Sawa uliyosema lakini SIYO KWELI kuwa mtu ambaye haongei kiingereza kwa ufasaha HANA ELIMU. Kiingereza ni lugha tu sawa na lugha nyingine yoyote. Vile vile ukumbuke kuwa watu wanatofautiana vipaji katika masomo mbalimbali ndiyo maana wengine ni wazuri kwenye lugha wengine ni wazuri kwenye numbers.
Pia kiingereza kilitapakaa duniani kwa sababu Waingereza walikuwa na makoloni mengi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Kwa hiyo usiwakandie watu wasioweza kuzungumza kiingereza vizuri ukadhani hawana akili au hawana elimu.
Ukienda Uingereza au hata hapa Tanzania kwa watoto wa darasa la tano wanaosoma shule zinazofundisha kiingereza tu utawakuta wanaongea kiingereza kizuri sana tofauti na wazazi wao waliosoma shule za Kayumba, sasa unataka kutuambia kuwa hao watoto wana elimu zaidi kuliko hao wazazi? Au ni wa maana zaidi kuliko wengine wasiozungumza kiingereza?
Kiingereza kwa Tanzania ni Lugha ya kujifunzia lakini pia ni lugha rasmi, ( official Language) hasa wewe O’ level na A’level umejifunzia kiingereza halafu haujakimaster vyema inaonekana hata uliyosoma haukuyaelewa ndio sababu akiongea kiingereza Mchina kwake anaweza kuungaunga maana kwao lugha rasmi ya kujifunzia ni kichina, tusiwatetee watu wasioweza kuongea lugha waliyojifunzia