi walikuwepo. Haya sasa mficha maradhi........
Mbona Magu alikuwa anateuwa na kutumbua wasipotekeleza wajibu!!? au hili swala umelisahau.....kwa ufupi wa fikra zako
 
I second you. JPM kwa uzalendo alikua namba moja, sidhani kama kuna Rais aliyekua na uchungu na hii nchi kama yule mzee

Tatizo lake kubwa alikua anataka kutengeneza "Cult personality" kwamba watu wote waone juhudi zake yeye kama yeye binafsi sio serikali kwa ujumla. Na watoto wa mjini walilijua hilo wakawa wananata na biti hapo hapo kumpamba huku wanafanya mitikasi yao
Huo ndio udhaifu mkubwa ambao kwa ngazi ya raisi hakutakiwa kuwa nao. Ile ni taasisi lakini kama ulivyosema kila kitu alitaka aonekane yeye.
 
ukisema hivo unakosea kiongozi ufanisi mbaya wa kiongozi sio reflection ya aliyemchagua huo ni ubadhilifu wa kiongozi mwenyewe
Kama sio reflection ya kiongozi aliomteua kwanini magufuli alikuwa anakesha kutumbua na kuwaminisha watanzania kuwa yeye si fisadi ilhali kazungukwa na wateule fisadi?
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Ripoti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ametoa agizo la kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari(TPA) kutokana ubadhirifu mkubwa unaoikumba mamlaka hiyo.

Mkurugenzi mkuu huyo anasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa kina.
Jafo naye kaonywa vikali sana kuhusu tamisemi, ila hayo yote c yalitokea kwenye utawala wa jiwe
 
Unachotaka kusema hiyo report ya cag imeandaliwa mwezi huu tar 17 march baada ya jpm kufariki?
Unachotaka kusema hiyo report ya cag imeandaliwa mwezi huu tar 17 march baada ya jpm kufariki?
Mkuu tusubiri moto wa bunge na ripoti ya CAG mwakani. Hii imeumauma sehemu nyingi maana iliandakuwa kumpendeza bwana jiwe.
Ndio maana kwenye recommandation ilishughulikia wadogo, wakubwa hawakuguswa.
 
Kwa JPM haikuwa taasisi, ilikuwa ni one man show!


Kwanini mnasahahu kuwa makamu wa Raisi kazi yake kuu ni kutembea na mkasi kukata utepe na sio kutoa maagizo? Tena serekaki ya jiwe labda akutume, kama hajakutuma uthubutu kutoa amri yeyote.


Kama Rais Samia Suluhu Hassan alikiri kufundishwa na kumudu kazi zake zote kama makamu wa JPM na hadi kwenye maombolezo akaendelea kukiri kwamba JPM alikua kaka na mwalimu wake kwenye kazi...

Wewe ni nani nikusikilize unaposema ilikua one man show



Jikalieni kimya hapo kwenye foleni huku mkisubiri sindano za mama ziwaingie
 
Ukiangalia jinsi rais alivyomsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA ni uamuzi aliouchukua hapohapo baada ya kusomewa ripoti na CAG,sasa huyu kigogo alijuaje???..au kulikuwa na mipango ya mkurugenzi kutimuliwa kabla ya ripoti kusomwa??..huenda huyu kigogo anafanya kazi vizuri kabisa na serikali,baadhi ya viongozi wakubwa serikalini bila mzee pombe kujua..yaani rais alikuwa anazungukwa na wateuwa wake kwa maslahi Fulani!..
 
Tukumbushe pale ambapo kigogo alitabili mtu kutumbuliwa na JPM
Mm mambo ya kigogo siyazingatii sana. Halafu suala la kutumbua nafikiri Chuma JPM hata yeye wakati mwingine alikuwa hajui kuwa atatumbua. Maamuzi aliyafanya papo kwa hapo.

Mama inaonekana unafanyika uchunguzi na hapo ni rahisi kujua kuwa unaweza tumbuliwa au wanahabari wakazipata mapema.
 
Back
Top Bottom