Rais Samia tahadhari na tulia kidogo. Kazi zako Ikulu anazifanya nani?

Samia mnamuonea tu kumuuliza maswali magumu hivi.... ye ni mama shughuli... harusi, vikoba, kitchen party na kisomo.... mambo ya sirikali akuuuu hayajui hata hivyo atakwambia urais ni taasisi wapo wanaofanya kazi ye kutia siginecha tu zinduzi na uzungu fulani aaah ndio mahali pake... anamwita waziri jina kwa kufupisha... Mwanangu Inno yaani anabembeleza... then utegemee huyu atatulia kupitia madodoso na taarifa za kaguzi,
 
Ningekuwa Admini wa Jamii Forum ninge kuleftisha.

Wewe ni hasara kuwemo humu.

Wanaweka mambo ya msingi wewe unakuja kudharau hadi majukumu ya Rais.

Unataka kuwa ceremonial president?.

wewe hujui muundo wa uongozi wa hii nchi.
 
Hizo si qualities nzuri za Urais.
Kudelegate sawa lakini hata aliye delegetiwa inabidi maamuzi yake yapitiwe kwenye hiyo ngazi ya juu.
Sio kila jambo linatakiwa kuwa delegated.

Kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya yeye mwenyewe lakini hayafanyi anadelegate.

Na matatizo mengi awamu hii yanatokana na mapungufu hayo.
 
Kuna kingine huwa anawaza zaidi ya tozo akiwa ofsini !!!?
Bora asasfiri akitulia mjue anakuja na tozo amesema hana maajabu
ya kujaza mifuko yenu.
 
Nafikiri hata mama akiwasoma humu hawaelewi anawashangaa tu. Kwake mambo ni mazuri ila tatizo ni vita Ukraine na Urusi!

Nyerere aliyeisuka hii nchi alisema CCM ikiyumba nchi itayumba. CCM imetoka kwenye misingi ya kuandaa viongozi wenye maono na uwezo wa kutuongoza zama hizi za dunia iliyojaa hila za kila namna.

CCM imechoka, CCM inahitaji mtifuano wa reformation maana bado hatuna chama mbadala kilicho tayari kushika dola kwasasa.
 
Anatuonesha mfano sisi wababa tunaokimbia familia, kwamba hata ukikimbia kuna watu watakulelea hasa kama mkeo bado anaita akipita barabarani. Sasa kwenye kulelewa kubali siku ukirudi familia inaweza isikuheshimu maana hukuonesha nia ya kuijali na kuipenda familia yako. Kuna wakati matukio mengine ni kumuagiza msaidizi wako we unabaki ofsini kutafakari na kuamua baadhi ya mambo nyeti ya nchi.
 
born town,mzee, tanzanite,sk gang wanampa pressure, she is just hanging in the air; hajui hata la kufanya.Bado anawaza atalimpa ngapi mzee kwa ku-play role ya informer.
Duh !!
 
Ningekuwa Admini wa Jamii Forum ninge kuleftisha.

Wewe ni hasara kuwemo humu.

Wanaweka mambo ya msingi wewe unakuja kudharau hadi majukumu ya Rais.

Unataka kuwa ceremonial president?.

wewe hujui muundo wa uongozi wa hii nchi.
Sasa si una akili ndogo ndio maana huwezi kufikiria, ceremonial president ndio nini? Nani huyo ambae ni ceremonial? Nani anafanya Kazi za Rais ?

Usiwe ndezi
 
umejuaje juaje kama hatulii,pia ujue mikoa yote kuna ofisi ya rais
 
Mara zote mnatwambia urais ni taasisi. Vipi leo? Tulipowauliza kwa nini hawataki akae ofisini mlitujibu hivi hivi.
 
Unachekesha,kuna Nchi bei za mafuta Kwa Lita ni hadi 6,000 na chakula kinafika mjini..

Kwa akili zako ndogo,those days wakati mafuta ni Bei chini lakini barabara haziko Vijijini mbona chakula kilikuwa kinafika mjini Kwa bei kubwa?

