Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria Mkutano wa COP 26 Nchini Scotland

Mchungaji Msigwa alisafiri sana na Nyalandu wakati akiwa Waziri kivuli wa Utalii
 
Swala si kutoka bali serikali haitakiwi iwe na mambo ya kubahatisha,namaanisha lazima hii safari ilete faida zaidi ya gharama watakazotumia.
 
Inasemekana ni kesho.

Nyepesi ataambatana na mzee wa Msoga wanaenda kuhudhuria kongamano lihusulo mazingira.

Kazi mnayo Wadanganyika 😂
Anga kwa anga (sayansi na gharama zigo la mwananchi) vs ungo kwa ungo (nguvu za giza kwa gharama za mgonjwa maluweluwe)
 
We sema tu hujaniona siku nyingi...hii ni kutokana na majukumu niliyonayo kwa sasa.

Ila nitarejea.Nashukuru kwa kunimiss.

Ni kweli bado nipo katika maombolezo ya mwamba JPM...
 
Hata kama ni tetesi ungejikita katika kueleza faida za mkutano na hasara zake.

Kujenga nchi si lelemama.
 
Inasemekana ni kesho.

Nyepesi ataambatana na mzee wa Msoga wanaenda kuhudhuria kongamano lihusulo mazingira.

Kazi mnayo Wadanganyika 😂
Kwa hiyo wewe ndugu yangu umeona tu kusafiri ukaweka na 'emoji' yako ya cheko la pwani! Hili ni jukwaa la great thinkers; ungetuambia anaenda ktk mkutano gani, faida za huo mkutano kwa wewe, mimi na ndugu zetu vijijini. Mambo haya ukaona hayana umuhimu.

Sasa taarifa ya Ikulu iko wazi, anaenda ktk mkutano wa kukabiliana mabadiliko ya Tabianchi. Mafuriko, ukame, joto kali, njaa na majanga mengine.#Tujadili issues siyo porojo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…