Rais Samia, tusifukie Mahindi na Maharage ya Marekani, naomba tuyapeleke Haiti

Uandishi ni kazi sana,yani kwa namna ulivyoandika hii habari haijulikani either ni maneno ameyasema SAMIA,Bashe au ni ushauri wako katika hilo swala.
Ndio nami nimemuuliza ni mapendekezo yake au ya bashe/rais!
 
Hakuna kitu kinaitwa msaada wewe fungua ubongo huo
 
Huyu Bashe aache upuuzi kwenye mambo ya maana...., Hayo Mazao yaliyojaa Tanzania ayanunue yeye na kuwapa misaada watu kitaa wanaolalamika hali ya maisha ni ngumu....

Yaani siku hizi ni mwendo wa Maigizo na Propaganda tu.....
 
Kuna wakimbizi hapo kigoma hawana chakula tuwapelekee. Wapewe UNHCR wawape hao wakimbizi
 
Siasa ni kilimo.
Tanzania 🇹🇿 hakuna njaa.🙂
 
Hata kama ingekuwa ni kweli,siku zote mwambaji hatakiwi kuchagua.
Inasikitisha sana kwa population ya 61M na ardhi ya sq.945K ambayo 3/4 ni arable land kuchukua mahindi na Mchele wa msaada.
 
Yapelekwe ubalozini kwao pale. Mahindi yapo na msimu uliopita tulivuna sana.
 
Huo msosi kuumwaga hiyo ni kufuru na jeuri ya masikini. Umepewa msaada upokee kwa moyo wa shukrani, habari ya kuula au kutoula utajua mwenyewe, lakini mwenye kutoa msaada afurahie msaada wake kupokelewa.
Marekani hajaanza leo kutoa misaada ya vyakula hapa na Duniani. !

Marekani hana ugomvi na Watanzania !
Na hata kule kwenye ugomvi na mahasimu wake huwa anatoa misaada ya vyakula na madawa !
Hatujawahi kusikia wamewekewa virutubisho vya hatari !
Leo ukienda Pakistan na Afghanistan utakutana na watoto wenye polio wengi sana kutokana na huo uzuzu wa kudhani eti wazungu wakileta misaada ama ya chakula au chanjo wanakuwa wameweka dawa za ugumba au ushoga !!
Nonsense !
 
Haiti Ni mbali Sana ndege yetu itatumia mafuta mengi,tuwapelekee Sudan kusini na Congo pia.ndege yetu ikipiga round moja tu nshaaaaaaaa isharudi tunaikosha tunaipaki kivulini.
 
Hata kama ingekuwa ni kweli,siku zote mwambaji hatakiwi kuchagua.
Inasikitisha sana kwa population ya 61M na ardhi ya sq.945K ambayo 3/4 ni arable land kuchukua mahindi na Mchele wa msaada.
Inasikitisha sana lakini ni lazima tuchukue huo msaada na tuutumie kwa sababu watu wana hali ngumu za maisha !
Hao wenye magari yenye namba E ambao wamejaa Dar wao haiwahusu hii issue !
Wenzetu wanakula Pizza 🍕 na Burgers 🍔 !
Kama yapo mashaka apewe kazi mkemia Mkuu kuchunguza hivyo virutubisho ni vya aina gani !

Mimi naona hii Conflict of interest kwa vibopa wa hizo biashara Nchini !
“ Acha punda Afe lakini mzigo ufike “
That’s their motto !
 
Haiti Ni mbali Sana ndege yetu itatumia mafuta mengi,tuwapelekee Sudan kusini na Congo pia.ndege yetu ikipiga round moja tu nshaaaaaaaa isharudi tunaikosha tunaipaki kivulini.
Kweli kabisa !
 
Hakuna kitu kinaitwa msaada wewe fungua ubongo huo
Sio msaada ni malipo ya ziada ya madini yetu ya dhahabu ambayo walipewaga kuyachimba kwa bei Cheee na wajanja miaka mingi iliyopita!

Wameona warudishe angalau fadhila kidogo kwa Watanzania !!
Samahanini wenye kurundika mpunga huko kwenye mastoo yao wasubiri watauza hata mwakani !
Ngojeni wenye njaa wasaidiwe kwanza ili wapate nguvu za kulima tena. !
 
Kuna wakimbizi hapo kigoma hawana chakula tuwapelekee. Wapewe UNHCR wawape hao wakimbizi
Na siku zote wakimbizi huwa wanakula vyakula vya USAID !
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa !
Wenye magari ya namba E hawataki kusaidiwa !
Tuleteeni sisi wa Nanjilinji na Nzuginaminzi tunauhitaji huo mchele na mahindi !
 
Kwamba hayo mahindi yakipelekwa Haiti alafu yapimwe na kukuta zinashida nani atawajibika Tanzania au Marekani? Jambo dogo sasa limekuwa ya kisiasa tena siasa yenyewe inasemwa ki rahisi sana.
Kwamba tumeshindwa kuyapima na kuyabaini au yakiingia bila vipimo?
Yaleyale ya Papai amekutwa na Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…