Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Na kesi ya Mbowe ndio inazidi kumtenga na huruma ya Wananchi, asipojitafakari upya atashangaa wenzake wanasimama pembeni kumsimanga.
Tena Ccm vigeugeu kma kinyonga utasikia si tulimshauri hakusikia
 
Waache kumnanga marehemu. Huyu ndo alikuwa shujaa wetu
Mama kadanganywa na kikwete alidhani uraisi ni kazi rahisi akaanza kumtukana MAGUFULI THE GREAT sasa lazima atapata tabu sana atakapokuwa anashindwa jambo lolote kulifanya vizuri maana aliingia madarakani kwa kujipigapiga kifua dhidi ya jpm akitaka kutuaminisha kuwa yeye ana akili kuliko jpm
 
Ningelipata nafasi ya kumshauri Mama neno moja tu, ningemshauri ahamishie alichokifanya Karume Jr, afanye kampeni ya muafaka wa kitaifa, serikali ya umoja wa kitaifa, katiba ibadilishwe kuwapatia room wapinzani.

In that case, CCM itajihakikishia kubaki na wapinzani watajihakikishia nafasi ya ushiriki kwenye serikali.

Kuongoza watanganyika ni rahisi sana, coz wengi wao wanalilia maslahi tu! Agawe keki ya taifa kwa wote.
Ni ngumu sana kumshahuri mtu mwenye sifa ya UZUZU nikama kujaribu kumshauri speaker wa bunge utapata tabu sana tena sana
 
kwanza tuambiwe na mifumo rasmi ya uchunguzi Dr. Magufuli alikufa je? kila nafsi itaonja mauti ila tunataka tu kujua ilikuwa je mpaka mzee wa watu akafikwa na umauti?
Eti Rais wa inchi kubwa kam hiii anakufa hata hakuna uchunguzi wa kifo chake si hatari hiii
 
Hahahaha mkuu nakuona ukiamini sukuma gang Wana nguvu sana hahahaha hivi ni vichekesho kama vile vya Voda/tigo tu .

Hawana lolote na hawajawahi kuwa na lolote Hawa wa kupiga chini

Stori za wabunge ni zao la magu na Bado wanaamini kwenye upuuzi wa magu ni stori za kitoto tu sijui watapitisha azimio hawana imani na raisi (wakati wanapitisha ye amekaa tu akiwasubiri wajikusanye kusanye ) anawaachaje kulifuta bunge

Mkuu kifupi we ni mnufaika wa sukuma gang na unawapigia promo kijanja hawa wapuuzi wataondoka mmoja baada ya mwingine na hawatakuwa na Iyo nguvu uisemayo (wakitoka tu nje ya mfumo kwisha habari yao)
Ukitaka kuamini JPM Ana nguvu, huyo mama yako aruhusu kura za maoni kwa nafasi ya Urais mwaka 2025
Itambeba CCM ambayo hata akigombea paka anapita
 
Leo kwa mara ya kwanza Rais Samia amekuja hadharani na kukiri wazi kuwa anaongoza serikali iliyogawanyika vibaya, amezungukwa na wasaidizi wanao mhujumu wazi wazi na yuko kwenye vita kali ya kuupambania urais wake kwa hali na mali. Hali ni tete mnoo kwake, na hatakubali!

Bila kumumunya maneno, wacha tuuseme ukweli ili kumsaidia Rais Samia popote alipo na ikibidi utafute njia ya kutokea.

Kwanza niweke wazi jambo moja kubwa na muhimu, kwa sasa Rais Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa, yaani umechokwa. Hili halina ubishi na halihitaji takafari yote yote kubwa.

Kitendo cha mama Samia kuja hadharani na kukiri kuwa 'wenzake wanamzunguka' hivyo hatakubali! Hapo tunaona picha kubwa moja tu, maji yamezidi unga na mama Samia anahitaji msaada ili avuke.

Sasa kuna jambo moja kubwa pekee linaloweza kumuokoa mama Samia mahali alipo, hana ujanja inabidi alikimbilie. Kwa ufupi, jambo hilo ni;

Kutafuta muafaka wa kitaifa ili kuweza kuiunganisha nchi iliyoparaganyika vibaya kisiasa. Kama Samia hataweza kukaa na kumaliza tofauti zake na kundi kubwa la wafuasi wa Magufuli (sukuma gang) au wapinzani (hususani Chadema) basi ajue hawezi kutoboa. Hayo ndio makundi yenye nguvu kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, na kwa sasa yote mawili kwa pamoja (pasipo kuongozwa na mtu yoyote) yanasema wazi wazi kuwa mama Samia hafai, hatoshei kwenye kiti cha urais na hayamtaki tena. Huo ni uasi wa kisiasa.

