Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #21
Acha dharau wewe.Yeye mwenyewe uwepo wake hapo ni kwa hisani ya WANAUME. Aache maneno mengi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha dharau wewe.Yeye mwenyewe uwepo wake hapo ni kwa hisani ya WANAUME. Aache maneno mengi.
Luca acha kubishaba na neno la Mungu. Mwanaume ndio kichwa na njia ya mafanikio. Wanaume ndio walilinda katiba na kuhakikisha mwenyekiti anakuwa rais! Kwani ni uongo?Acha dharau wewe.
Nasubiri jibu lao 😂😂😂Unaonaje 98% ya askari wa JWTZ wakiwa wanawake ili kuongeza ufanisi?
Wako asilimia ngapi?Kwani wewe hujawaona wanawake huko Jeshini?
Anaongoza Nchi na siyo Taasisi.taasisi anayo ongoza yeye inafanya poa ama ndio tia maji tia maji
Nchi inapalanganyika,nchi imekosa msimamo,nchi haina mwenyewe,watu wanajichotea tu kwa sababu ya usimamizi mkuu kutoka kwa wanawake.Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Amesema ya Kuwa Taasisi Zenye kuongozwa au zenye idadi kubwa ya Wanawake huwa zinafanya vizuri sana na kuleta au kutoa Matokeo Chanya. Kauli hiyo ilikuwa ni katika kurejelea utafiti wa kisayansi ambao umewahi kufanywa siku za nyuma na kuja na matokeo hayo.
Rais wetu amezungumza hayo katika kuelezea nafasi, Mchango ,uwezo wa Mwanamke katika uongozi na katika kuchochea maendeleo.
Katika hilo Mimi Mwashambwa Lucas ninamuunga mkono Rais wetu. Hata ukiangalia katika Nchi yetu utagundua ya kuwa Wanawake ni watu makini sana maofisini na katika kazi zao za kila siku,ni watu wanaozingatia sana kazi bila kupuuza wala kuleta ubabaishaji.
Na ni watu makini, waadilifu,waaminifu , wachapakazi na wenye kuridhika na maslahi wanayopokea au kupata . Ndio maana huwezi kuwakuta kwenye makashifa au skendo za Rushwa na Ufisadi.
Embu jaribu kuona hapa Nchini makashifa ya rushwa na ufisadi mkubwa mkubwa ambao umewahi kutokea na kufanyika hapa Nchini. Utakuta majina yaliyojaa na watu waliohusika kwa kiasi kikubwa ni wanaume pekee yaoo.
Ni wanaume ndio utakuta wakitumia hovyo sana hata madaraka yao katika kujinufaisha. Wakati wanawake wanatumia madaraka na vyeo vyao kwa ajili ya watu wote. Wanawake ni watu wakarimu, wanyenyekevu,wapole na wastaarabu sana wawapo katika nafasi za uongozi na hivyo kufikika kiurahisi na watu wenye shida na wenye kuhitaji msaada na kusaidiwa.
Wanawake ni watu wenye kuwaza watu badala ya matumbo yao na tamaa zao au matamanio yao binafsi. Wakati unakuta wanaume akipata kazi tu cha kwanza anaanza kuwaza namna ya kuiba,kuchota na kufuja pesa za umma kwa maslahi yake binafsi. Wanaume wanakuwa wanafaya kazi ya kushindana kuiba na kuficha pesa. Huwezi ukakuta Mwanamke ni kiongozi amefungua akaunti nje ya Nchi kwa ajili ya kuficha pesa za wizi ,rushwa na ufisadi.
Mwanamke ni mtu mwenye huruma ,upendo na mwenye kuguswa na shida za watu. Ni mtu ambaye anaumia kuona mtu akiwa na shida. Ni wepesi wa kutoa msaada na kumuhudumia mtu. Wakati wanaume ni wagumu kuguswa na shida za watu .badala yake atataka umpooze kwa chochote kile kwa ajili ya tumbo lake. Wakati mwanamke anaona huruma ya kumfanyia ubaya na roho mbaya mtu.
Mwanamke ukimpa ofisi anakuwa na uchungu nayo ,kuijali na kutaka kuona ikiendelea kufanikiwa na kufanya vizuri. Wakati mwanaume yeye anafanya vitu kwa maslahi yake binafsi na hana hata huruma hata kama ikifa kwa kupata hasara yeye anakuwa hana uchungu wala kujali wala kuumia. Ndio maana kuna mashirika ya umma yameuwawa ,kufilisika na kupata hasara kwa sababu ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma uliofanywa na wanaume.
Watanzania tunakila sababu ya Kumshukuru Mungu kwa kutupatia Rais Samia kuwa Rais wetu. Tuna kila sababu ya kuona fahari kuwa Na mama kitini.tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mama na kuendelea kumuombea ili Mungu amjalie Maisha marefu yenye Heri na furaha.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Lucas is number one for this issue.
Katika makuzi yako ulipata malezi ya Mama yako Mzazi? Kwamba mama yako aliyekuzaa huamini kama anaweza kuwa kiongozi na kuongoza? Kwanini unatoa kauli za udhalilishaji kwa wanawake ikiwepo na Mama yako mzazi ambaye naye ni Mwanamke?Nchi inapalanganyika,nchi imekosa msimamo,nchi haina mwenyewe,watu wanajichotea tu kwa sababu ya usimamizi mkuu kutoka kwa wanawake.
Unajua tunaweza tukawa tunakomaza mafuvu kwamba wewe ni Lukas yule msafwa wa umalila kumbe wewe ni Abdul na Mama samia ni Mamako mzazi, maana sijawah kukuo a unasifia mamako alokuuza, mkuu kama wewe Abdul Sema kuna ishue nikwambie kuhusu Maza ako.Katika makuzi yako ulipata malezi ya Mama yako Mzazi? Kwamba mama yako aliyekuzaa huamini kama anaweza kuwa kiongozi na kuongoza? Kwanini unatoa kauli za udhalilishaji kwa wanawake ikiwepo na Mama yako mzazi ambaye naye ni Mwanamke?
Wewe ni mjinga tu na hilo jina la Lucas linatumika vibaya kudhalilisha uumbaji wa mwenyezi Mungu.Mbona Marekani inafanya vizuri bila hata hao wanawake mnaowapa kipaumbele?Mbona Russia inasonga mbele bila hao wanawake mnaowaona malaika?Mbona China inasonga mbele bila ya usimamizi wa hao wanawake manaowaona ni waaminifu.Mbona Japan inafanya vizuri zaidi bila ya usimamizi wa hao wanawake?Katika makuzi yako ulipata malezi ya Mama yako Mzazi? Kwamba mama yako aliyekuzaa huamini kama anaweza kuwa kiongozi na kuongoza? Kwanini unatoa kauli za udhalilishaji kwa wanawake ikiwepo na Mama yako mzazi ambaye naye ni Mwanamke?
Uliongea lini na Mungu akakupa Mipango yake? Kwanini usingemwambia akupatie na wewe akili japo kidogo.Wewe ni mjinga tu na hilo jina la Lucas linatumika vibaya kudhalilisha uumbaji wa mwenyezi Mungu.Mbona Marekani inafanya vizuri bila hata hao wanawake mnaowapa kipaumbele?Mbona Russia inasonga mbele bila hao wanawake mnaowaona malaika?Mbona China inasonga mbele bila ya usimamizi wa hao wanawake manaowaona ni waaminifu.Mbona Japan inafanya vizuri zaidi bila ya usimamizi wa hao wanawake?
Nchi nyingi Ulaya zinaendelea kuporomoka kimaisha kwa sababu ya kuendekeza propanganda ambazo siyo mpango wa Mungu.
Kwani Mama yangu ndiye Rais? Umewahi kusikia kuwa Mama yangu ameongeza Bajeti ya kilimo kutoka Billioni 250 hadi Trilioni moja na point kama alivyofanya Rais Samia? Je ni nani anayetoa pesa za Elimu bure, kuongeza bajeti ya mikopo ya Elimu ya Juu,kuongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo kufikia Elfu kumi kwa siku na mengine mengi kama siyo Rais Samia Mwenyewe? Aliyefanya si ni Rais Samia Mwenyewe? Sasa unataka nimsifie Mama yangu mzazi wakati Dunia nzima inafahamu mtekelezaji ni Rais Samia?Unajua tunaweza tukawa tunakomaza mafuvu kwamba wewe ni Lukas yule msafwa wa umalila kumbe wewe ni Abdul na Mama samia ni Mamako mzazi, maana sijawah kukuo a unasifia mamako alokuuza, mkuu kama wewe Abdul Sema kuna ishue nikwambie kuhusu Maza ako.
Sawsaw tutakujengea statue au wew mwenyew ukuwe hiyo.CCM ni chama safi na ndio maana ukibainika kuhusika katika vitendo vya ufisadi na rushwa ni lazima Uchukuliwe hatua
Wewe huna akili kila siku siku kusifia wenzio,si upambane na wewe siku moja tukuite Mbunge,Spika,Waziri au Rais kuliko kutumia muda wako vibaya kufubaza fikra zako.Uliongea lini na Mungu akakupa Mipango yake? Kwanini usingemwambia akupatie na wewe akili japo kidogo.
Kweli ukosahih ila sijawahi kutana na mti mwenye hulka kama ya kwako ktk maisha live. Sku nikikutana naye i hope itakuwa mara yangu ya kwanza kukutana msukule.Kwani Mama yangu ndiye Rais? Umewahi kusikia kuwa Mama yangu ameongeza Bajeti ya kilimo kutoka Billioni 250 hadi Trilioni moja na point kama alivyofanya Rais Samia? Je ni nani anayetoa pesa za Elimu bure, kuongeza bajeti ya mikopo ya Elimu ya Juu,kuongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo kufikia Elfu kumi kwa siku na mengine mengi kama siyo Rais Samia Mwenyewe? Aliyefanya si ni Rais Samia Mwenyewe? Sasa unataka nimsifie Mama yangu mzazi wakati Dunia nzima inafahamu mtekelezaji ni Rais Samia?
Hayo siyo mahitaji ya watanzania.Watanzania sio Mifugo ya CCM tunataka KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI.