Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,227
Acha uongoMama usipojitofautisha na Mwendazake basi huko mbele kuna kukwama kama alivyokwama Jiwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha uongoMama usipojitofautisha na Mwendazake basi huko mbele kuna kukwama kama alivyokwama Jiwe
Yeye darasa la ngapi?Akawape vipande vyao
Hasa wale darasa la saba..
Mzee Mgaya kwa sasa ni mshauri wa chama!Bora tumuingize mzee mgaya humo
Au vp!
Tuwapunguze wasema mipasho mule
Ova
subiri tu 2025.Saa ingine mnajitoa ufahamu sana,mnaona kama vile Samia yupo pale kwa tiketi ya chademaMama Samia, unda Tume Huru kisha vunja Bunge turudi kwenye uchaguzi kama kweli uko serious maana hili sio Bunge kabisa.
Aisee kweli. Katika majimbo yalio nyuma hapa nchini Kongwa iko katika kumi mbaya.KONGWA NI KWA KUPATIA UBUNGE TU; JAMAA NYUMBANI KWAKE NI SALASALA DAR ES SALAAM! BUNGE LIRUDISHE HESHIMA YAKE KWA KUMUONDOA HUYU MGOGO.
Alivunje bunge kama kweli ana taka mshikamano wa watanzania hatuwezi kuwa na umoja wakati wawakilishi wengi sio chaguo la watanzania ni chaguo la hayati kwa dhuluma kubwa au BASI wale Covid 19 awazingue 😆😆😆Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge Alhamisi Aprili 22 2021 jioni
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Mama Samia kulihutubia Bunge tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19 mwaka huu.
================
Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amelitangazia Bunge leo Jumatatu Aprili 19, 2021 kuwa Rais Samia atalihutubia Bunge Alhamisi ya wiki hii kuanzia saa 10 jioni.
Hivyo, Spika Ndugai amewaagiza wabunge wote walioko nje ya Jiji la Dodoma kurudi na wale wanaotaka kuondoka wazingatie kuwapo kwa shughuli hiyo kwanza.
Rais Samia atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha Rais wa tano, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.
Mwananchi
Mambo mengine ni ya ajabu sana! Yeye amesema na marehemu ni kitu kile kile sasa anataka kuhutubia ili aseme lipi ambalo marehemu hakupata kusema? Au ndio anaenda kufafanua jinsi yeye na marehemu walivyo damu damu? Kuna uzi ulikuwa umewekwa humu nadhani na MTU SERIOUS kidogo nashangaa umefutwa!Labda bila kuhutubia Bunge anajihisi hajawa Raisi kamili.
Mimi ningalifurahi asiishie tu kuliona Bunge halijadili mambo yasiyo na Afya kwa Taifa bali achukue hatua. Ikiwa Bunge ndio chombo cha kuhakiki na kuchunga Afya ya Nchi na limechepuka kufanya hi vyo achukue hatua ya kulivunja tu ili tuingie kwenye uchagzi ili tupime nguvu yake anayosema yuko sawa na marehemu.Hahahaha alafu atakuwa mgombea wa Chadema? Hzo ni ndoto cha mchana yeye mwenyewe anajua hawezi na hato jaribu kufanya hvyo hata siku moja
Ameshasema yeye na JPM ni kitu kimoja,acheni kuleta migawanyo.Zungumzieni mambo ya msingi.Sasa sijui wabunge wa CCM wataanza kuijadili hotuba ya Rais Samia au wataendelea kuhubiri legacy ya JPM !!
Mkuu umeandika mengi na yameweza kukutambulisha wewe kisiasa upo kambi ipi.Mambo mengineni ya ajau sana! Yeye amesema na marehemu ni kitu kile kile sasa anataka kuhutubia ili aseme lipi ambalo marehemu hakupata kusema? Au ndio anaenda kufafanua jinsi yeye na marehemu walivyo damu damu? Kuna uzi ulikuwa umewekwa humu nadhani na MTU SERIOUS kidogo nashangaa umefutwa!
