Rais Samia unao muda wa kujisahihisha; Pokea maoni ya kuboresha mkataba au futa mkataba wa DP WORLD

Wabunge waliopo bungeni ni zao la Mwendazake..tuone sasa umwamba wao wa kumuenzi Mwendazake kwa kukataa kupitisha huu Mkataba.

Mimi binafsi naona mkataba ukiwekwa vizuri hamna shida as long as jamaa wametuhakikishia kwamba wataongeza mapato kwa margin kubwa.

Sisi wabongo maeneo mengi tu tumefeli..kitu kizuri tu kama Mwendokasi tumeshindwa kuufanya mradu u-run smoothly and efficiently.
 
Dah......wakuu....twende mbele turudi nyuma....tumpe muda mama.....bado mapema sana 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
nimesikia mama mmoja mpaka mkorogo akisisitiza kuwa hili walibebe wakaombee kura kwa wananchi wao
 
Kwa nini kuwe na Single Source katika Mkataba huu?. Mhe. Rais achukue ushauri wa Prof. Lipumba.
 
Naunga mkono hoja, isipokuwa ulipomtaja vibaya Hayati JPM ambaye binafsi naamini mpaka kesho kuwa alipendwa na kuaminiwa na Watanzania wengi sana kulinganisha na wachache (japo wenye nguvu) waliomchukia.
 
Unaona umuhimu wa yule ambaye huwa hupendi kusikia jina lake?
 
Acheni kujitia wajuaji wakati kumbe mnazidi kujionesha kuwa wajinga tu!! hivi mkataba wa ushirikiano wa nchi na nchi unakuwaga na kipengele cha muda?

Nani kakwambia hakukuwa na uwazi? Kama hufuatilii mambo ni wewe na ujinga wako tu!! Hizo kampuni zingine zilizoomba ziliombaje kama hakukuwa na uwazi?

Bunge limefast track vipi? uliwahi kuona mkataba wa bwawa la Nyerere? Uliuliza? mbona husein unitised? uliwahi kuona mkataba wa sgr Dar - Moro? Uliuliza? Mbona husemi unitishwe?

Acheni ujuaji na siasa zenu kwenye masuala ya msingi ya maendeleo ya nchi wapuuzi nyie
 
Chadema pembeni CCM itawale maisha yote. CCM ndio Hifadhi yenu na heshima yenu. Dalili hazioneshi kuwa man uwezo wa wa kuifanyia Tanzania kuwa salama nje ya mikono ya CCM. Chadema hamjaonesha uwezo wa kuwashawishi watanzania kuwa nyinyi ni mikono salama kwa watanzania.
 
Too late samaki ameshameza chambo.
 
Mimi sioni how anaweza kubaki 2025, yaani how, atatuambia nini waTanganyika? Labda kama atatumia jeshi, ila kwa civilised method sioni itawezekana vipi!

Ni ngumu kubebeka hata kwa mbeleko ya greda, its impossible, yaani haiwezekani, halafu binadamu inakuwaje unakosa aibu kabisa usoni? Kwamba unafanya jambo la aibu mno halafu unaongea uso unakuwa mkavu kabisa, totally dry, hiki nacho ni kipaji.

Au hajui kinachoendelea? Au kaambiwa ni chumba cha ku-scan makontena ndio kimeuzwa?Anategemea nini?
 
Anategemea kikwete ,Makamba ,nape na mwigulu ndo wampiganie
 
Dah......wakuu....twende mbele turudi nyuma....tumpe muda mama.....bado mapema sana 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Kumpa muda ndiyo kuingia mkenge mazima. Hii kitu ISITISHWE mara moja hata ikibidi kwa NJIA YA MAHAKAMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…