Rais Samia, tusifukie Mahindi na Maharage ya Marekani, naomba tuyapeleke Haiti

Rais Samia, tusifukie Mahindi na Maharage ya Marekani, naomba tuyapeleke Haiti

Kuna Mahindi ambayo Marekani imetoa msaada kwa Tanzania.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kawa na wasiwasi nayo. Amedai yamewekewa Virutubisho ambavyo havijulikani.

Pia Waziri kasema Tanzania tuna Mahindi mengi hayana Soko, hivyo wangetumia mahindi yetu na kuweka Virutubisho Watanzania wakiwa wanaona.

Mimi napendekeza, kuliko kuyamwaga, Tuchukue hayo Mahindi, Mafuta ya Alizeti na Maharage waloleta, tupakie kwenye ile ndege ya mizigoo ya ATCL tuwape msaada Wananchi wa Haiti wanaokufa Njaa.
Ni mchele siyo mahindi wee mzee. Halafu vigezo na masharti kuzingatiwa: msaada uliopewa huwezi baadaye kuugawa kwa yeyote asiye mlengwa
 
Waziri Bashe ndo kaharibu kabisaaaa

Badala ya kuseek info sahihi kutoka ubalozini, yeye kaenda kwenye media na kulalamika kana wapiga udaku wanavyolalamika
Marekani hajaanza leo kutoa misaada humu Nchini na Duniani !

Sisi tulishakula uji wa Burgoo tukiwa Shuleni enzi zile na pia tulikula unga wa Yanga sana tu enzi zile. !!

Wazungu wakitaka kutudhuru zipo njia nyingi za siri wanaweza kuzitumia sio kwenye Chakula !!
Wenzetu sio mazuzu kiasi hicho !

Watu wanaogopa biashara zao zitabuma. 🙏🙏
 
Hawa jamaa kwani Tz tumeeenda kuwalilia lini shida za vyakula hakuna mzungu mwenye urafiki na mtu mweusi kutoka Africa kiasi Cha kutoka msaaada bila kuombwa tumia akili yako si lazima kiongozi aongee hata wewe unatakiwa kujiongeza
 
Huo msosi kuumwaga hiyo ni kufuru na jeuri ya masikini. Umepewa msaada upokee kwa moyo wa shukrani, habari ya kuula au kutoula utajua mwenyewe, lakini mwenye kutoa msaada afurahie msaada wake kupokelewa.
 
Hata kama ni mimi nimetoa msaada halafu msaada wangu ukanyanyampaliwa, aisee nitakata tamaa na siku nyingine sitatoa msaada kwa huyo masikini jeuri kama atapata shida na anahitaji msaada atajibeba mwenyewe. Masikini ana nyodo sana halafu hana uwezo. TBS, mamlaka ya chakula wapo, wameshindwa nini ku prove hivyo virutubisho kama vinafaa kwa afya
 
Hii mada ikibaki Hai basi babu yako alikuoika kweli kweli yaani.

Mada kama hii ilitupwa jalalani huko kisa virutubisho daaa!.
 
Kiongoz muwe waelewa bas na wakati mwingine mjithamin

Umeshaambiwa wameyatilia shaka sasa ww unataka ya nini?

Vimba kaka hata kama unanjaa, bule ni aghali

Tusipende sana mterezo we kula uote manyonyo bas

Maana watanzania sijui mnashida gan mkiambiwa kitu mnataka kufanya majaribio ngoja sasa watoto wenu wawe mashoga
SASA BROTHER, MBONA MSAADA WA ARV HAMUUKATAI? AU MNAFIKIRI WANASHINDWA KUWEKA HIVYO VIRUTUBISHO MNAVYOVIHOFIA HUKO?
 
Kuna Mahindi ambayo Marekani imetoa msaada kwa Tanzania.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kawa na wasiwasi nayo. Amedai yamewekewa Virutubisho ambavyo havijulikani.

Pia Waziri kasema Tanzania tuna Mahindi mengi hayana Soko, hivyo wangetumia mahindi yetu na kuweka Virutubisho Watanzania wakiwa wanaona.

Mimi napendekeza, kuliko kuyamwaga, Tuchukue hayo Mahindi, Mafuta ya Alizeti na Maharage waloleta, tupakie kwenye ile ndege ya mizigoo ya ATCL tuwape msaada Wananchi wa Haiti wanaokufa Njaa.

Tanzania wanajifanya maskini jeuri. Yaani miaka ya 78 na mwanzo mwa 80 nchi nzima ilikula sembe la USA .. tena ilikuwa ni kile kipindi ambacho tulikuwa tunajiita wajamaa (Ka Noth Korea kadogo ka Afrika). Sasa si wangetumaliza wote tu kwa kutumia hilo sembe ..... anyway, wawapelekee Sudan ... kuna watu wanakufa kwa njaa na vita.
 
Kuna Mahindi ambayo Marekani imetoa msaada kwa Tanzania.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kawa na wasiwasi nayo. Amedai yamewekewa Virutubisho ambavyo havijulikani.

Pia Waziri kasema Tanzania tuna Mahindi mengi hayana Soko, hivyo wangetumia mahindi yetu na kuweka Virutubisho Watanzania wakiwa wanaona.

Mimi napendekeza, kuliko kuyamwaga, Tuchukue hayo Mahindi, Mafuta ya Alizeti na Maharage waloleta, tupakie kwenye ile ndege ya mizigoo ya ATCL tuwape msaada Wananchi wa Haiti wanaokufa Njaa.
Miaka ya 90,tulipewa Msaada wa mahindi ya njano kutoka USA! Tukayala Sana! Kelele zilipigwa nyingi Sana, eti watoto watakufa, Leo Sisi ndio madingi,na wengine tuna wajukuu! Kama huo mchele upo, kwanini haushuki bei sokoni!?
Swala la kusema wangechukua mchele wetu wakatia virutubisho, ndio wakatuuzia!? Ni akili ya kijinga!
Pesa wanatoa wao, lazima wanunue kwa wakulima wao! Ni akili ndogo tu!
Mbona wa china wakitupa msaada wa kujenga flyover, huwa hatuwaambii watupe pesa, harafu mkandarasi tuchague wenye we!?
Wanatupa mkopo, mkandsrasi wanachagua wenyewekutoka china, na lazima mkopo upitie benk zao!
Hili swala la mchele limethibitisha ukilaza wa namba moja pale magogoni na machawa mawaziri wake
 
Uandishi ni kazi sana,yani kwa namna ulivyoandika hii habari haijulikani either ni maneno ameyasema SAMIA,Bashe au ni ushauri wako katika hilo swala.
 
Kiongoz muwe waelewa bas na wakati mwingine mjithamin

Umeshaambiwa wameyatilia shaka sasa ww unataka ya nini?

Vimba kaka hata kama unanjaa, bule ni aghali

Tusipende sana mterezo we kula uote manyonyo bas

Maana watanzania sijui mnashida gan mkiambiwa kitu mnataka kufanya majaribio ngoja sasa watoto wenu wawe mashoga
Wewe na Bashe wote hamna akili, TBS na TFDA kazi ya msingi ni ipi?
 
Mimi napendekeza, kuliko kuyamwaga, Tuchukue hayo Mahindi, Mafuta ya Alizeti na Maharage waloleta, tupakie kwenye ile ndege ya mizigoo ya ATCL tuwape msaada Wananchi wa Haiti wanaokufa Njaa.

Ni wewe au Bashe, au Rais ndie amependekeza hili?
 
Back
Top Bottom