Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Angalau ametoa ule mkanganyiko, japo ni awamu ya sita lakini ilani inatumika ya awamu ya tano au anaandaa ya awamu yake, niweke sawa kidogo hapo chief.
Kwani Zanzibar alipouwawa Karume Sr na kuingia Jumbe walibadili Ilani?
 
Hapo mama yetu amekosea

Awamu ya 6 kivipi? Na Majaliwa ni waziri mkuu wa serikali ya ngapi?
Samia ni Rais wa 6, lakini serikali ya awamu ya 5
 
Hapana.

Haiwezi kuwa :"serikali ya Awamu ya Sita."

Wananchi bado hawajapiga kura kuiweka serikali hii madarakani.

Awamu ya Sita inaanza 2025; baada ya iliyopo sasa "Awamu ya Tano" kumaliza muda wake.

Mama asiachwe kuendeleza kosa hili.

Akitaka Serikali yake ya Awamu ya Sita, asubiri kuingia ulingoni 2025.
 
Awamu bado Ni ya tano.Awamu ya tano iliisha lini?

Awamu ya uraisi Tanzania ni miaka kumi, siyo mitano .

MH.Samia bado anahudumu ktk awamu ya tano akiwa Rais wa 6.

Awamu ya tano inakamilika 2025.
Huwez kuhesabu awamu kwa miaka b asi nyerere akiongoza kea miaka 22 hvyo alikjwa na awamu ngapi
Awamu inahesabika kwA kipindi Cha uongozi wa mtu
 
Nakubaliana kupingana na wewe...awamu ni term ya Uongozi..Yani ni nyakati kwa namna nyingine tunaweza kusema..Yaya nyakati hii BADO ni ya awamu ya tano yenye Serikali ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ..mwaka 2025 ikigombea akashinda anakuwa Rais wa 6 katika awamu ya Sita Kama atakuwa Rais Mwingine akishinda anakuwa Rais wa Saba katika awamu ya Sita..Angalia Marekani ndio utaelewa ..
Uongo
Rais Tz anapesa mihula miwili ya uongozi yenye kipindi Cha miaka mitano
Anaweza kuongoza kea miaka 5 asiendelee awamu yake imepita
 
MH Rais amekosea..yeye ni Rais wa 6 katika awamu ya Tano..kila awamu inakuwa na vipindi viwili...akigombea mwaka 2025 atakuwa Rais wa 6 katika awamu ya 6 ..mwaka 2030 itakuwa Serikali ya awamu ya Sita Rais wa Saba ..hivyo hivyo kadri itakavyoenda
Kwa mfano Tundu Lisu angeshinda uchaguzi ulopita angekuwa rais Wa awamu ya ngapi!?
 
Neno awam halina mantiki kwa muktadha wa senario iliyojitokeza baada ya Incumbent kufariki(R.I.P JPM)
Kwa ufupi kama miaka ingekua ni awam, je baba wa Taifa alikua na awamu 2 au 3?
Kwa lugha rahisini Rais(mtu) wa 6 kama nchi tukiwa Tanzania Huru, hayo mengine ya awamu labda kwny chama chao
Naona unachanganya matikiti na matango,tunaita awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kutokana na kuwa kwa kipindi chote cha utawala wake yeye ndie alikuwa raisi pekee na ndio maana tunasema kipindi cha utawala wake wote awamu ya kwanza,alipokuja Mwinyi katawala miaka 10 hiyo ni awamu ya pili na vivyo hivyo kwa kipindi hiki ni awamu ya tano hadi 2025 ndio atakayekuwa raisi atakuwa wa awamu ya sita. Mambo ya kusema tukiwa huru ni yako na familia yako Tanzania tumekuwa huru kuanzia 1961 pale bendera ya mkoloni iliposhushwa na bendera ya Tanganyika ikapandishwa juu tena kileleni mwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Nyirenda.
 
Kuna namna mbili za kuwa raisi Tanzania kulingana na katiba. Si uchaguzi tu. Mbona mambo madogo tu haya hayaitaji akili kubwa. Awamu inahesabiwa kwa raisi si miaka. Nyerere alitawala awamu ngapi kama awamu ni miaka? Kwann tupo awamu ya tano?
Jibu ni rahisi tu sababu ni utawala wa awamu ya 5
 
Ilikuwa iwe awamu ya sita lakini kwa namna alivyoanza kuna uwezekano mkubwa wa kufeli darasa hivyo itabidi arudie awamu ya tano.
 
Naunga mkono mama hii ni awamu ya 6 kula kichwa Cha Sabaya,Happi,Muro,Kitwala vinginevyo itabaki kuwa awamu ya 5 tu.
 
Haikwisha, aliyeibeba awamu hii keshakufa, imeishia njiani hiyo..

Hii maana yake tunarudi square one. Anaingia mbeba maono mwingine na kufungua kitabu kipya kabisa...

Hii ni awamu mpya, Awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassani...
Manake anapiga vipindi viwili......
2021-2025 /2025-2030 ukishaambiwa hii ni awamu mpya utaratibu ndio huo hapo juu
 
Lakini wateule wa rais wapo chini ya kiapo cha agano lililopita.

Kumaanisha hii ni awamu nyingine lazima kuwe na agano kati ya wateule na mteuaji. Agano halithibitiki bila kiapo!
Unadhani Rais ni mjinga ? Ameanza vizuri kwa kutafuta upenyo wa kupangua Baraza na kuanza kuweka watu wake.

Kadiri mda unavyoenda atawapangua wote na ataweka watu wake haaaa,hawezi kufanya ghafla maana nchi bado iko kwenye kiwingu cha marehemu,

Muda ni mwamuzi mzuri nyie tulieni maana lazima atafute kura 2025.

Kuhusu awamu ,kama mda anaorithi ni kuanzia miaka 3 na kuendelea inahesabika ni awamu mpya kwa hiyo ni awamu ya sita ya kipindi chake cha kwanza .
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hii ni Serikali ya awamu ya 6 hivyo atakayeshindwa kasi yake ataachwa njiani.

Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliweka sawa hili kwani jana watu wengi walinibishia nilipowaambia mimi naamini hii ni awamu ya 6.

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
Awamu ya tano, Rais wa sita.
Awamu ya tano ktk utaratibu wa nchi yetu kuwapata viongozi haijaisha.
 
Kwa mfano Tundu Lisu angeshinda uchaguzi ulopita angekuwa rais Wa awamu ya ngapi!?
Angekuwa Rais wa sita katika awamu ya tano..simple like USA trump hakumaliza awamu naingia biden..so Biden ni wa 48 katika awamu ya 47 nadhan
 
Uongo
Rais Tz anapesa mihula miwili ya uongozi yenye kipindi Cha miaka mitano
Anaweza kuongoza kea miaka 5 asiendelee awamu yake imepita
Mzee..hivi unasoma katiba ama unafikiri kwa kutumia makwapa!? Haijalishi kuendelea ama kutokuendelea kwake..awamu huwa inahesabiwa kwa.miaka 10 ,mitano ya kwanzA na mitano ya pili ...ndio awamu inakuwa imeisha...kasome katiba uieleewe
 
Back
Top Bottom