Kwanza nikupe pole na majukumu rais wetu.
Baada ya pole nije kwenye point, Kumekuwq na mjadala mkubwa sana kuhusu mkataba wa bandari, kiukweli Watanzania walio wengi hawaelewi kuhusu huo mkataba zaidi ya kusikia tu wanasiasa wakiksema hili na lile.
Nikiri hata mimi binafsi sijui kwa kina kuhusu huo mkataba, zaidi tunasikia tu mara bungeni, mara kwenye vyombo vya habari wakijadili hili na lile.
Mimi siupingi huo mkataba, ila mimi shida yangu ni kwenye kipengele cha muda tu cha huo mkataba, tunaambiwa mkataba utakuwa ni wa miaka 100.
Mimi ninacho shauri, kwanini muda usiwe angalau miaka 10, ili tukiona kuwa haufai kama wanavyosema wengine basi muda huo ukiisha tusitishe au kama utakuwa mzuri kama mnavyosema basi tuongeze, lakini kwa miaka 100 mimi binafsi siafiki kabisa.
Pili napenda kukushauri mheshimiwa rais, hao watu wanaokuzunguka kuwa nao makini sana, wengi wao ni wanafki na wapo kwa ajili ya maslahi yao. Chochote utachosema au kupendekeza wao wanaunga mkono tu ili kukufurahisha.
Nikupe mfano kidogo, kipindi cha nyuma hayati rais Magufuli alipiga marufuku wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo, hao watu wako ndio walikuwa wa kwanza kumsifu Magufuli kila mahali kwamba ametumiwa na Mungu sababu hao wasichana wangeenda kuwaharibu wanafunzi wengine huko mashuleni, haya Mafuli akaenda zake, ukaja wewe Rais ukasema waliopata mimba wakiwa shuleni waruhusiwe, watu hao hao wakageuka na kuanza kukusifu kwamba wewe ni mkarimu, unajali utu na sifa chungu nzima
Si hilo tu, njoo kwenye ishu ya korona, Magufuli alikataza dawa na vifaa kutoka nje akasema tutumie tiba zetu za asili, wote walimsifu na kumtukuza kwa nyimbo na mapambio, badae ukaja wewe ukaruhusu chanjo, wote wakageuka na kuanza kukusifu.
Sasa hivi wote wanaupigia debe huo mkataba, wanaupamba kwa kila aina ya manukato uonekane ni mzuri, wanapishana kwenye vyombo vya habari na makongamano ili uwaone jinsi wanavyopambana. Mheshimiwa hao wote ni wanafiki.
Ebu fanya unajaribu tu useme kwamba umejaribu kuupitia huo mkataba umegundua kuna vipengele havipo sawa uone jinsi watavyopiga roundabout na kuanza kuupinga huo mkataba. Kwa kifupi wote wapo kwa ajili ya maslahi yao na wala si kwa taifa.
Kwa kumalizia nakuomba tu Rais wetu, ebu fanya hili jambo kwa maslahi mapana ya nchi yetu na vizazi vijavyo. Miaka 100 ni mingi sana, yaani toka tupate uhuru mpaka leo hatujaifikia hata hiyo miaka. Naamini utauzungatia ushauri wangu.
Wako, Mwananchi wa kawaida.