Rais Samia Vunja Baraza la Mawaziri Nchi ipone. Waziri Majaliwa Habebeki

umeharibu uzi wako ku quote hizo takataka...
 
Hamuoni aibu?
Kila mwenye akili timamu akisoma maelezo yako uanjua wewe na kundi lako ndiyo tatizo na Kassim Majaliwa ni kikwazo kwenu.
Siasa hizi za maji taka ziliisha na utawala wa JK. Cha kushangaza zimerudi kwa kasi awamu ya Mh. Samia sasa sijui tuamini tuhuma za kwamba JK ndiyo ameshika remote awamu hii ya Mh.Samia?

Mh.Samia umezidi kupoa sana kiasi kwamba kila takataka za enzi za JK zimerudi kama vile tuna kiongozi dhaifu kama wakati ule. Nimemnukuu John Mnyika suala la udhaifu wa kiongozi awamu ile.
 
Mnataka atimuliwe ili mle mpaka msaze sio. Majaliwa is the best, zaidi hata ya hangaya kwenye utendaji, ufuatiliaji na ku provide leadership.
 
Acha kutukoseaa

Wanaotakiwa kujiuzuli ni

Nape misses

January Makamba

Ndio Mawaziri mizigo
 
Naona Majaliwa anawanyima ulaji na kukwamisha Mipango yenu dhalimu. Mnatumika vibaya
 
Ajabu sana, unamlaumu PM kama vile yeye ndie Rais wa nchi.!! hao mawaziri humuita Rais "mama" nae huwaitikia kwa kuwaita "wanangu" kumbe wanamzunguka nyuma ya pazia nae asijue chochote.

Unazidi kuthibitisha jinsi kule juu palivyo na incompetent personnel, ndio maana wasaidizi wake wote wanajiamulia chakufanya [Mwigulu na tozo, Makamba na biashara yake ya mitungi ya gesi].

Ningekuona wa maana kama ungemwambia yule wa kule juu kabisa aondoke, lakini akibaki, hata wasaidizi wake wapya watakuja kumchezea tu, kwasababu ni dhaifu.
 

Nimesoma huu uzi ila nakiri kutoelewa tatizo la Majaliwa Mjaliwa ni lipi hapa.

Nimeona sehemu umedai mawaziri wanamdharau Rais lakini Majaliwa anakunywa nao juice, sasa hapa tatizo ni la Majaliwa? Rais yeye hajui kama kuna mawaziri wanamdharau? Kwanza hebu tuwekee list ya hao mawaziri ambao wanamdharau Rais wewe unawajua na Rais hawajui.

Kwa tuhuma zote umetoa hapa, unaonesha kabìsa unamlaumu Rais na wala sio Majaliwa.

Ninachoona mimi, hapa tatizo ni Uwaziri mkuu tu. Huko alipo Majaliwa wote ni wapigaji tu, labda mseme mmekasirikiana kwakuwa kuna mmoja kapiga kuliko mwenzake au kuna mmoja kazuia mwenzake kupiga.
 
Kama inafika wakati Wasaidizi wa rais wanamdharau kisa ni Jinsia ya Kike, kuna nini tena?
Inawezekana kabisa ikawa ni wewe mwenye matatizo hayo, ya kudharau watu kwa misingi ya aina hiyo au nyingine.
Wewe (mwandishi), umejuwaje kuwa rais anadharauliwa kwa misingi ya "jinsia yake", na siyo kwa mambo mengine, kama kutokuwa na uwezo wa kiuongozi?
 
Magufuli alisema kuna watu walishaagiza suti wakijiandaa na Uwaziri mkuu lakini akamchagua Majaliwa ambaye hata hakujua kama atakuwa.

Kundi la walioshona suti ndio linamkaanga majaliwa sasa, na watamkaanga sawa sawa.
 
Uh-Oh!

Sikujua, kumbe hii ni vita ya ndani kwa ndani! Ni mnyukano unaoendelea humo humo ndani ya serikali yenyewe?

Haya maneno uliyomalizia andiko lako nayo, yanaonyesha dhahiri ya udhaifu wa huyu Samia, ambaye kumbe hata wewe mwandishi unaufahamu vyema.

Sasa ninakuuliza, kwa nini usipige kampeni ya kuiondoa serikali yote nzima, ikiwa ni pamoja na huyo rais unayejuwa kuwa "anapangika"?
Wewe mwandishi, kweli unayo mapenzi dhati na nchi hii na wananchi wake, au mapenzi yako ni kwa kujaza matumbo yenu mkiwa na rais huyo mnayemwona "anapangika"?
Kwa sasa hivi inaonekana unafanya juhudi kubwa za "kumpanga" awe upande wenu ili nanyi mfaidike kama akina Kassim wanavyofaidika sasa hivi!
 
Umejuaje au uongo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…