Rais Samia: Taasisi Zenye Idadi Kubwa ya Wanawake Zinafanya Vizuri sana na Kufanikiwa.

Rais Samia: Taasisi Zenye Idadi Kubwa ya Wanawake Zinafanya Vizuri sana na Kufanikiwa.

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Amesema ya Kuwa Taasisi Zenye kuongozwa au zenye idadi kubwa ya Wanawake huwa zinafanya vizuri sana na kuleta au kutoa Matokeo Chanya. Kauli hiyo ilikuwa ni katika kurejelea utafiti wa kisayansi ambao umewahi kufanywa siku za nyuma na kuja na matokeo hayo.

Rais wetu amezungumza hayo katika kuelezea nafasi, Mchango ,uwezo wa Mwanamke katika uongozi na katika kuchochea maendeleo.

Katika hilo Mimi Mwashambwa Lucas ninamuunga mkono Rais wetu. Hata ukiangalia katika Nchi yetu utagundua ya kuwa Wanawake ni watu makini sana maofisini na katika kazi zao za kila siku,ni watu wanaozingatia sana kazi bila kupuuza wala kuleta ubabaishaji.

Na ni watu makini, waadilifu,waaminifu , wachapakazi na wenye kuridhika na maslahi wanayopokea au kupata . Ndio maana huwezi kuwakuta kwenye makashifa au skendo za Rushwa na Ufisadi.

Embu jaribu kuona hapa Nchini makashifa ya rushwa na ufisadi mkubwa mkubwa ambao umewahi kutokea na kufanyika hapa Nchini. Utakuta majina yaliyojaa na watu waliohusika kwa kiasi kikubwa ni wanaume pekee yaoo.

Ni wanaume ndio utakuta wakitumia hovyo sana hata madaraka yao katika kujinufaisha. Wakati wanawake wanatumia madaraka na vyeo vyao kwa ajili ya watu wote. Wanawake ni watu wakarimu, wanyenyekevu,wapole na wastaarabu sana wawapo katika nafasi za uongozi na hivyo kufikika kiurahisi na watu wenye shida na wenye kuhitaji msaada na kusaidiwa.

Wanawake ni watu wenye kuwaza watu badala ya matumbo yao na tamaa zao au matamanio yao binafsi. Wakati unakuta wanaume akipata kazi tu cha kwanza anaanza kuwaza namna ya kuiba,kuchota na kufuja pesa za umma kwa maslahi yake binafsi. Wanaume wanakuwa wanafaya kazi ya kushindana kuiba na kuficha pesa. Huwezi ukakuta Mwanamke ni kiongozi amefungua akaunti nje ya Nchi kwa ajili ya kuficha pesa za wizi ,rushwa na ufisadi.

Mwanamke ni mtu mwenye huruma ,upendo na mwenye kuguswa na shida za watu. Ni mtu ambaye anaumia kuona mtu akiwa na shida. Ni wepesi wa kutoa msaada na kumuhudumia mtu. Wakati wanaume ni wagumu kuguswa na shida za watu .badala yake atataka umpooze kwa chochote kile kwa ajili ya tumbo lake. Wakati mwanamke anaona huruma ya kumfanyia ubaya na roho mbaya mtu.

Mwanamke ukimpa ofisi anakuwa na uchungu nayo ,kuijali na kutaka kuona ikiendelea kufanikiwa na kufanya vizuri. Wakati mwanaume yeye anafanya vitu kwa maslahi yake binafsi na hana hata huruma hata kama ikifa kwa kupata hasara yeye anakuwa hana uchungu wala kujali wala kuumia. Ndio maana kuna mashirika ya umma yameuwawa ,kufilisika na kupata hasara kwa sababu ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma uliofanywa na wanaume.

Watanzania tunakila sababu ya Kumshukuru Mungu kwa kutupatia Rais Samia kuwa Rais wetu. Tuna kila sababu ya kuona fahari kuwa Na mama kitini.tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mama na kuendelea kumuombea ili Mungu amjalie Maisha marefu yenye Heri na furaha.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wanaume Ndio hawa akina Lucas Mwashambwa 😂😂😂

Dunia simama nishuke 🐼
 
Kwani wapi waliapa kuitumikia na kuilinda Hiyo GOMA? Ulinzi wa Congo ni jukumu la wa Congo wenyewe na siyo letu watanzania
Kama nchi washirika wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni jukumu letu pia kulinda ndugu zetu, majirani zetu c ndio maana tulipeleka jeshi letu kule na tuka host kabisa na meeting ya kusolve yanayojiri humo na wakaalikwa na viongozi karibu wote wa ukanda huu
 
