Rais Samia, tusifukie Mahindi na Maharage ya Marekani, naomba tuyapeleke Haiti

Rais Samia, tusifukie Mahindi na Maharage ya Marekani, naomba tuyapeleke Haiti

Marekani hajaanza leo kutoa misaada humu Nchini na Duniani !

Sisi tulishakula uji wa Burgoo tukiwa Shuleni enzi zile na pia tulikula unga wa Yanga sana tu enzi zile. !!

Wazungu wakitaka kutudhuru zipo njia nyingi za siri wanaweza kuzitumia sio kwenye Chakula !!
Wenzetu sio mazuzu kiasi hicho !

Watu wanaogopa biashara zao zitabuma. [emoji120][emoji120]
Hakuna kitu kinaitwa msaada wewe fungua ubongo huo
 
Huyu Bashe aache upuuzi kwenye mambo ya maana...., Hayo Mazao yaliyojaa Tanzania ayanunue yeye na kuwapa misaada watu kitaa wanaolalamika hali ya maisha ni ngumu....

Yaani siku hizi ni mwendo wa Maigizo na Propaganda tu.....
 
Kuna wakimbizi hapo kigoma hawana chakula tuwapelekee. Wapewe UNHCR wawape hao wakimbizi
 
Siasa ni kilimo.
Tanzania 🇹🇿 hakuna njaa.🙂
 
Miaka ya 90,tulipewa Msaada wa mahindi ya njano kutoka USA! Tukayala Sana! Kelele zilipigwa nyingi Sana, eti watoto watakufa, Leo Sisi ndio madingi,na wengine tuna wajukuu! Kama huo mchele upo, kwanini haushuki bei sokoni!?
Swala la kusema wangechukua mchele wetu wakatia virutubisho, ndio wakatuuzia!? Ni akili ya kijinga!
Pesa wanatoa wao, lazima wanunue kwa wakulima wao! Ni akili ndogo tu!
Mbona wa china wakitupa msaada wa kujenga flyover, huwa hatuwaambii watupe pesa, harafu mkandarasi tuchague wenye we!?
Wanatupa mkopo, mkandsrasi wanachagua wenyewekutoka china, na lazima mkopo upitie benk zao!
Hili swala la mchele limethibitisha ukilaza wa namba moja pale magogoni na machawa mawaziri wake
Hata kama ingekuwa ni kweli,siku zote mwambaji hatakiwi kuchagua.
Inasikitisha sana kwa population ya 61M na ardhi ya sq.945K ambayo 3/4 ni arable land kuchukua mahindi na Mchele wa msaada.
 
Yapelekwe ubalozini kwao pale. Mahindi yapo na msimu uliopita tulivuna sana.
 
Huo msosi kuumwaga hiyo ni kufuru na jeuri ya masikini. Umepewa msaada upokee kwa moyo wa shukrani, habari ya kuula au kutoula utajua mwenyewe, lakini mwenye kutoa msaada afurahie msaada wake kupokelewa.
Marekani hajaanza leo kutoa misaada ya vyakula hapa na Duniani. !

Marekani hana ugomvi na Watanzania !
Na hata kule kwenye ugomvi na mahasimu wake huwa anatoa misaada ya vyakula na madawa !
Hatujawahi kusikia wamewekewa virutubisho vya hatari !
Leo ukienda Pakistan na Afghanistan utakutana na watoto wenye polio wengi sana kutokana na huo uzuzu wa kudhani eti wazungu wakileta misaada ama ya chakula au chanjo wanakuwa wameweka dawa za ugumba au ushoga !!
Nonsense !
 
Kuna Mahindi ambayo Marekani imetoa msaada kwa Tanzania.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kawa na wasiwasi nayo. Amedai yamewekewa Virutubisho ambavyo havijulikani.

Pia Waziri kasema Tanzania tuna Mahindi mengi hayana Soko, hivyo wangetumia mahindi yetu na kuweka Virutubisho Watanzania wakiwa wanaona.

Mimi napendekeza, kuliko kuyamwaga, Tuchukue hayo Mahindi, Mafuta ya Alizeti na Maharage waloleta, tupakie kwenye ile ndege ya mizigoo ya ATCL tuwape msaada Wananchi wa Haiti wanaokufa Njaa.
Haiti Ni mbali Sana ndege yetu itatumia mafuta mengi,tuwapelekee Sudan kusini na Congo pia.ndege yetu ikipiga round moja tu nshaaaaaaaa isharudi tunaikosha tunaipaki kivulini.
 
Hata kama ingekuwa ni kweli,siku zote mwambaji hatakiwi kuchagua.
Inasikitisha sana kwa population ya 61M na ardhi ya sq.945K ambayo 3/4 ni arable land kuchukua mahindi na Mchele wa msaada.
Inasikitisha sana lakini ni lazima tuchukue huo msaada na tuutumie kwa sababu watu wana hali ngumu za maisha !
Hao wenye magari yenye namba E ambao wamejaa Dar wao haiwahusu hii issue !
Wenzetu wanakula Pizza 🍕 na Burgers 🍔 !
Kama yapo mashaka apewe kazi mkemia Mkuu kuchunguza hivyo virutubisho ni vya aina gani !

Mimi naona hii Conflict of interest kwa vibopa wa hizo biashara Nchini !
“ Acha punda Afe lakini mzigo ufike “
That’s their motto !
 
Haiti Ni mbali Sana ndege yetu itatumia mafuta mengi,tuwapelekee Sudan kusini na Congo pia.ndege yetu ikipiga round moja tu nshaaaaaaaa isharudi tunaikosha tunaipaki kivulini.
Kweli kabisa !
 
Hakuna kitu kinaitwa msaada wewe fungua ubongo huo
Sio msaada ni malipo ya ziada ya madini yetu ya dhahabu ambayo walipewaga kuyachimba kwa bei Cheee na wajanja miaka mingi iliyopita!

Wameona warudishe angalau fadhila kidogo kwa Watanzania !!
Samahanini wenye kurundika mpunga huko kwenye mastoo yao wasubiri watauza hata mwakani !
Ngojeni wenye njaa wasaidiwe kwanza ili wapate nguvu za kulima tena. !
 
Kuna wakimbizi hapo kigoma hawana chakula tuwapelekee. Wapewe UNHCR wawape hao wakimbizi
Na siku zote wakimbizi huwa wanakula vyakula vya USAID !
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa !
Wenye magari ya namba E hawataki kusaidiwa !
Tuleteeni sisi wa Nanjilinji na Nzuginaminzi tunauhitaji huo mchele na mahindi !
 
Kwamba hayo mahindi yakipelekwa Haiti alafu yapimwe na kukuta zinashida nani atawajibika Tanzania au Marekani? Jambo dogo sasa limekuwa ya kisiasa tena siasa yenyewe inasemwa ki rahisi sana.
Kwamba tumeshindwa kuyapima na kuyabaini au yakiingia bila vipimo?
Yaleyale ya Papai amekutwa na Corona.
 
Back
Top Bottom