Ukweli ni kuwa JPM alikuwa na mpango wa kuanzisha mkoa mpya wa Rubondo. Na chato ilikuwa itangazwe kuwa makao makuu ya mkoa wa Rubondo mwezi April mwaka huu atakapokuwa mapumziko ya pasaka.
Mipango hiyo ilikuwa imeshafanyika mapema kwa kujenga nadhani unakumbuka jinsi chato ilikuwa ikipendelewa kwa kujengewa vitu kama hospital ya rufaa, jengo la mahakama mkoa, msd head quarter, crdb mkoa, uwanja wa ndege na mengineyo. Ambavyo sisi tulikuwa tukihoji kwanini vitu hiyo na miundo msingi ya mkoa wa Geita inajengwa chato badala ya makao makuu ya mkoa? Kumbe ilikuwa ni mpango wa kuifanya chato kuwa makao makuu ya mkoa wa Rubondo.
Rais Samia kujibu hivyo si kwamba alikuwa hajui kinachoendelea, ila isipokuwa anaona kwa hakika ulikuwa ni upendeleo dhahiri ulofanywa na mtangulizi wake na hivyo haoni tija kuendelea nao, ndo maana kajibu kwa wepesi na kwa kidiplomasia kwa kuwambia "nasikia mlikuwa na mchakato, mkikidhi vigezo itakuwa".
Lakini hakika, hiyo ni chenga ya mwili hajataka tu kusema wazi, kwakuwa ilikuwa ni msibani, na yeye ndo punde tu kahold ofisi hakutaka kuibua hisia mseto juu hili, tena mapema hivi.