#COVID19 Rais Samia: Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa Corona. Chanjo itakuwa ya hiyari

#COVID19 Rais Samia: Tanzania kuna wagonjwa zaidi ya 100 wa Corona. Chanjo itakuwa ya hiyari

Mimi nina mwezi na nusu tangu nichanje full. Naendelea kuvaa barakoa kwani najua chanjo si kinga asilimia 100. Ila ukichukua chanjo ukajumlisha barakoa, distancing , kujisanitize au kunawa unakaribia kabisa kujikinga kwa asilimia 100.

Dunia ina lengo la kuukomesha ugonjwa huu. Katika lengo hilo ndipo zinakuja hatua mbalimbali ikiwemo kutoa fedha ili kuziwezesha nchi masikini ( Afrika) . Hata Ulaya zipo nchi zimewezeshwa kifedha ili kupigana na covid 19.

Wanaoona hizi fedha ni mtego ni wivu wao tu unawasumbua. Mbona hapo awali hawakusema ni mtego au kwavile zilichukuliwa kimyakimya zikawekwa mifukoni mwa miungu yao!

Mama endelea kuupiga mwingi. Unafanya kazi inayoonekana , siyo blabla tulizokuwa tunaimbiwa na wale watesaji.
Sasa hapo chanjo ya nini bwashee.
 
Akili ya Lissu = akili ya Kabudi x 100
Hiyo ni Lissu na Kabudi je vp wewe akili yako kwa Lissu ni sawa na nini? Angalieni isije siku mkalinganisha hadi na Mungu huyo Lissu wenu.
 
Huyu alikufa kwa fedheha kubwa hadi watu wanaficha bana!
Ndio ueleze hiyo fedha ni ipi katika kifo chake? Kama Mungu alitaka kumfedhehesha hakuna binaadamu wa kuweza kuficha sasa niambie hiyo fedha ni ipi?
 
Hiyo ni Lissu na Kabudi je vp wewe akili yako kwa Lissu ni sawa na nini? Angalieni isije siku mkalinganisha hadi na Mungu huyo Lissu wenu.
Mkuu upo!! Hvi ikitokea Chanjo ya Covid ikadaiwa kama yellow fever kila unaposafiri nje je una maoni gani juu ya hilo? Au upo radhi waTZ tusiwahi safiri nje?
 
Mkuu upo!! Hvi ikitokea Chanjo ya Covid ikadaiwa kama yellow fever kila unaposafiri nje je una maoni gani juu ya hilo? Au upo radhi waTZ tusiwahi safiri nje?

Yellow fever Watanzania wengi wanajichanja kwa kutumia chanjo ya miwa. Kulikoni corona? Acheni watu wajichanje kwa chai za michai chai ,mdalasini, hiliki na tangawizi. Serikali ibakie kutoa hati za vyeti.
 
Jf kuna wapumbavu wengi sana wanaomiliki smartphones. Imagine mtu atajitokeza anasema "hatutaki chanjo" wewe na nani mbwa wewe? Yaani lile jamaa likufe tena

We dalali wa chanjo usituletee mahasira yako ya ajabu ajabu.

Hayo machanjo yenye sumu ukajidunge wewe na mmeo!!
 
Rais Samia amesema wafanyabiashara wengi wa Kitanzania wameshachanja chanjo ya Corona wengine Dubai, SA na Nairobi.

Rais amesema baraza la mawaziri limekaa na kuamua tukubaliane na chanjo na iwe ni hiyari.

Serikali imeshatenga usd 470 milioni kukabiliana na covid 19.

Nawasalimu kwa jina la JMT.



---
Kuna wanaoona hatuko serious ktk mapambano dhidi ya #COVID19. Nilipoingia madarakani nilitamani tupambane na ugonjwa huu kama wanavyofanya mataifa mengine. Tanzania tuna wagonjwa zaidi ya 100 wenye #coronavirus #wave3, kati yao Wagonjwa 70 naa, wapo kwenye mitungi na wengine matibabu ya kawaida.

Tumeamua tukubali chanjo kwa walio tayari.

