Mie nilisema mapema, Mh. Rais wangu SSH achana na wapinzani, piga kazi, hao watukuzodoa, watakudharau, watakutukana, watakuona huna maana hata uwafanyie nini, Mh. Rais akianza kutaka kuwadhirisha wapinzani ni sawa na kujaza maji gunia.
Umeona Lissu alivyogeuka, umeenda kumuona, umempatia passport, umeahidi uso kwa uso kushughulikia maslahi yake aliyokuwa analilia kutwa, bado anasema ww sio alivyokufikuria, kasema vibaya sana juzi kati ulivyokutana na ile tume ya kutoa maoni ya vyama vya siasa.
Lissu au Mbowe hata ufanye nini, ni bure kabisa, huwezi kuwaridhisha. Achana nao. Umeona juzi Mbowe kwenye jukwaa akikunanga.