Wakati ukuta, na majuto ni mjukuu, wenye hekima wameshaelewa!
Kwa mazingira anayoyapitia Mama SSH kwa hivi sasa, na ili aweze kuweka mambo sawa, ni vyema akauvunja mwiko kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Na pia aufufue upya ule mchakato wa katiba mpya.

Sitaki kuonekana kama mbaguzi wa kijinsia, lakini ni ukweli usiopingika kwamba mama zetu hawa wanapokuwa katika mtanziko mkubwa na kukabiliana na changamoto kubwa huwa wanafanya maamuzi mengine kwa hasira ambayo huja kuyajutia baadaye. Kwa hiyo ni vyema kwa sasa Rais wetu awe karibu sana na washauri wake na apewe ushauri mzuri pia.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mnapokosea ni ile kusema ati asifanye kazi na watu wa Maguguli.I can tell you hapo mnakosea sana na mnataka kumwangusha.Wabunge wote waliyopo ni wa Magufuli.sasa unaposema ati asifanye kazi na watu wamagufuli what do you mean ?Hivi wakitaka kumwangusha si ni kupitisha azimio kule bugeni kuwa hawana Imani na Rais? What is so wrong akifanya kazi na watu wa Magufuli? Guys acheni kumpotosha rais wetu.Na akifanya vita na watu wa Magufuli vita hii itamshinda vibaya sana.Yawezekana kuna mahara JPM alikosea lakini makosa yake ni 5% ya mabaya yake compared to 95 % ya mazuri aliyoifanyia nchi hii.She better be careful na watu wa Magufuli. Mnapokosea etu watu wa Magufuli ni wasukuma.you are 100% wrong.

Hata wabunge wanaojifanya kuwa wanamchukia JPM wakati yeye ndiye aliyewapitisha na kuwanadi kwa waanchi,nao mwisho wao 2025.Nawashauri wafanye kazi kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 ,mambo mengini hayana faida kwa taifa letu.
Mama ukifanya vita na watu wa Magufuli iko siku watakurushia bomu la shutuma hutapona walahi.
Kusema asifanye kazi na watu wa Magufuli ni kama kuji shoot kwenye mkono wa kushoto kuliko na moyo kwakua Hayati JPM alitumia mfumo mzima wa nchi kwenye utawala wake sasa ukitaka hayo ya tokee basi futa kila aliyewahi kuwa kwenye public service uanze upya....Hata JPM alitaka kujaribu ikamshinda...

Tatizo la Tanzania ni corrupt beings ambao wamekwepo tangu enzi za Mwl Nyerere waki perpetuate hiyo tabia yao mbaya....Hao wote ambao ma faili yao yapo waondolewe tubakie na wachache hao hao wenye institutional memories ya nchi hii walivushe taifa kwakuunda serikali ya umoja wa kitaifa bila kujali vyama, ukanda, gender au age....Maana hata miongoni mw avijana bado wapo ambao wamekuwa consistent na composed hata katika hii turbulence....


Naamini kabisa Tanzania will find its way through kwakua watanzania wametoa sadaka nyingi sana huku duniani ikiwamo kuwapigania wa africa wenzao ambao wengine leo chumi zao zinatawala Africa....Over to you my God who never disappoints nor fails, forever you remain the same, AMEN
 
Na kesi ya Mbowe ndio inazidi kumtenga na huruma ya Wananchi, asipojitafakari upya atashangaa wenzake wanasimama pembeni kumsimanga.
Hiyo kesi mama anashindwa kuifuta maana kawaaminisha mabwanazake mabeberu kuwa mbowe ni gaidi hivyo akifuta mabeberu wataanza kumuandama kuwa alikuwa anagandamiza democracy na vyama vya upinzani vitaanza tena kusikilizwa na mabeberu
 
Mi sioni kigumu hapo,ushauri wangu ni kuwa tu achangamshe yale waliyoyaanzisha awamu ya 5 kwani inaonekana kama kuna kupungua kwa speed kidogo,otherwise she is still on right track,lastly asiwe mvivu kumfyatua mtu ambaye anahisi kutokwenda na speed yake hii itamsaidia sana,itajenga discipline...
Hayo unayo sema ni magumu sana kwa mama
 
Mama sijui anamlalamikia nani ikiwa aliyetoka ni ccm, na nyuma nyuma yake walikuwapo ccm.