Mimi kwa maoni yangu,namshauri mama apunguze maneno bali azidishe matendo. Kama kazi inaendelea,basi iendelee kwa vitendo na sio mambo ya Hotuba Hotuba. Nchi ilishajazwa Hotuba kwenye Ansard huko! Uraisi wa Hotuba hauna tija zama zetu hizi. Kwa nini asikae Ofisini kutafuta pesa za kuendesha Miradi ya Urithi? Ninampa mausia yafuatayo:
1. Mintarafu Uongozi wowote ule, watu ndio kwanza wanakutaka na sio ulazimishe wakutake. Hili inabidi alijue vizuri.Yeye ni Raisi wa Katiba na sio wa Kuchaguliwa! Asifike mahali akaona kama ni lazima awe Raisi wetu. Ikiwa Chama chake hakiridhiki na uwezo wake ni bora akaheshimu hilo. Kama Chama kimeshimu Katiba kuwa hakuna namna inabidi ashike mdaraka kikatiba hivyo hivyo Chama kikifika mahali kikaona hawezi kusukuma maono ya Nchi basi na yeye aheshimu Katiba ya Chama na watanzania kwa ujumla. Marehemu Magufuli alishatueleza kuwa ifikapo mwaka 2025 wangaling'atuka yeye na Makamu wake. Makamu wa Raisi ni Raisi na ni kutokana na Logic hiyo mama amekuwa Raisi Automaticlly. Kwa Misingi hiyo, tunaomba asifanye Juhudi zozote za kujibakiza madarakani baada ya 2025 kwa kusema eti naye anahitaji miaka 5 au 10 ili kukamilisha awamu yake ya Sita. Kama watu walihoji au waltaka asipewe nafasi hiyo watu hao sio wa kupuuzwa. pengine wanamjua vizuri zaidi.Nchi hii ilisha-define inataka Kiongozi wa aina gani na wa kuipeleka wapi.Katibu Mkuu wa Chama sio mtu mdogo. Huyo ndo mtu mwenye taarifa za Mwenendo na uwezo wa kila Mwanachama. Mama naye ni Mwanachama. KM ndiye intelligensia ya taarifa za Chama na hivi kama yeye na wenzie walimtilia mama mashaka ya kiuwezo basi asipuuze. Mambp ya majaribio tumeshayaona. Hili la uwezo nitaliandikia kwa kina siku zijazo.
2. Yeye kishasema na Magufuli ni kitu kimoja. Sasa kama ni Kitu kimoja ni kwa nini unamshauri amtimue PM?Anamutimuaje mtu aliyekuwa ameteuliwa na Mtu ambaye anadai wanafanana kitabia na kiutendaji?{ hIli nitakuja na bandiko lake siku zijazo). Hivi kama yeye na Marehemu ni kitu kile kile anasumbuka kuunda timu mpya ya nini wakati aliyeunda timu iliyopo anafanana naye kiuwezo na kiutendaji? Kwa nini kwa maneno mengine anasambaratisha timu ambayo aliiuda mwenyeewe?
3. Kabla mama hajaendelea na kupanga timu yake ni vizzuri afanye utafiti wa jinsi anavyokubalika miongoni mwa Watanzania. Hivi anajua kuwa kuna watu hata Hotuba zake hawataki kusikiliza? Hvi anajua kuwa ikifika wakati wa kuhutubia wegine wanazima TV na kuondoka? Watu wanamjua uwezo wake. Aaachane na mambo ya kutueleza kuwa Makonda ndiye alifanya RATIJG yake. Hivi kweli tunaweza kumuamini kama ni kiongozi anayetufaa kutokana na rating ya Makonda? Leo Makonda yuko wapi kama Makonda ndiye Benchmark yake?
