Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

Dah ikiwa hivyo kufikia 2050 Tz itakuwa na mikoa 75!
 
Kukataa sio lazima useme hapana.... Wala kukubali si lazima useme ndio....

Kuelekezwa kama hamna vigezo ni kupewa sababu za kukataliwa

Kupewa sababu inamaana hamna vigezo.
 
Zingekuwa Enzi hizo... Hapo hapo chato ingetangazwa mkoa na kutangazwa mkuu wa mkoa
 
Itakua unasikiliza Lisu Redio Fm ila kama umemsikiliza rais, mipango ya chato iko pale pale.
Hamna cha chato wewe ulitaka asemeje wakati mwili wa bos wake bado haujazikwa ngojea azikwe akalie kiti aone cha moto ndo utajua hujui, yaan huku wanalia ajira, huku wanalia maafa huku korona akumbuke kujenga uwanja wa mpira chato mh nicheke kidogo hiiiiiiiiiii
 
Mkuu, kama kuna wilaya zinahitajika kuifanya Chato kukidhi vigezo vya kuwa mkoa, kwa nini isiwe kwamba Chato ndiyo iende iunganishwe na hizo wilaya halafu moja ya hizo wilaya zingine ndiyo iwe mkoa?

Kwanza inatoa picha gani mzee wa Chato anajua mipango mikubwa ya nchi kama hiyo huku aliyekuwa Makamu wa Rais hakuwa na habari nayo? Kuna uzi nauandaa, embu ngoja wazike kwanza.
 
Ukikidhi vigezo alisikika raisi. Shida ni vigezo si jambo lingine. Ukishakidhi vigezo kwann usiwe mkoa?
Na hivyo vigezo ndio ngumu kufikiwa! Mwanza iligawanywa ukapatikana mkoa wa Geita, sasa Geita nayo igawanywe upatikane mkoa wa Chato! Kipi cha zaidi huku? Kule Moro kuna wilaya ili uifikie unatumia masaa karibu 16 kwa nini wasifikirie kuugawa mkoa kama huo!?
 
Kazi ipo
 
We jamaa una point sana kwenye hili. Mimi mwenyewe sielewagi sababu za kugawa mikoa.

Wanachohitaji ni kuboresha huduma za jamii, kugawa mikoa hakuleti ufanisi wowote zaidi ya kuongeza gharama za serikali. Tena ukizingatia hatuna majimbo, haya maamuzi hayana maana.
 
Andamana Mkuu
 
Mama amekubali, amesema hata kama wataona vigezo havijakidhi basi watawaelekeza ili vigezo vikidhi....
Kuna wimbo wa twanga pepeta unaimba, "Chuki binafsi haifai yooo... Tuiacheni jamani italeta tafrani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…