Atulie tuu miaka yake iishe waje wengine wale keki ya taifa. Maana kila akizichanga karata zake anaona kabisa ushawishi wake ni mdogo kuelekea 2025.

Kama yeye anajiamini atembed bila biti ya ccm aone kama kutoboa kupo.
Kajishusha mwenyewe thamani kama issues za kovidi,kushobokea chanjo eti tu kisa ana chuki na marehemu magufuli kulimpotezea thamani kwa 80%
 
Siku za mwisho za ccm zilianza na Magufuli
Hapo umebugi magufuli alikuwa ni nyota ya mapambazuko ya alfajiri kwa bara la africa usimfananishe na wapumbavu. Tz maraisi ni wawili tu NYERERE NA MAGUFULI BASI
 
Ningelipata nafasi ya kumshauri Mama neno moja tu, ningemshauri ahamishie alichokifanya Karume Jr, afanye kampeni ya muafaka wa kitaifa, serikali ya umoja wa kitaifa, katiba ibadilishwe kuwapatia room wapinzani.

In that case, CCM itajihakikishia kubaki na wapinzani watajihakikishia nafasi ya ushiriki kwenye serikali.

Kuongoza watanganyika ni rahisi sana, coz wengi wao wanalilia maslahi tu! Agawe keki ya taifa kwa wote.
Atawagawiaje ulaji serikalini watanganyika wote? Au unafikiri akiwapa baadhi ya viongozi vinara wa upinzani nyadhfa serikalini (serikali ya umoja wa kitaifa) basi upinzani kwake utakuwa umeisha?

Watanganyika sio wajinga kiasi hicho. Na Tanganyika si sawa na zenj.
 
Hapo umebugi magufuli alikuwa ni nyota ya mapambazuko ya alfajiri kwa bara la africa usimfananishe na wapumbavu tz maraisi ni wawili tu NYERERE NA MAGUFULI BASI
Nyie ndio wale Polepole anawaita wahuni
 
Ni ukosefu wa busara mtu kujinasibu kupambania cheo chako. Cheo hakipambaniwi. Ukiwa na fikra za kupambania cheo, KATU huwezi kuwa Mtendaji mzuri abadani. Maana focus yako itakuwa ni cheo na si mahitaji halisi ya watu wako.

Ndo maana kila hitaji muhimu la binadamu limepanda,utafikiri hakuna Kiongozi katika nchi. Imekuwa kama nchi ya Kusadikika chini ya Mfalme Juha. Kumbe watu wako bize kupambania vyeo badala ya kuwatumikia wananchi.

Usifanye hivyo mama, wewe wafikirie wananchi, afu wao watakilinda cheo chako kwa mema utakayowafanyia, na siyo kujifikiria wewe kwanza. Cheo ni mapito tu Mama, kisikuwazishe sana!
Kiongozi na wenzake wako bize kuhusu 2025 na ndio kwanza 2021 hii.
 
Hahahaha mkuu nakuona ukiamini sukuma gang Wana nguvu sana hahahaha hivi ni vichekesho kama vile vya Voda/tigo tu .

Hawana lolote na hawajawahi kuwa na lolote Hawa wa kupiga chini

Stori za wabunge ni zao la magu na Bado wanaamini kwenye upuuzi wa magu ni stori za kitoto tu sijui watapitisha azimio hawana imani na raisi (wakati wanapitisha ye amekaa tu akiwasubiri wajikusanye kusanye ) anawaachaje kulifuta bunge

Mkuu kifupi we ni mnufaika wa sukuma gang na unawapigia promo kijanja hawa wapuuzi wataondoka mmoja baada ya mwingine na hawatakuwa na Iyo nguvu uisemayo (wakitoka tu nje ya mfumo kwisha habari yao)
Ukipambana na Sukuma Gang hakuna siku utashinda.
 
Kwa vile tu ni Mzanzibari ndio mnazuka kwa umoja wenu,WaZanzibari lazima popote walipo waamke huu ulimbukeni wa hawa jamaa wanaodai ni ndugu,hawa hawana kheri hata moja hata uwatendee kitu gani,Raisi Samia ajitahidi aipapatuwe Zanzibar kisha awaachie zigo lao walane nyama.
 
Back
Top Bottom