Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Tuongeze vyanzo vya mapato hapo ndipo tutaweza kusema wazee na watoto wote matibabu bure.....umasikini mkubwa sana vijijini huko hata buku kwa siku mtu hapati...ni shida sasa Rais atafanyeje ? Kwa sasa hana ubavu wowote hata aje nani ....labda siku tukipata pesa za mafuta uganda zitasaidia sana mno boast revenue ....kupunguza makali umasikini ....masna watalipa pesa kubwa sana mwaka 75% bajeti yetu sasa....hapo tutajidai kidogo kupambana umasikini lakini sio kwa bajeti hii 65% tunasaidiwa donors.....
 
MKUU PESA ZIPO TENA NYINGI SANA.
Tazama huko bungeni na BOT wanavyokula helza zetu kwa kulipana mabilioni....
 
Lakini si JPM alitupeleka uchumi wa kati?,huyu SAMIA anatupeleka wapi wakuu?
 
Huyu mama amechemka mapema sn hii kazi ni ngumu haiwezi
Hii kazi ilikua ya JPM,kuteka teka watu,kuongopa data,kuvunja katiba,kutoajili raia........kuua upinzani.......JK na Samia hii nchi wameonesha kufeli......viva JPM
 
Nzuri ni ile ya kuchota mahela ikulu halafu kila anayelalamika njiani unamgawia burungutu.....viva JPM[emoji16][emoji122]
 
Samia ndio kaleta hii mikopo,JPM alikua anatumia vyanzo vya ndani .
Note:Nyerere hadi kikwete Deni la taifa trillioni 40,JPM Deni la taifa trillioni 37[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Afya ni eneo nyeti Sana Watanzania wengi wanapoteza maisha na kudhalilika Sana hospitali hata za umma kwa kukosa pesa.
JPM si akiingia hii nchi uchumi wa kati?......imekuaje tena wakuu?,huyu Samia anatupeleka wapi?[emoji16]
 
Tumpe muda gani zaidi? Tangu March Hadi Sasa hajamaliza kuteua . Bado madc,maded wa halmashauri,,makatibu tawala. Speed yake ni ndogo sana sana. Songwe na kigoma atafika lini?
Huko JPM alishaipeleka.nchi uchumi wa kati.......nchi hii ni tajiri sana,sisi ni Tanzania mpya A+,[emoji16][emoji16]
 
Rais anayejenga uwanja wa ndege kijijini kwao,ilhali akiacha sehemu zenye potential yakitalii na kibiashara bila hio huduma,atakukwamua wewe kiuchumi.......umerogwa wewe[emoji16][emoji3]
 
Wananchi si mafukara,sisi ni matajiri,sisi tupo uchumi wa kati,sisi hatukopi.....JPM aliingiza hii nchi kwenye uchumi wa kati
 
Reactions: BAK
JPM aliiweza hii nchi.......Nyerere hadi Kikwete walikopa trillioni 40,JPM pekee yake alikopa Trillioni 27........JK alitoa ajira kwa kada ya elimu na afya kila wanaomaliza shule......JPM hata waliokuepo aliwafukiza........JK alijenga miundombinu bila upendeleo.......JPM alijenga kijijini kwake chato tu......
Ni kweli....JPM aliiweza hii nchi hadi kufika uchumi wa kati[emoji3][emoji16][emoji122][emoji122]
 
Muda ndio utaweza kumfananisha JPM na Samia......kama tu ulivoweza kumtofautisha kati ya JK na JPM......................msomi yeyote hupima Takwimu katika muda kama factor muhimu[emoji120][emoji3578][emoji419]
 
We must highlight all issues we need our President to put them right. This must not be restricted to her, we shall extend it to the next Presidents . Never should we be hindered by many good for nothing imbeciles.
 

Hebu twende taratibu kisha ujipime. 2014 kabla ya Magufuli kuwa rais tulikuwa tunaimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas, wakati huo Magufuli alikuwa waziri na yeye alibariki suala la umeme wa gas. Tukakopa $1.3b sawa na 3t kujenga bomba la gas toka Mtwara, tuliambiwa kwenye umeme wa Gas tutazalisha 5,000m, na kweli bomba liko hapa Dar na uzalishaji umeanza kiwango 450mg kama sikosei, ukichanganya na umeme wa vyanzo vingine tuna umeme 1,500m+. Inakuwaje Magufuli awe rais aanze mradi mpya wa maji wa 6.5t utakaozalisha 2,115m aache wa gas utakaozalisha 5,000? Tena anatumia maji, ambapo akiwa waziri alikuwa ni mmoja ya waliotumanisha tatizo la umeme wa maji ni mabadiliko ya tabia nchi? Je angeweka 2.5t asingeweza kuzalisha 2,115m hapo kwenye gas ambapo tayari bomba liko hapa Dar, na fedha zinazobaki zikiingia kwingine? Hilo ni moja.

Tuje kwenye hilo la ndege, sina popote ninapobeza kuwa na ndege, ila ndege zilipaswa kuwa kipaombele cha mwisho dhidi ya vipaombele vingine. Ama ni bora angenunua ndege nyingi ndogo za ndani kuwezesha safari za ndani, kuliko hizo za masafa marefu wakati ushindani wa biashara hiyo kimataifa kwetu ni mdogo. Kuliko kuwekeza 1.8t kwenye ndege alizonunua, angeweza kujenga viwanda vya kimkakati kwenye maeneo yalimayo pamba, korosho, kahawa, tumbaku nk vya wangalua 50b@, kisha atoe ajira. Ama basi angejeja shule za VETA kila mkoa ymza 10b@ vijana wapate ujuzi. Kama una akili nzuri ulipaswa kujiuliza mambo hayo, na sio kusubiri kulishwa propaganda na kuanza kusifia kama kipofu.
 
Hahahahahahaha eti dhalimu alifanya vitu vikubwa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 vitu vikubwa vipi hivyo? Bomoa bomoa? Kuteka na kubambikia kesi? Kununua ndege zilizoingiza hasara ya karibu bilioni 400? Kudharau katiba, mahakama na Bunge? Kufanya mauaji dhidi ya raia wasio na hatia? Kujichotea trillions hazina kinyemela? Hebu acha kuandika UPUUZI!!!!
Na wewe leo unaunga mkono aanze kufanya vitu vikubwa vikubwa?!!!, unweza kuvitaja, maana mwendazake alifanya hivyo vikubwa , lakini kila siku unamtukana.

hebu tutajie hivyo vitu vikubwa zaidi ya alivyofanya mwendazake.
 
Naomba kueleweshwa kidogo kuhusu ukubwa wa deni la taifa.
Hili deni huwa linathaminishwa kwa Tsh au USD?
Hoja yangu iko hapa; mwaka 2015 wakati JPM anaingia madarakani thamani ya tsh ilikuwa 1800+ kwa dola moja ya marekani na kufikia 2021 thamani imepanda hadi 2300+. Je,kama 2015 mlidaiwa tsh 38T za kitanzani,thamani yake itaendelea kuwa hiyo hiyo au itabadilika kulingana na kupanda ama kushuka kwa dola ya marekani?
Samahani kama niko nje kidogo ya mada ila kuna utata kuhusu nani amelikuza hili deni parefu kati ya marais 3 waliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…