Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Hapa jukwaani au hapa duniani? Mi nahitaji kuwa chawa japo nionje kidogo mema ya nchi kabla sijafa.

Mema tutayaonja katika uzima wa milele if at all you are on a right truck to be there after this world's life.
 
Mpango yupi tena jamani?
Si tulikubaliana mama aweke safu mpya na team Msoga wawemo?
Mpango alivutwa na nani kurudi bongo na kupewa majukumu? Kisha alikuwa mshauri wa nani masuala ya uchumi? Nani alimuweka kusimamia tume ya mipango?
 
Msaada kwenye tuta. Kama VP ambaye ni running mate wa rais huwa si mbunge (au ana jimbo), je kutakuwa na uchaguzi mdogo Buhigwe - Kigoma kwa ajili nafasi hiyo itakuwa wazi au ?
 
Mlimfikiri mtampangia Rais Mama Samia.
Tumpangie sisi kama nani? By the way, mimi na akina nani? Mimi ni Mtanzania tu Mzalendo wa Nchi yangu, na adui namba 1 wa @ccm nchini!

Hamchelewi nyinyi MATAGA kusema na mimi niko Ufipa kwa akina John Mnyika!
 
Jamani baadhi ya wabunge mnapaswa mumuadress Samia kama rais Samia siyo Mama Samia.
Tokea akiwa vice alikua akiitwa Mama,
Nyerere alikua anaitwa mwalimu je kuna ubaya napo nadhani mama ni heshima tu na wala sio kupunguza ukuu wake Kama Rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama
 
Timu Msoga imeshatoa kiongozi wa juu hivyo timu nyingine nazo zinapewa nafasi.
Yap 50/50,kikubwa hawa wote walifanya kazi vema na hayati JPM,cha umuhimu wakatekeleze vyema ilani ya CCM Tanzania tusonge mbele.
 
Wakuu, hivi zile nafasi za ubunge wa kuteuliwa na Raisi zilibaki ngapi?
Je walioteuliwa na mwenda zake wanatambuliwa kisheria? Maana aliyewateuwa keshatembea mbele
Polepole naona kakaa kimya sana
 
Msaada kwenye tuta. Kama VP ambaye ni running mate wa rais huwa si mbunge (au ana jimbo), je kutakuwa na uchaguzi mdogo Buhigwe - Kigoma kwa ajili nafasi hiyo itakuwa wazi au ?
Wahi tu mkuu ukachukue fomu! Jimbo liko wazi hilo.
 
Yani hata uwezo wa ku analyze mambo huna...wewe ni chuki tu..sasa mpango ni legacy ya nani ? Alikuwa mtu anaaminiwa na nani? Mpango ameletwa na magufuli.
Mpango katolewa WB na JK, akawa mshauri wake wa masuala ya kiuchumi, akamuweka kusimamia tume ya mipango huko kwenye BRN. Ilikuwa ni tabia ya JK kuwarudisha wataalamu wetu walionje waje kujenga nchi. Alishakuwa anaranda Ikulu akiwa na Jk.
 
Ndio basi tena, yale matrilioni sasa yatakuwa salama...Hakuna mtu atachunguza HAZINA wakati aliyekuwa waziri wa fedha kawa MAKAMU WA RAIS
 
Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai akisoma ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema..

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Soma > Wasifu wa Dkt. Philip Isdori Mpango






Dk Philip Mpango alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Hata hivyo, hadi sasa taarifa zake za elimu ya msingi, sekondari na shahada za awali za chuo kikuu hazijapatikana naye amekuwa vikaoni Dodoma muda mrefu na alishindwa kuzitoa kwa wakati.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Taarifa zake za shule za msingi hazijapatikana kwa sababu alisoma kongo
 
Tunategemea wabunge 356 mliopo mtapiga kura za ndiyo ili kuthibitisha Jina la MH.Philip Mpango. Tunawaomba Mafikizolo, Inzile na Gweregwere msiendeleze yale masuala yenu kwenye zoezi hili.
 
Back
Top Bottom