Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Lengo ni kwenda na dunia ya sasa. Unapokuwa na treni ya viwango vya SGR hauwezi kuwa na uchumi wenye ufanisi kwa aina ya bandari tuliyonayo hivi sasa. Mzigo utakwenda kuielemea na malalamiko yatakuwa mengi na watu watafungua nyuzi nyingi humu jukwaani wakiupigia kelele mkwamo wa bandari.Mechanisms za kuwajibisha wazembe na wapigaji zipo, vinginevyo kwa hoja yako hiyo unataka sasa serikali ibinafsishe taasisi zake zote kwa wageni kwa kuamini kwamba watanzania wote ni wazembe na wezi, siyo?
Lengo kuu ni kusogea uchumi wa juu wa kati mahali tulipokuwa tukielekea kabla ya mlipuko wa covid ulioturudisha nyuma mwaka jana.
Kitaifa tuna lengo la kuufikia uchumi wa kati wa juu, hivyo SGR itakapoanza kazi kutakuwa na ongezeko la mzigo unaoingia na kutoka bandarini kuliko huu wa sasa. Haupo uwezekano wa ufanisi huu wa sasa kwenda sambamba na matakwa mapya ya kiuchumi ya wakati huo.
Wengi wa hawa wanaopiga makelele ni fikra za wanaharakati tu, wanatumiwa bila ya wao kujua kuwa wanafikisha mawazo ya watu fulani ambao wana malengo ya kibinafsi.