Kwani Mama yangu ndiye Rais? Umewahi kusikia kuwa Mama yangu ameongeza Bajeti ya kilimo kutoka Billioni 250 hadi Trilioni moja na point kama alivyofanya Rais Samia? Je ni nani anayetoa pesa za Elimu bure, kuongeza bajeti ya mikopo ya Elimu ya Juu,kuongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo kufikia Elfu kumi kwa siku na mengine mengi kama siyo Rais Samia Mwenyewe? Aliyefanya si ni Rais Samia Mwenyewe? Sasa unataka nimsifie Mama yangu mzazi wakati Dunia nzima inafahamu mtekelezaji ni Rais Samia?
Lukas kila siku nakwambia pesa sio za kwake ni za watanzania, utaelewa? Yeye anatekeleza jukumu analotakiwa kulifanya sababu kapewa kazi na watanzania sasa kwanini unasifia kila siku mama hivi mama vile Yan kama hela zinatoka mfukoni kwake wakati hata mshahara anaolipwa ni kodi za watanzania, run kwenu hata na aibu. Leo msifie hata Mamako mzazi basi, lakin kama wewe ni Abdul haina noma mwanangu we endelea kumsifia mamako...Lakin mnaharibu vijana nchi hii sababu saivi madogo hawataki kazi wanataka uchawa na wanaona machawa wanavyopewa publicity ila machawa wengi ni mashoga, sio wote ila wengi ni machoko. Acheni propaganda za kitoto anachofanya mama samia ndio kazi alotumwa kufanya ndio sehemu job attributes ya kazi aliyopewa sio nyie kuifanya ionekane kama anawonea huruma watanzania anaona awasaidie kwa hela zake mfukoni, Sawa mkuu. Machawa mnaharibu hii nchi kuna siku itakuwa kama kongo sababu hakuna nchi duniani ina chawa wanajua kusifia mabosi kama kongo....utayasikia "papa mukulu mutu ya watu, nazombe nangai, chew, mutu ya pesa mingi, solola bien, mutu ya suti kutoka parisi, mosi kitoko, elokote, raisi wa maraisi wote duniani ukuye mbele utomboke na mambo ya dollar " Yan bosi anasifiwa saa nzima. Lukas oneni huruma mtaani watu wana njaa kali punguzeni propaganda kwenye magroup yenu anaefanya kazi kazi inaonekana wala haiitaji kumsemea kila ukiamka.. Achenu hizo bwana
 
Umepamba umepitiliza hata yeye mwenyewe anakushangaa,na anajua kabisa unampamba si kwasababu unampenda sana,ni kwasababu ya njaa.
Mwenye uhakika wa kula na kushiba mihogo yake hana muda huo .
 
Kama nchi washirika wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni jukumu letu pia kulinda ndugu zetu, majirani zetu c ndio maana tulipeleka jeshi letu kule na tuka host kabisa na meeting ya kusolve yanayojiri humo na wakaalikwa na viongozi karibu wote wa ukanda huu
Kama wao wanakimbia majukumu ya kulinda Ardhi yao .wanataka nani amwage Damu kwa ajili ya kutetea ardhi yao?
 
Umepamba umepitiliza hata yeye mwenyewe anakushangaa,na anajua kabisa unampamba si kwasababu unampenda sana,ni kwasababu ya njaa.
Mwenye uhakika wa kula na kushiba mihogo yake hana muda huo .
Mimi nimeandika ukweli na siyo kupamba kama ukumbi wa sherehe
 
Lukas kila siku nakwambia pesa sio za kwake ni za watanzania, utaelewa? Yeye anatekeleza jukumu analotakiwa kulifanya sababu kapewa kazi na watanzania sasa kwanini unasifia kila siku mama hivi mama vile Yan kama hela zinatoka mfukoni kwake wakati hata mshahara anaolipwa ni kodi za watanzania, run kwenu hata na aibu. Leo msifie hata Mamako mzazi basi, lakin kama wewe ni Abdul haina noma mwanangu we endelea kumsifia mamako...Lakin mnaharibu vijana nchi hii sababu saivi madogo hawataki kazi wanataka uchawa na wanaona machawa wanavyopewa publicity ila machawa wengi ni mashoga, sio wote ila wengi ni machoko. Acheni propaganda za kitoto anachofanya mama samia ndio kazi alotumwa kufanya ndio sehemu job attributes ya kazi aliyopewa sio nyie kuifanya ionekane kama anawonea huruma watanzania anaona awasaidie kwa hela zake mfukoni, Sawa mkuu. Machawa mnaharibu hii nchi kuna siku itakuwa kama kongo sababu hakuna nchi duniani ina chawa wanajua kusifia mabosi kama kongo....utayasikia "papa mukulu mutu ya watu, nazombe nangai, chew, mutu ya pesa mingi, solola bien, mutu ya suti kutoka parisi, mosi kitoko, elokote, raisi wa maraisi wote duniani ukuye mbele utomboke na mambo ya dollar " Yan bosi anasifiwa saa nzima. Lukas oneni huruma mtaani watu wana njaa kali punguzeni propaganda kwenye magroup yenu anaefanya kazi kazi inaonekana wala haiitaji kumsemea kila ukiamka.. Achenu hizo bwana
Umewahi kujiuliza lengo la kuanzishwa hadi tuzo ya uchezaji bora? Kwanini mmoja apewe uchazaji bora wa Dunia wakati hachezi peke yake uwanjani na hachezi bure?
 
Katika maana ya wakubwa kufanikiwa zaidi ndio. Lakini hakuna mtu atamuweka kwenye issue sensitive mtu kama huyo maana hana akili zaidi ya kutumika kama condom tu
Hayo ni hadi pale atakapo kuwa na utambuzi
 
Umewahi kujiuliza lengo la kuanzishwa hadi tuzo ya uchezaji bora? Kwanini mmoja apewe uchazaji bora wa Dunia wakati hachezi peke yake uwanjani na hachezi bure?
Aloo we jamaa umeshindikana Yan kumbe wasafwa ndio mlivyo ? Yan daah 😂😂😂😂 me nakushangaa sana sasa boli na kazi ya uraisi inafanana ? How ? Ujue mkuu unakuja huku kwa kina messi ma ball dancer huku sasa ndio utaelewa yote huku hakuna cha kusema mama anaupiga mwingi anaupiga mwingi wanaonekana kwenye video na statistics zinasoma, kwanini unafananisha vitu viwili tofauti ?
 
Umewahi kujiuliza kwanini kuna tuzo mbalimbali kwa watu wanaofanya vizuri katika maeneo yao ya kazi? Umewahi kujiuliza kwanini wanapewa tuzo kwa kazi wanazolipwa mishahara?
 
Back
Top Bottom