Rais Samia: Tuziangalie Sheria za Uchaguzi zisiwanyime haki wanaokosea kuandika majina yao

Rais Samia: Tuziangalie Sheria za Uchaguzi zisiwanyime haki wanaokosea kuandika majina yao

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania anapoakea ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2020, Ikulu Dar. Katika Uchaguzi huo, Mgombea wa CCM Hayati Rais John Magufuli akiwa na Samia Suluhu kama Mgombea mwenza walishinda

Rais Magufuli alipofariki Machi 2021, aliyekuwa Mgombea mwenza Samia Suluhu akaapishwa kuwa Rais



Rais Samia: Tuziangalie sheria zisiwanyime haki wanaokosea kuandika majina yao

Rais Samia Suluhu amesema sheria za uchaguzi ziangaliwe ili zisiwanyime haki wagombea kwa makosa ya kiufundi

Makosa hayo ni kama kukosea herufi za jina lake au la chama
=====

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema Uchaguzi MKuu wa Mwaka 2020 uligharimu Tsh. 262,493,380,671 ambayo iligharamia ununuzi wa Karatasi za kupigia kura, Mafunzo, Ununuzi wa masanduku na uchapishaji nyaraka
-
Pamoja na gharama hiyo, jumla ya Tsh. 154,313,824,607.88 ilitumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
-
Tume ya Taifa imesema gharama zote ziligharamiwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

NEC: TULIPOKEA RUFAA 165 NGAZI YA UBUNGE
-
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeripoti kupokea jumla ya rufaa 165 za Ubunge ambapo, rufaa 67 zilizotaka Wagombea kurudishwa kwenye kinyang’anyiro zilikubaliwa, 31 zilikataliwa. Rufaa 4 zilizotaka Wagombea kuondolewa zilikubaliwa
-
Wasimamizi wa Uchaguzi walipokea mapingamizi 1,298 ambapo mapingamizi 451 yalishindwa kuamuliwa na kufika Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo Wagombea Udiwani 235 walikubaliwa kurejea katika kinyang’anyiro, mapingamizi 154 yalikataliwa. Rufaa 62 zilizotaka Wagombea kuondolewa zilikataliwa

Rais Samia: Uchaguzi tuligharamia wenyewe, ulimwengu haukuamini kama tungeweza kugharamia wenyewe

Nawapongeza watanzania wote kwa uchaguzi mzuri uliofanyika mwaka jana

Rais Samia, Niwaombe wadau waangalie mapendekezo yaliyotolewa na wayalete serikalini tuangalie namna ya kuyafanyia kazi

Pendekezo la kusaidia taasisi za kiraia na kuwa na wasimamizi wa uchaguzi hadi ktk halmashauri kunaongezea gharama serikali
 
Afu uchaguzi wa Zambia last week haumsuti? Na ataenda kuhudhuria kuapishwa kwa rais aliyeshinda kihalali kabisa - mfano bora wa demokrasia barani Afrika.
Tz tunakwama wapi nasi kuwa mfano?
kwani akili yako invyokutuma ni kuwa akishinda mpinzani ndiyo kashinda kihalali?
 
hela zimeliwa vibaya mno maana kiukweli hakukuwa na uchaguzi kama ni karatasi za kupigia kura mbona zilizagaa mitaani na wengine kukamatwa nanvyo kwenye viroba.

Hapa Raisi aliepo itabidi aitishe uchunguzi kujua kila sentitano ilipotea vipi.
 
Bora aikatae hio ripoti au aipokee kwa shingo upande na kueleza kuwa ameivunja hiyo tume iliyoandaa ripoti,aloo wanamdanganya Raisi maana haya au ukisikia manyago ndio haya. Mijitu mizima.
 
Uchaguzi ujao wapite woooote bila ya kupingwa.
 
Kitakachosemwa kwenye hafla hiyo: Mbona wagombea walioshindwa hawakuenda mahakamani?[emoji23][emoji23][emoji23]
Mbowe anashinda kila uchaguzi na yeye anatumia polisi

USSR
 
Back
Top Bottom