Rais Samia: Vita ya Urusi, Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei

Rais Samia: Vita ya Urusi, Tanzania hatutanusurika, bidhaa zote zitapanda bei

Na Russia amesema anakata gesi kabisa.

Binafsi naona hizo mnazoita solution ni provisional tu, bora huyu ansyetuandaa kisaikolojia!
Kabla urusi hajasema ujerumani walishafunga bomba la gesi kubwa kutoka Russia linaloenda Europe kupitia kwao .Waziri wa mambo ya nje wa ujerumani akasema wataagiza gesi nje ya Urusi na ongezeko la bei itayotokana na hatua hiyo wamekubaliana na wengine kuwa Serikali zita subsidize

Tayari nchi za Ulaya wameanza ujenzi mbio wa LNG plants za kuhifadhi gesi toka nje ya nchi ya urusi
 
Ila huyu maza jamani hana washauri walau wawe wanamchagulia ni kipi cha kuongea.

Mtu mnaetegemea awape faraja ndo anawadidimiza zaidi na zaid na kujificha kwenye visingizio vya ajabu ajabu.

Na huyo ndio mkuu wa nchi huyo!! Ajabu sana sana. Kulikua na haja gani ya kuruhusu bei kupanda kiholela, hapo kama hajui ni karuhusu wafanyabiara kupandisha bei kiholela.

Kwa kukwepa lawama anajifanya kujitetea kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Mama hapa umepotoka aisee.. tena vibaya sanaa
 
Sio kweli USA wametoa mamilioni ya mapipa ya mafuta kutoka oil reserves zilizoko Texas kuziingiza sokoni kupunguza makali ya bei

Ulaya wanasema watatoa ruzuku kwenye gesi kupunguza makali ya bei kwa watumiaji wa gesi
Sawa lakini bado bei ya gallon moja imefika $ 4 wakati kabla ya vita ilikua $3.32.
Na sehemu nyingine kama Uko California imepanda mpaka $6
 
..Tz hatujachagua upande ktk vita hii.

..kwa hiyo tunatakiwa kuwa watu wa mwisho kulalamika.

..viongozi wanajua hawana uwezo wa kutatua shida za wananchi ndio maana wanakuwa wepesi kutoa visingizio.
Ulichoelezwa ndio ukweli wenyewe!
 
You must be ignorant on economic issues you better shut your mouth. Hii sio siasa hapa ni hali ya kiuchumi inayosababishwa na vita, wewe hata hutazami TV au Redio (CNN, BBC nk.) unashangaza sana. Rais kasema uongo wapi huna maana kabisa.
Hauna uelewa wowote naww mkuu. Sasa kama unajua bei ya mafuta itapanda inatakiwa ufanyaje ili isipande??? Kama kweli wewe ni mwanauchumi jibu hili swali.
 
Rais anadhihirisha jinsi ambavyo hana msaada wowote au hata ubunifu wa kukabiliana na hali hiyo ila anachoweza kufanya ni kutoa vitisho tu.

Very hopeless and poor excuse for a leader.
 
Bi mkubwa Tangu utuambie mbowe ni gaidi na ushaidi unao ,juzi mmekutana na huyo gaidi ikulu mkakumbatiana ama kweli Mimi kukuamini itakua ngumu bi mkubwa
 
Taifa ambalo linakubali kuwepo bila Rais kama Tanzania lina laana.

Imagine nchi ina Rais hewa ambae muda wote yupo busy kutafuta chaka la kuficha uzembe,mauchafu pamoja na madhaifu ya Serikali yake.Hangaya is the inept hopeless leader.
Hakuna binadamu asiye na mapungufu.
 
JPM atakumbukwa milele,Nchi hii bila kupatikana Rais mzalendo wa kweli hamna kitu kitaenda kila mtu atapambana na hali yake mpk mvi zituote.

2025 mama tenaaaaaaa😆
 
Ila huyu maza jamani hana washauri walau wawe wanamchagulia ni kipi cha kuongea.

Mtu mnaetegemea awape faraja ndo anawadidimiza zaidi na zaid na kujificha kwenye visingizio vya ajabu ajabu.

Na huyo ndio mkuu wa nchi huyo!! Ajabu sana sana. Kulikua na haja gani ya kuruhusu bei kupanda kiholela, hapo kama hajui ni karuhusu wafanyabiara kupandisha bei kiholela.

Kwa kukwepa lawama anajifanya kujitetea kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Bei ya mafuta inatengenezwa kwenye soko la dunia, Rais hawezi kufanya lolote labda kama unataka awadanganye kama watoto wadogo ili muweze kupata usingizi usiku. Na bei ya mafuta ikipanda, bei za kusafirisha bidhaa na vyakula zitapanda na kila mtu zitamgusa. Maana meli, ndege, malori, magari, mabasi yote yanatumia mafuta kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom