Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Mkuu .....Sababu zilizotolewa ni dhaifu sana tukichukulia zinatolewa na Mkuu wa nchi yaani Rais wa JMT. Ni sababu dhaifu sana. Katao sababu gani za kushawishi umma uamini hapo mwanzo tulikosea. Wimbi la kwanza anakubali corona haikuwa na madhara makubwa. Kama ndio hivyo kwa nini njia zilizotumika katika wimbi la kwanza zisiendelee kutumika tunahamia kwenye chanjo ambayo hatujui kwa uhakika ni ipi tuitumie?
Wafanyabiashara wamesha chanjwa huko nje ya nchi wanaendelea
na shughulia zao. Hii ndio sababu inaweza kutolewa na Mkuu wa nchi?! Jamani sasa kama wamechanjwa ndio iweje?
Lakini usisahau kuwa TULIPIGANA KIIMANI ZAIDI dhidi ya UVIKO....
Hayati JPM alitushajiisha moyo mkuu wa kupambana na UVIKO kiimani sana.... Japo hesabu zake zilikuwa zinawiana na SAYANSI pia kuwa TUKIPAMBANA nao...UKITUPIGA utaifanya MIILI YETU itengeneze KINGA dhidi ya UVIKO....
Labda wataalamu wetu wameona pamoja na miili KUTENGENEZA kinga hiyo ila kumetokea MADHARA MAKUBWA (idadi ya walioathirika vibaya sana)......
Kwa hiyo wataalamu wameonelea TUPAMBANE NA UVIKO kwa kuchoma CHANJO ambayo itasaidiana na YALE MAPAMBANO aliyoasisi hayati JPM......
Mkuu usisahau kuwa Kuna kitu kinaitwa TOUGH DECISION MAKING....ambayo ni sawa na "weighing scale"......
Mkuu bado huwezi kujitenga na DUNIA.....mama amesema kuwa TUENDELEE NA KILA AINA YA MBINU ZA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO na chanjo ikiwemo ndani yake....ubaya uko wapi ?!!!!
KINGA NI BORA KULIKO TIBA!!!