Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD

Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD

Kwa mkataba huu wa kuuza bandari za Bara zote, Saa100 soon atarajie NGUVU ya UMMA.
 
Keyboard worrious..hizo nyuzi zinasaidia nini kama hamchukui maamuzi?
 
Washauri wa Saa100 na yeye mwenyewe asome huu mkataba ili wajifunze na kujiuliza kwanini ni bandari za Bara tu .

Na aone wazi kuwa ameuza Tanganyika.

Pia aone kuwa hatoshei nafasi aliyopewa na katiba
Pia mikataba 17 aliyosaini huko Dubai iwekwe wazi isije ikawa Ngorongoro crater na SGR amesainisha tena waarabu mikataba ya aina hiyo
DP keshaini muda mrefu tu mkataba kule Rwanda. JPM aliacha ujenzi wa SGR umekwisha kusogea, muda sio mrefu inakaribia kumalizika.

Hiyo ni chain kubwa ya biashara inayotoka Dubai kwenda DRC na Rwanda na kurudi kupitia bandari ya Dar.

Amesaini na DP akiwa mkuu wa nchi, kwa ajili ya maslahi ya taifa. Zanzibar hakuna SGR na hakuna mazingira yenye kuweza kuifanya bandari yao ikahitaji maboresho, pia kasaini akiwa kama mkuu wa nchi iitwayo Tanzania hakusaini kwa kutazama asili yake akiwa mwenyeji wa Zanzibar.
 
Mechanisms za kuwajibisha wazembe na wapigaji zipo, vinginevyo kwa hoja yako hiyo unataka sasa serikali ibinafsishe taasisi zake zote kwa wageni kwa kuamini kwamba watanzania wote ni wazembe na wezi, siyo?
Hakuna anayetaka kubinafsisha bandari ni mkataba wa kibiashara unaokwenda kuongeza pato kutoka trilioni saba pesa aliyokuwa analipa TICTS kwa mwaka mpaka trilioni 26 na hapo hayo ni makadirio tu kwani inaweza kuzidi kiasi hicho.

JPM alipokuwa anapambana usiku na mchana kujenga reli kwa kiwango cha SGR tulikuwa tunadhani lengo lake lilikuwa ni lipi?.
 
Hakuna anayetaka kubinafsisha bandari ni mkataba wa kibiashara unaokwenda kuongeza pato kutoka trilioni saba pesa aliyokuwa analipa TICTS kwa mwaka mpaka trilioni 26 na hapo hayo ni makadirio tu kwani inaweza kuzidi kiasi hicho.

JPM alipokuwa anapambana usiku na mchana kujenga reli kwa kiwango cha SGR tulikuwa tunadhani lengo lake lilikuwa ni lipi?.
Kwani ukubwa wa mzigo wote wa Rwanda ni kiasi gani kwa mwaka? Sidhani kama Rwanda wanafika 900,000 tonnes per annum
 
Kwanza nikupe pole na majukumu rais wetu.
Baada ya pole nije kwenye point, Kumekuwq na mjadala mkubwa sana kuhusu mkataba wa bandari, kiukweli Watanzania walio wengi hawaelewi kuhusu huo mkataba zaidi ya kusikia tu wanasiasa wakiksema hili na lile.

Nikiri hata mimi binafsi sijui kwa kina kuhusu huo mkataba, zaidi tunasikia tu mara bungeni, mara kwenye vyombo vya habari wakijadili hili na lile.

Mimi siupingi huo mkataba, ila mimi shida yangu ni kwenye kipengele cha muda tu cha huo mkataba, tunaambiwa mkataba utakuwa ni wa miaka 100.

Mimi ninacho shauri, kwanini muda usiwe angalau miaka 10, ili tukiona kuwa haufai kama wanavyosema wengine basi muda huo ukiisha tusitishe au kama utakuwa mzuri kama mnavyosema basi tuongeze, lakini kwa miaka 100 mimi binafsi siafiki kabisa.

Pili napenda kukushauri mheshimiwa rais, hao watu wanaokuzunguka kuwa nao makini sana, wengi wao ni wanafki na wapo kwa ajili ya maslahi yao. Chochote utachosema au kupendekeza wao wanaunga mkono tu ili kukufurahisha.

Nikupe mfano kidogo, kipindi cha nyuma hayati rais Magufuli alipiga marufuku wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo, hao watu wako ndio walikuwa wa kwanza kumsifu Magufuli kila mahali kwamba ametumiwa na Mungu sababu hao wasichana wangeenda kuwaharibu wanafunzi wengine huko mashuleni, haya Mafuli akaenda zake, ukaja wewe Rais ukasema waliopata mimba wakiwa shuleni waruhusiwe, watu hao hao wakageuka na kuanza kukusifu kwamba wewe ni mkarimu, unajali utu na sifa chungu nzima

Si hilo tu, njoo kwenye ishu ya korona, Magufuli alikataza dawa na vifaa kutoka nje akasema tutumie tiba zetu za asili, wote walimsifu na kumtukuza kwa nyimbo na mapambio, badae ukaja wewe ukaruhusu chanjo, wote wakageuka na kuanza kukusifu.

Sasa hivi wote wanaupigia debe huo mkataba, wanaupamba kwa kila aina ya manukato uonekane ni mzuri, wanapishana kwenye vyombo vya habari na makongamano ili uwaone jinsi wanavyopambana. Mheshimiwa hao wote ni wanafiki.

Ebu fanya unajaribu tu useme kwamba umejaribu kuupitia huo mkataba umegundua kuna vipengele havipo sawa uone jinsi watavyopiga roundabout na kuanza kuupinga huo mkataba. Kwa kifupi wote wapo kwa ajili ya maslahi yao na wala si kwa taifa.

Kwa kumalizia nakuomba tu Rais wetu, ebu fanya hili jambo kwa maslahi mapana ya nchi yetu na vizazi vijavyo. Miaka 100 ni mingi sana, yaani toka tupate uhuru mpaka leo hatujaifikia hata hiyo miaka. Naamini utauzungatia ushauri wangu.

Wako, Mwananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom