thuwainize
Senior Member
- Jan 29, 2022
- 178
- 382
Kuna hali mbaya mno kiuchumi ipo mlangoni ndani ya kipindi cha miaka mitatu hali itakuwa mbaya sana na hii ni ulimwengu mzima. Athari za korona na hii vita zimeharibu sana uchumi wa dunia na unaedelea kuharibika. Kampuni kubwa ya uzalishaji wa mbolea YARA washasema gharama za uzalishanj wa mbolea zimepanda maradufu, uzalishaji wa ngano umeathirika tayari, mafuta na gesi ndiyo bei zinazidi kupanda. Sasa wenye nguvu kiuchumi wana ahueni wana uwezo wa kutoa ruzuku kwenye hizo bidhaa ili wananchi wao wanunue kwa bei ambayo siyo kali sana, na wana uwezo wa kununua kwa bei kubwa iliyopo sokoni maana wana misuli ya kiuchumi sasa shida ni hizi nchi zisizo na akiba na wala hazina nguvu za kiuchumi kwa kuwa mafuta na gesi ishakuwa bidhaa adimu na zinazidi kuwa gharama ina maana haziwezi tena nunua kwa kiwango kikubwa hata wafanyabiashara waliopo wanaoleta mafuta wanapoenda sokoni na wao wanakutana na ushindani na bei ikiwa kubwa maana yanahitajika kwa wingi kuliko stock iliyopo. demand kubwa supply kidogo.Bei ya mafuta inatengenezwa kwenye soko la dunia, Rais hawezi kufanya lolote labda kama unataka awadanganye kama watoto wadogo ili muweze kupata usingizi usiku. Na bei ya mafuta ikipanda, bei za kusafirisha bidhaa na vyakula zitapanda na kila mtu zitamgusa. Maana meli, ndege, malori, magari, mabasi yote yanatumia mafuta kufanya kazi.
So bi Tozo hapo kaongea ukweli, na ni mtihani mkubwa kwa washauri wake je watashauri nini kifanyike ili angalau makali ya maisha japo yameshaanza but yasilete athari kubwa kupindukia.
Kipindi kama hiki dunia nzima ndipo washauri wa serikali na viongozi wakuu huwa na wakati mgumu sana maana inabidi watoe suluhu ya changamoto zilizopo na hapa ndipo washauri wengi wanapoonekana wa maana au si wa maana kipimo chao ni sasa.