Tanzania tumeingia kwenye #COVAX community. Wataalamu wetu wanafanyia kazi Chanjo ipi inafaa kwa Watanzania. Kuna mashirika mengi wamejitokeza kutaka kusaidia Watanzania lakini lazima wataalamu wetu ndio watoe ushauri kitaalamu.

Sisi kama Serikali tunahimiza yale yanayoshauriwa na wataalamu; kama unaamini kwenye kupiga nyungu - wewe piga. Kila mmoja atekeleze wajibu wake. Jikingeni sana na wakingeni watoto.


Abdala naona iko poa sana...
 
Nimeshaliandaa BEGA langu KUCHANJWA.

Ninaisubiria kwa hamu siku hiyo ya KUCHANJWA.
Dalali lingine hili hapa... hahahaaa....

Yaani nyinyi, thubutu yenu!

Hayo machanjo yataoza huko kwenye maboksi maana wananchi hawataki hata kuyasikia.

Mmebaki nyinyi madalali wachache mitandaoni mnajibaraguza tu hapa na pale.

Huku mtaani mambo ni tofauti sana!
 
Yellow fever Watanzania wengi wanajichanja kwa kutumia chanjo ya miwa. Kulikoni corona? Acheni watu wajichanje kwa chai za michai chai ,mdalasini, hiliki na tangawizi. Serikali ibakie kutoa hati za vyeti.
Samia kasema zipimwe then zirasimishwe!! Hoja yangu ni kwamba kma sio globally certified na taasisi kma EMA au WHO je fate ya waTanzania wataotaka kusafiri kipindi hicho itakuaje?
 
Ya kwako ambayo haina sumu iko wapi?.au unabwabwaja tu uku kichwani ukiwa empty set.
Hayo machanjo hayana faida yoyote ile zaidi ya kuharibu tu mfumo wa DNA.

Kwanza hakuna mtu anayeugua corona — mna viherehere tu vya kushabikia machanjo ya ajabu ajabu
 
Hizo takwimu za wagonjwa kwanini zisiwe zinatolewa kwa public?

Rais anajitahidi sana kuendana na kile WHO wanataka, ningependa atuambie hao wagonjwa wamelazwa hospitali zipi? familia zao wameziweka karantini? na mikoa ipi inaongoza kwa maambukizi.

This is a wake up call, tuamke, ile likizo ya Corona imeisha, now kirusi kipo mjini.
Ilikuwa likizo ya kutosema, lakini corona ilikuwapo inatafuna tu
 
Samia kasema zipimwe then zirasimishwe!! Hoja yangu ni kwamba kma sio globally certified na taasisi kma EMA au WHO je fate ya waTanzania wataotaka kusafiri kipindi hicho itakuaje?

Watapewa vyeti kama wa yellow fever wanavyopewa. Kwani ulishasikia Mtanzania karudishwa/ kuzuiwa kuingia nchi flani kwa vile amejichanja yellow fever kwa kutumia juice ya miwa ya kipemba iliyochanganywa na ndimu?
 
Amesema ni zaidi 100 hivyo hata maelfu ni zaidi ya 100. Kuna mikoa kama Kilimanjaro na Arusha Hali si shwari kabisa. Nasikia pia Mwanza bila kusahau Baba Lao DSM.
Duuh tumerudi kulekule,na vile tulivyokua wazembe, hatukuwahi kuchukua tahadhali tuliishi kwa mazoea
 
Covid -19 ipo sana na inaua. Tuwaige jirani zetu wa Kenya ambao leo wametangaza kuwa ifikapo Oktoba, 2021 watakuwa wamechanja wananchi wao millioni 10 na ifikapo mwaka kesho Oktoba 2022 watakuwa wamechanja wananchi wao millioni 26.

Kama chanjo ni kitu kilichopendekezwa na watalaam kwa nini sisi Tanzania tusichukue hatua za haraka?. Kila kukicha watu wanakufa tena nguvu kazi ambao wanategemewa. Inabidi tuamke na kuchukua hatua za haraka sana.
 
Back
Top Bottom