Nakumbuka sana kipindi cha Magufuli wapinzani walipokuwa wanapambana Watanzania wapate katiba mpya mlivyokuwa mnawabeza!!
Nafikiri hamkuelewa kwenye maisha kuna nyakati njema na kuna nyakati ngumu!! Na katiba ingekuwa ni kiungo kizuri sana cha kupata viongozi bora bila kuburuzwa!! Na namna ambayo watanzania wangeweza kutetea haki yao kirahisi.
Shida ni kwamba wakati matumbo yanashiba leo mnasahau kesho njaa inaweza kutokea na namna ya kutatua lazima misingi iwekwe leo!!
Ndo hivyo sasa Samia ndo Rais wako mpaka 2030!! Habari ndo hiyo!!
Endeleeni kubeza kila kinacholetwa na upinzani badala ya kutanguliza Taifa mbele!! Na hilo kundi lillilomzunguka hamna cha kuwafanya na hata 2030 tayari walishakuandalia Rais wa kukuongoza hadi akili ziwakae sawa!!