The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Mwendazake Rais John P. Magufuli alikuwa na sifa moja nzuri kwa kiongozi yeyote.
Kusimamia utekelezaji wa kile alichoamini na kukiamua bila kujali matokeo yake yaani yawe wazuri au mabaya, hasi au chanya.
Alikuwa ni aina ya viongozi "risk takers". Hakuogopa matokeo ya kushindwa. Nadhani ndiyo maana tulimchukia kwa sababu licha ya sifa zingine mbovu, chafu na hovyo alizokuwa nazo kama kiongozi mkuu wa nchi, alikuwa ni " risk taker" kupitia maisha ya watu [something which was very bad] na kuwaathiri wengi negatively.
Sasa tunaye huyu mama mwenye jina la Samia Suluhu Hassan ambaye mimi namwona kama "Ceremonial President tu asiyeweza kusimamia kwa vitendo anachokitaka kiwe ili kilete matokeo anayoyataka.
Sina hakika kama ni hofu na woga unaochangiwa na jinsia yake ya kike au kutojiamini au kuhujumiwa na wasaidizi wake wa kisekta.
Tunafahamu kuwa, kwenye uongozi wa kisiasa hususani ktk siasa za kiafrika (Tanzania ikiwemo), maneno na ahadi zenye kutumainisha waongozwa huwa ni nyingi lakini kuweka ktk utekelezaji maneno hayo ya ahadi huwa kwa 80% ni BIG ZERO.
Hata hivyo, in this short period of time of her presidency, Mama Samia Hassan seems to have failed spectacularly.
Hivi ndivyo mtu anaweza kumwelezea Rais wa JMT, Mama Samia Suluhu Hassan.
Zifuatazo ni baadhi ya ahadi za kiutendaji za serikali ambazo zilishatolewa na Rais Samia S. Hassan ndani ya karibu miezi minne ya U - Rais wake lakini hakuna utekelezaji;
1. Katika sherehe za wafanyakazi [maarufu kama MEI MOSI] Mwanza mwaka huu aliahidi kwa kinywa chake mchana kweupe mambo mawili kwa wafanyakazi wote. Moja kupunguza PAYE kwa 1% kuanzia mwaka mpya wa fedha Julai 2021/2022 na kupandisha kima cha chini cha mishahara mwaka wa fedha ujao Julai 2022/2023.
MATOKEO YAKE:
å 1% ya PAYE haijaondolewa [ni ZERO ACTION] unless wafanyakazi wa mshahara wawe hawaja realize hili kupitia mishahara yao ya mwezi July.
å Kupandishwa mishahara, bado inasubiriwa maana ni mwakani kama alivyoomba/ahidi. Kwa hili, tunampa the benefit of the doubt and see if she meant what she promised.
2. TOZO za miamala ya simu. Mara baada ya malalamiko ya wananchi kukolea, mara moja kwa maneno yake laini alijitokeza na kutaka hilo liwe suspended ili liangaliwe upya.
MATOKEO YAKE:
å Bado ni zero. Cha kushangaza zaidi leo akiwaapisha wale mabalozi 13, kasema tozo zipo ila marekebisho "fulani" yanaweza kufanyika. Hii siyo kauli ya Rais mwenye mamlaka. Hii ni kauli ya kiongozi asiyejiamini. Kwa wanaoweza kutambua lugha, hiyo maana yake TOZO ZITAENDELEA. Kama kuna abishae, asubiri.
3. Kuhusu "national political reconciliation", aliahidi kukutana na wanasiasa wenzake walio nje ya serikali maarufu kama "vyama shindani dhidi ya chama kinachoongoza serikali" ili kujadili namna wanavyoweza kufanya shughuli zao za kisiasa bila mikwaruzano...
MATOKEO YAKE:
å Big ZERO. Badala yake huyu amegeuza yaliyokuwa yawe maridhiano ya kisiasa kati ya chama cha siasa kinachoongoza serikali [CCM] na vyama shindani dhidi yake kuwa vita huku chama tawala kikitumia vizuri udhaifu wa mfumo wa kikatiba na kisheria kunyanyasa na kuonea wapinzani wake. This is too bad.
SWALI NI:
Atafika wapi huyu mama na wenzake kwa uongo na ulaghai wao wa kisiasa?
Ni hayo tu kwa uchache kwa leo