Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

Memento

Maza kishajua kuna watu nyuma ya pazia wanataka kumfanyia kauzibe. Sasa ameamua kuanza kampeni mapema kujiimarisha.

Kitendo cha kuwaambia watakuwa wajinga kuachia bahati waliyopewa na Mungu as if wanawake wote wa Tanzania watafaidiaka kwa yeye kuwa Rais ni kutangaza vita na Wanaume wa Tanzania .... sijui nani kamdanganya aongee hayo kwenye public.

Kama anataka kujijengea sifa na credibility ndani na nje ya Tanzania ni bora a stick kwenye principles na kama hotuba zinamshinda basi abakie kwenye script kila anapohutubia. Kwangu naona hili ni kosa la pili. La kwanza lilikuwa la wadada wa soka wa Tanzania.
 
Anatakiwa kufocus Sana na kukuza uchumia na sio kuweka nia ya kugombea.
Mtu aliyelewa madaraka katika style hii atakuwa na focus gani zaidi kutumbua raha na kulinda cheo chake...?

Mtu ambaye her mind has been corrupted and compromised atafikiri saa ngapi kubuni njia za kujenga na kuinua uchumi...?

Ndiyo maana ni vyema kutakasa kiti cha Urais kwanza maana ndicho kinachozalisha uchafu huu...!!
 
Leo rais wa Tanzania ameyakusanya makundi ya wanawake jijini Dar na kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania kwa sasa inajipanga kuwahakikisha 2025 rais wa Tanzania lazima awe mwanamke, tena mwanamke mwenyewe ni yeye kwa sababu wanawake wamechoka kuwabeba wanaume kwa miaka mingi, na urais alionao sasa yeye kama mwanamke ameupata kikatiba kwa kudra za mwenyezi Mungu tu hivyo anajipanga kikamilifu kuhakikisha 2025 anakuwa rais wa kuchaguliwa na wananchi hivyo wanawake wajipange kumuunga mkono ili awabebe!

Hii ni kauli ya kibaguzi, kejeli na dhihaka ya kijinsia katika uwanja wa siasa za kidemokrasia hapa Tanzania, na inapaswa kupingwa kwa 100%.

Kwa kuwa Rais Samia ameitoa hiyo kauli hadharani yeye mwenyewe na sisi watanzania tumjibu hadharani, tunasema hatutaki utawala wa kijinsia wala urais wa kijinsia hapa Tanzania.

Rais Samia usitulazimishe sisi watanzania kufikiri kijinsia ama kuwapima viongozi wetu kwa misingi ya kijinsia. Ni hatari mnoo.

Kama ilivyo dini na kabila la mtu kuwa sio vigezo vya kugombea au kuchaguliwa kuwa kiongozi hapa Tanzania, jinsia ya mtu nayo sio kigezo cha kuomba kuwa rais wa Tanzania.
 
Hata mpige kelele kiasi gani I know hakuna impact yoyote itakayotokea na baada ya uchaguzi watu wataendelea na maisha yao kama leo hii baada ya Hayati kufariki hii ni [emoji1241]Tanzania na Rais atakuwa Mwanamke kama kauli ya Rais leo
 
Ni kauli si nzuri kabisa, yaani kifo cha bosi ni baraka kwake?
Kudra ni mambo anayofanya Muumba ambayo binaadamu hana uwezo wa kuyazuia! Hajakosea! Kifo cha magufuli ni kudra na yeye kuwa rais ni kudra!Hamjui kiswahili au mnapotosha kuchochea fitna!
 
Kutafuta uhalali wa kisiasa kwa kutumia kabila lako ni Ubaguzi, kutafuta uhalali wa kisiasa kwa kutumia dini yako ni ubaguzi. Kutafuta uhalali wa kisiasa kwa kutumia maumbile yako ni ubaguzi. Na dhambi ya ubaguzi dawa yake ni kukemewa kwa nguvu na kulaaniwa.
 
Not only five years to Her Excellence chief Hangaya but also she has to be a life president,with me, I appreciate her!!!!
 
Zanzibar-ASP
Hizo nyombo za kuwakomboa wanawake, kuwawezesha, kuwainua , kuwapa viti maalum, …mbona zipo zamani na zinaimbwa na wanaume pia! Why mnashangaa alipofanya rais na yeye ni mwmke, mwana siasa na ccm, si anatilia nguvu yale yanayopendwa na chama chake! Samia oyee!
 
Back
Top Bottom