Rais Samia Suluhu ana emotional intelligence, utulivu wa hali ya juu

Tofautisha imbecile na emotional intelligence mshabiki wewe
 
Ongezea hivyo vitu ndivyo hu define Busta ya mtu,ukiweza kudhibiti hisia hasi ujue wewe ni mshindi.

Watu dizaini ya kina Mwendazake,Lisu, Mwambukusi,Heche,Lema,Kitima na wengine wa aina hiyo kamwe hawafai hata kidogo kuwa Viongozi.

Ukiacha maamuzi ya ajabu ajabu na ego,wanaweza kuleta disaster kubwa na wakaishia kuwa makatili.

Samia anaonesha maana ya kuwa Kiongozi japo nashauri awabane kidogo,hapa Africa the so called Demokrasia na uhuru wa maoni Bado havitufai.
 
Binafsi nafikiri ameamua kuwa kimya ili awajue wanafiki vizuri.

Japo Mkataba ushasonga mbele
Kwani ukimya wake umeanzia Kwa jambo la DP World pekee? Yamepita mangapi kuanzia chanjo za uviko 19,Maasai wa Ngorongoro,mambo ya tozo nk

Umewahi kumsikia anapayuka? Sehemu pekee iliyomfanya akakasirika na kuongea ndivyo sivyo ni Ile siku ya ripoti ya CAG tuu.
 
Hii ajenda kubwa hapa taifani imeanza lini na mpaka sasa ni muda gani umepita ?

Na hata akijibu sasa muda huu naandika hio haitafanya nimuondoe katika kundi la viongozi wenye viburi
We Jamaa una matatizo,mtu mwenye kiburi hawezi.kupa nafasi tena atakuumiza ,so acha ujinga.
 
Sa100 na intelligence ni sawa na maji na mafuta. Katika kundi la vilaza yupo.
 
Ana sifa nyingi za uongozi ila kwenye usikivu anafeli kidogo huo mkataba kweni haurekebishiki?
Usikivj upi aliofeli? Hata hili la DP World atawapa muafaka kama kawaida hajawahi feli Kwa jambo lolote.

Vuta subira utapata jibu sio lazima limfurahishe Kila mtu
 
Wajinga wanataka tuu kumpima.Rais Samia kwenye issue ndogo ya DP World,kwangu naona ni ndogo ila ukitaka kujua ana akili wewe angalia tuu amebadili uelekeo wa vitu vingapi vya Jiwe katikati ya Wahafidhina na makali ya propaganda za Utawala wa Jiwe ,yote kayafanua ndani ya mda mfupi sana.

Samia mpaka Sasa ana define Demokrasia Kwa vitendo

Ana define uchumi na Biashara Kwa vitendo.

Ana define muelekeo wa Sera ya Nje ya diplomasia Kwa vitendo

Ana define sera Mpya ya Kilimo Kwa vitendo

Na ana define mambo ya Kijamii Kwa vitendo kuanzia kubadili sera ya Elimu Hadi Maji,Afya,Barabara Kila Kijiji nk

Mwisho juzi tuu hapo umetoka kuona ambavyo ameridhia kufutilia mbali mashirika yasiyo na Ufanisi ,kupunguza urasimu nk

Yote hii ni ku shape muelekeo Mpya wa siasa na Uchumi wa Nchi,wenye akili ndio wanaweza elewa haya mambo ila wale short-sighted hawajui chochote.
 
Samia hana uwezo wa kuongoza nchi. Acheni kupaka paka rangi.
 
Hana lolote wanampa kichwa,yaani wewe nyumbani kwako watoto wanazozana wewe unakaa kimya kama mzazi,yaani ata kupiga mkwara huwezi.
Kama ni mtulivu basi tungeona busara yake kabla ya kusaini ule mkataba wa Kimangungo.
 
Na ana-define ripoti za CAG kwa vitendo,kwa kusema Stupid kwa vibaka!
 
Muhubiri 4:13
Afadhali Kijana masikini mwenye hekima kuliko Mfalme Mzee mpumbavu ambaye hasikilizi shauri jema.
 
Na ana-define ripoti za CAG kwa vitendo,kwa kusema Stupid kwa vibaka!
Ripoti ya CAG sio amri ya Mahakama,wanaotakiwa kushughulikiwa Kwa kuwajibika watawajibika na wengine waliwajibishwa ikiwemo kuvunjwa Bodi na kufikishwa Mahakamani.

Hujasikia wahasibu wa Jiji wakifikishwa Mahakamani siku za karibuni? Wahasywa Mahakama Je?

Acha chuki wewe hater,Samia kawaccha wengi sana mbali kuleeee.
 

hili sakata limeanza lini? Tangu mwanzo badala ya yeye kusikiliza wakosoaji wanakosoa nini, yeye akatuma machawa wake wa ccm kuja kuupa promo huo mkataba. Umeona kiongozi yeyote wa ccm au wa serikali akijibu hoja za wakosoaji zaidi ya kuupigia promo?

it was simple, kusikiliza hao wakosoaji wanasema nini na kujibu hoja zao maana sio machizi kusema hawastahili kusikilizwa. Lakini two month now halafu wewe unakuja kumpa sifa za kijinga hapa, upo sawa kweli?

mpaka wakati huu hastahili hizi sifa za kinafiki mnazompa.

nakuonaga una akili ila hii mada yako sioni tofauti yako na pasco mayala.
 
Hoja ni kuwa marekebisho yafanyike.
Hoja za msingi zisikilizwe. Hasa hoja za wenye Akili. Kwa sababu jamii yetu Watu wengi bado wapo Gizani.
Na wengine wanaunga mkono hoja kishabiki

kama unalijua hili na hajaonesha uelekeo wowote miezi miwili sasa anaishia kusema nakaa kimya, utasemaje ana utulivu kama sio kiburi hiki??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…