Leo rais wa Tanzania ameyakusanya makundi ya wanawake jijini Dar na kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania kwa sasa inajipanga kuwahakikisha 2025 rais wa Tanzania lazima awe mwanamke, tena mwanamke mwenyewe ni yeye kwa sababu wanawake wamechoka kuwabeba wanaume kwa miaka mingi, na urais alionao sasa yeye kama mwanamke ameupata kikatiba kwa kudra za mwenyezi Mungu tu hivyo anajipanga kikamilifu kuhakikisha 2025 anakuwa rais wa kuchaguliwa na wananchi hivyo wanawake wajipange kumuunga mkono ili awabebe!
Hii ni kauli ya kibaguzi, kejeli na dhihaka ya kijinsia katika uwanja wa siasa za kidemokrasia hapa Tanzania, na inapaswa kupingwa kwa 100%.
Kwa kuwa Rais Samia ameitoa hiyo kauli hadharani yeye mwenyewe na sisi watanzania tumjibu hadharani, tunasema hatutaki utawala wa kijinsia wala urais wa kijinsia hapa Tanzania.
Rais Samia usitulazimishe sisi watanzania kufikiri kijinsia ama kuwapima viongozi wetu kwa misingi ya kijinsia. Ni hatari mnoo.
Kama ilivyo dini na kabila la mtu kuwa sio vigezo vya kugombea au kuchaguliwa kuwa kiongozi hapa Tanzania, jinsia ya mtu nayo sio kigezo cha kuomba kuwa rais wa Tanzania.