Mama naye azingatie ushauri aliopewa na Chama na Idara. Asinogewe na Madaraka. Uraisi kwa Zama zetu na mahali ambako Marehemu alishatufikisha, anaweza kupwaya. Huo ndio Ukweli! Akitaka kung'ang'ania kwa kudanganywa kuwa kama marehemu aliweza, kwa nini yeye ashindwe, atajikuta ametupeleka mahali ambako watanzania makini wanaweza kumfurusha kwa mawe. Kanisa Katoliki limeshatoa Sauti kama anajua kusoma katikati ya mistari.Limesema halitarajii kurudishwa nyuma tena kutoka marehemu alipoliacha! Huo ni Ujumbe amepewa na aufanyiea kazi! Watu wanatarajia kuona Ndege zaidi zinanunuliwa na Barabara zinajengwa.Na yote hayo yanawezekana kwa kukusanya Kodi. Sasa yeye anasema kodi ya dhuluma haitaki! Hataki kodi dhuluma ila anadai yeye na marehemu ni kitu kimoja? Kusema hutaki kodi ya dhuluma ina maana unatuma meseji kuwa kuna mtu amejenga nchi kwa kodi ya dhuluma. Sasa kama yupo halafu unajinasibu kuwa wewe na yeye kitu kilekile na wakati huo huo kudai wewe hutaki mambo yake ya dhuluma watu wenye akili wakueleweje? Mambo kama haya unaweza kuona ndiyo pengine watu walikuwa hawataki kabisa arithi hiyo nafasi.
Hili litawatesa Sana 2025.kama mama hatafanya magufulification katika uchaguzi.Bora maana bunge ni dhaifu kuliko mabunge yote yaliyowahi kuwepo toka historia ya nchi hii
Unampangia Rais kazi.Watanzania bwana,mnaota mchana kweupe.Halafu waanze tena kujadili hotuba ya Raisi badala ya kukamilisha waliyoyaanza wakati Ilani yao ni ile ile.
Mama Samia, unda Tume Huru kisha vunja Bunge turudi kwenye uchaguzi kama kweli uko serious maana hili sio Bunge kabisa.
Siandiki kishabiki bali kwa kutumia akili. Sihitaji kumshabikia waaidha mama wala marehemu bila sababu au vigezo vinavyovuka mashaka. Hivi niambie mama amefanya kitu gani ambacho mpaka leo unaweza kumnasibisha nacho? Mama sio mgeni Serikalini ama iwe Zanzibar au Serikali ya Muungano. Nimbie kwa miaka mitano iliyopita akiwa na Marehemu aling'ara kwa lipi? Kwa nafasi yake hakustahili kung'ara kwa lolote? Nafasi aliyokuwa nayo kiutendaji ni ya kutwezwa au ya kusema anasubiria nafasi nyingiyo ang'are?Mkuu umeandika mengi na yameweza kukutambulisha wewe kisiasa upo kambi ipi.
JPM ameshalala usingizi wa milele hataamka tena katika uhai huu wa sasa.
Ni suala la kukubaliana na ukweli na kuondoa vinyongo na kuendelea kuitazama kesho kwa matumaini huku rais akiwa Mama Samia.
Akifanya kazi vizuri 2025 atapeta bila taabu.
Hakuna namna lazima bunge livunjwe maana limekisa sifa ya kuitwa bunge.Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge Alhamisi Aprili 22 2021 jioni
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Mama Samia kulihutubia Bunge tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19 mwaka huu.
================
Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amelitangazia Bunge leo Jumatatu Aprili 19, 2021 kuwa Rais Samia atalihutubia Bunge Alhamisi ya wiki hii kuanzia saa 10 jioni.
Hivyo, Spika Ndugai amewaagiza wabunge wote walioko nje ya Jiji la Dodoma kurudi na wale wanaotaka kuondoka wazingatie kuwapo kwa shughuli hiyo kwanza.
Rais Samia atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha Rais wa tano, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.
Mwananchi
Unategemea miujiza ya kufanya vizuri? Unadhani kufanya vizuri kunatokana tu na wishes za watu wewe kufanya vizuri? Nguvu ya kufanya vizuri iko wapi? Ipo historia yoyote inayobeba hivyo viashiria vya kufanya vizuri?Mkuu umeandika mengi na yameweza kukutambulisha wewe kisiasa upo kambi ipi.
JPM ameshalala usingizi wa milele hataamka tena katika uhai huu wa sasa.
Ni suala la kukubaliana na ukweli na kuondoa vinyongo na kuendelea kuitazama kesho kwa matumaini huku rais akiwa Mama Samia.
Akifanya kazi vizuri 2025 atapeta bila taabu.