Nasema hivi hakuna serikali itafuta Kodi za maana kwenye mafuta na ambazo sehemu kubwa zinatumika kwenye road fund,Tarura,TanRoads na kwenye maji Ili tuu wewe ununue mafuta Kwa bei ya chini,narudia hakuna..

Zaidi tuu serikali itakachofanya ikijitahidi ni kupunguza walau sh.300.
 
Naunga mkono hoja. Ni wakati sasa Rais Samia atembelee mikoa ya Nyanda za Juu yaani Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe na Rukwa.

Kudanganyika kuwa kura za urais zinaamuliwa na Kanda ya Ziwa ambako ametembelea zaidi ya mara 7 toka aapishwe kuwa Rais kutampotezea kura mikoa hii muhimu kwenye uchumi wa Tanzania
 
Kwa wale fuata mkumbo na watu wa kujazwa chuki bila kutumia akili zao nataka muelewe hivi,

Rais wa JMT ambaye ndiye Amiri jeshi mkuu, kila siku ya Mungu anapewa daily briefing ya nchi nzima na ndio sababu ofisi zote za serikali asubuhi uanza na vikao, Polisi kuna morning call, Usalama wa Taifa hivyo hivyo then repoti zote za hali ya nchi zinafika kwa Rais.

Msimchukulie powa mama kwakuwa kaamuwa kuwarudishia Uhuru sasa mnataka kumpanda kichwani.

Naona mmeshasahau alivyowaonesha demo tu kwa Freeman Mbowe mlikuwa mnalialia humu.

Mnachokitaka mtakipata tu, Mungu huwa anajibu maombi, tuendelee kuomba kwa bidii turudishwe kwenye utawala wa kishetani Mungu atajibu maombi.

Mkiona kuna weakness kwenye utawala tumieni na nyinyi hizo weakness kupiga pesa na kuboresha maisha yenu na siyo kuwa na ulalamishi usiokuwa na kikomo.
 
Pengine uko mwezini maana hujaona migomo ya daladala.
Ma V8 mnayoendeshwa na mafuta ya bure na ving'ora yanaweza kuwatokea puani!
 
Mpango na Majaliwa wana kazi gani? Mnataka yeye awe ndo mfungua barabara, mpokea ndege ingawa naye alizipokea juzi, yeye huyu awe mtu wa kufukuza watu majukwaani? Kweli kweli. Mwalimu hakuna nchi hakuitembelea. Hata Bangladesh alipatembelea mara tatu. Je huko nako kulikuwa na nini? Samia anakwenda kukwamua nchi ila watakao kuwa hai wataweza kuona matunda ya kazi anayotukaniwa sasa.

Kama mlienda kwa mzee wa kikombe mkarudi mikono mitupu na hakuna aliyekaa kwenye key board kusema sasa huyu anayerudi na kitu na vingine vimeanza kuonekana kwanini tusimvumilie? Nchi nzima ilisimama kwenda kwa mzee wakikombe sijui huko wanaongea nini na mwendazake? Sijui walio hai wanajifunza nini kwa kuamini mambo ya kufikirika kuliko kutumia juhudi na maarifa. Kusoma kwingi siyo kuwa na maarifa.
 
Soma vizuri hoja uielewe.
Hakuna anyetaka kurudi Misri ya Mwendazake, if anything kule ilikuwa utumwani.
Tnachoona ni kumtakia Mama utawala bora ukiwa na maana atulie na kuonekana anaendesh mambo kadri ya matakwa ya wananchi.
CAG kaonyesha madudu, bado ngoma droo, na mambo yako kwenye mafaili!
Hapo unasemaje.
 
Midomo kwenye keyboard. Mbona hawaongei kwenye kadamnasi.
 
Sasa kila mtu akiwa anaijbia serikali, si nchi itaanguka? Pia kumbuka ww unaweza kutumia loophole kupiga, vipi wale wasiokua na hiyo loophole na ndio majority ya watanzania.
Serikali ifnaye kazi yake kuletea Maendeleo wananchi na sio kusema watu wapige kwenye loophole
 
Midomo kwenye keyboard. Mbona hawaongei kwenye kadamnasi.
Kadamnasi gani ambayo watu hawaongei? Unatkaa waende ikulu kuongea? Huku kwetu watu wanaongea kila leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…