Angeweza vipi kung’ara wakati yeye ni makamu kwa maana ya msaidizi mkuu?.

Alikuwa anamsaidia rais kwa kwenda kwenye mikutano mikubwa ya UN na ulaya, huo sio msaada?.

Ulitaka afanye lipi ili mchango wake uonekane kama makamu?.

Marehemu aliyekuwa karibu nae kikazi aliukubali uwezo wake, kipi tena cha ziada cha kuuthibitisha uwezo wake!.
 
Unategemea miujiza ya kufanya vizuri? Unadhani kufanya vizuri kunatokana tu na wishes za watu wewe kufanya vizuri? Nguvu ya kufanya vizuri iko wapi? Ipo historia yoyote inayobeba hivyo viashiria vya kufanya vizuri?
Ndio imeshakuwa kwamba makamu amekuwa rais baada ya rais kutangulia mbele za haki.

Iliandikwa na Mungu kuwa Samia atakuwa rais wa Tanzania kuanzia March 2021, ni suala la kukubaliana na mipango ya Mungu.

Baadhi yetu mfumo dume umeteka akili kiasi cha kushindwa kukubaliana na mapenzi ya Mungu, lakini hakuna chochote kinachoweza kubadilishwa.
 
hilo hawezi kufanya katu..... naye hana uhakika wa kurudi maana akina bashiru watamkomalia
Bashiru ni sawa na mamba anakuwa na nguvu akiwa majini.
Bashiru alikuwa na nguvu akipokuwepo jiwe .
 
Anasuburiwa atoe muelekeo wa awamu yake

Anasuburiwa atoe muelekeo wa awamu yake
Muelekeo upi tena ilhali Marehehemu alishatoa muelekeo huko nyuma na yeye mama anasema tukimkumbuka marehemu basi tumuone yeye na tukiomuona yeye basi tumkumbuke marehemu? Kwa kwenda kuhutubia Bunge ilhali anato kauli kama hizi ni kama anaji-contradict.
 
Uzandiki at its best... Rais alivunje Bunge!!!? 🤣🤣🤣
 
Nakuunga mkono kwa 100%
 
Mfumo dume umekuja leo baada ya kuwa Raisi? Suala la kukosa uwezo sasa mnataka kulifutika chini ya mfumo dume? Amekuwa Makamu wa Raisi kwa miaka mitano na ushee uliwahi kusikia watu wanataka aondoke kwa sababu ya jinsia yake? Hebu mnaomtetea kwa mihemko tu jipangeni kwa hoja zingine na sio hii ya mfumo dume!
 
Alivunje bunge kama kweli ana taka mshikamano wa watanzania hatuwezi kuwa na umoja wakati wawakilishi wengi sio chaguo la watanzania ni chaguo la hayati kwa dhuluma kubwa au BASI wale Covid 19 awazingue [emoji38][emoji38][emoji38]
Comment mzuri sana
 
Aisee kweli. Katika majimbo yalio nyuma hapa nchini Kongwa iko katika kumi mbaya.
Next time nagombea Kongwa kwa tiketi ya chama changu.
Wana Kongwa walisha mkataa huyo mzee wa bakora
 
Huyu ndio rais wetu mkuu. Tunae mpaka 2025 Mungu akipenda.

Kusema hajafanya chochote cha maana ni kumkosea heshima na ni ukosefu wa shukrani.

Angekuwa hana uwezo 2020 asingeendelea na umakamu. Kumbuka katoka jasho majukwaani kufanya kampeni hajabebwa bali uwezo wake ndio umeongea.
 

Hivi Makamu wa Raisi ni mpika chai wa raisi? Kwa mjibu wa katiba, hana majukumu ya kufanya? Unataka kusema marehemu hakumpa duties na resposibilities za kutimiza? Ofisi ya Makamu ipo kumpikia Chai Raisi wa nchi au ipo kwa majukumu maalumu? Unapokuwa msaidizi wa mtu unakuwa unakaa tu ukisubiria unayemsubiria aondoke ndipo ufanye kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…