Ni jambo la aibu sana kukopa pesa za kujenga stand.
Waafrika ns watanzania kwa ujumla wanaongozwa na ubinafsi wa kisiasa.
Nchi hii imekua ni uCCM na madaraka tu ndiyo ajenda ya watawala. Hawawazi kabisa kuhusu maendeleo ya wananchi na uwekezaji wa ndani .
Tumejaza watawala wabinafsi.
Tumesimama na katiba ya kuwaneemesha watu wabinafsi.
Tumeamua kusimama na katiba inayowaneemesha watu wanaoangalia uchaguzi tu na kurudi madarani.
Hii ni aibu kubwa na janga kwa Taifa. Kuna jambo nililisikia kuwa awamu ya Tano ililenga kuleta katiba mpya Baada ya uchaguzi mkuu wa 2025. Nadhani Katiba mpya ni Muhimu sana ili wananchi wachague watu kwa sera bora na sio kwa kutumia mabomu na risasi kama ilivyo sasa.
Stand ni biashara kubwa sana za Halmashauri za miji na majiji. Hakuna sababu ya kusubiri pesa toka kwa Rais wakati Jiji linaweza kuwekeza kwenye Miradi ya stand na kupata mapato zaidi huku wananchi wakiendelea kupata huduma bora.
Hivi kweli Jiji la Arusha kwa miaka 60 ya Uhuru halina uwezo wa kujenga Stand au ni hujuma tu ya watawala kutaka kuonekana kuwa wanafanya kila kitu kwa utashi wao wa kisiasa?
Hivi kweli Jiji la Arusha linashindwa kuingia mkataba na wafanyabidhara wa ndani pale Arusha wakajenga stand ya kisasa kwa makubaliano ya miaka 20 wakiwa wanachangia na Jiji kwenye kukusanya mapato ili kurudisha fedha zao.?
Kwa nini tukope toka nje wakati tuna wafanyabiashara wa ndani wanaoweza kuwekeza kwenye stand kwa kushirikiana na mabenki. Stand sio huduma ya bure bali inalipiwa mpaka choo. Kwa Jiji la Arusha ingejengwa stand yenye ukumbi mkubwa na mabaa na magrocery na maduka ingekua ni mradi mkubwa sana.
Yaani hata yale yanayoweza kufanywa na wazawa bado tunataka wageni watupe pesa.
Wananchi wanataka huduma bora sio siasa. Wanasiasa wanataka madaraka sio huduma bora.
Ndio maana tunataka katiba mpya ili tuweze kuwachagua watu wenye ushindani na hoja za ushindani zenye kufikirisha sio kama ilivyo sasa CCM nguvu yao kubwa ni kuweka watu wa kulinda ,Chama kitawale hata kwa nguvu ya majeshi, huo ni ujinga mkubwa kwa watawala Raia kutumia majeshi kuumiza na kuua watanzania ambao ni ndugu moja ili kulinda watu wachache ili tu wajineemeshe kwenye madaraka na kurithisha watoto wao madaraka.Mara sijui CCM inalinda amani ya nchi wakati kuna majeshi ambayo yamepewa kazi hiyo na wanalinda amani ili wanasiasa wasijiingize kwenye majeshi na kugawa majeshi yetu , yani watu wakiingia madarakani hawatumii tena maarifa makubwa Bali wanatumia muda mwingi kulinda nafasi zao ,mara sijui mitano tena, sijui mapinduzi daima. Wanalinda vimaneno vya ajabu ajabu vinavyowaneemesha wachache huku mambo ya wananchi kama Stand ,makazi bora ,ajira na afya vikiachwa ili viwe kamba ya kuwanyongea wale wanaowatamkia hadharani kuwa wanyongwe.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app