Rais Samia: Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka

Rais Samia: Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Wakuu wa wilaya nchini wameacha kufanya kazi kwa hofu ya kuondolewa au kuhamishwa vituo vya kazi.

“Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka. Sikusema nitawabadilisha leo au kesho, kwahiyo kama hamfanyi kazi hao ndiyo wangu.”

“Kutoa mkeka ni kazi yangu na nitautoa wakati muafaka, wakuu wa mkoa nataka ripoti za wakuu wenu wa wilaya.”

Ameyasema hayo wakati akishiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, katika Jengo la Kitega Uchumi jijini Dodoma
 
Ndio ubaya wa vyeo vya kuteuliwa. Tuige mfano wa Kenya. Mkuu wa mkoa (kaunti) anachaguliwa na wananchi na ana cheo cha gavana. Hawana haya mambo ya mtu kusubiri kuteuliwa kila baada ya wiki.
 
Hufanyi kazi sababu unasubiri mkeka halafu unaonekana hujafanya kazi na huwezi umeshindwa kazi ukija mkeka mpya unaondolewa
 
Ila mama kama unalalamika sana siku hizi. Mama wewe ni Rais na amiri jeshi mkuu, hebu chukua hatua alafu toa taarifa. Yaani kama hapo badala ya kulalamika ungesema nimemtengua Fulani na Fulani sababu hawafanyi kazi wannasubiri mkeka na nimempa onyo la mwisho Fulani. Uwanibikaji utarudi mama
 
Unateuliwa mkuu wa wilaya, unapongezwa na ndugu, jamaa, na marafiki, halafu siku ya pili baada ya pongezi unaanza kutetemeka hujui lini utaondolewa, matokeo yake hata mood ya kufanya kazi mtu anakosa, akiharibu anaondolewa, anawekwa mwingine & the circle continues..
 
Hivi vyeo vya RC na DC vilitakiwa viwe vimefutwa miaka mingi kwani ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi!
Hawana chochote cha maana wanachofanya zaidi ya kulinda maslahi ya chama chao ktk maeneo waliyopo!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Wakuu wa wilaya nchini wameacha kufanya kazi kwa hofu ya kuondolewa au kuhamishwa vituo vya kazi.

“Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka. Sikusema nitawabadilisha leo au kesho, kwahiyo kama hamfanyi kazi hao ndiyo wangu.”

“Kutoa mkeka ni kazi yangu na nitautoa wakati muafaka, wakuu wa mkoa nataka ripoti za wakuu wenu wa wilaya.”

Ameyasema hayo wakati akishiriki hafla utiaji saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe leo tarehe 30 Septemba, katika Jengo la Kitega Uchumi jijini Dodoma
Mlio karibu na mama pelekeni cv yangu, Naweza kumsaidia vizuri wilaya au mkoa wowote hasa kanda ya ziwa, mkeka huo nisikose wazee
 
Wafanye kaz gan wakat hamna cha kufanya? Hivi vyeo vya rc na dc havina mana yan mkoa mmoja unakuta una wabunge zaid ya wa3, dc,rc,ras,das na wote wanalipwa kupitia kodi na tozo za wananch
Halaf mkoa wenyewe Daslam
Bora hata ingekuwa Tabora, Morogoro,kigoma et al......
 
Ni kweli

Cheo cha mkuu wa Wilaya kifutwe DED anatosha

Mbona RDD aliondolewa na RC anachapa kazi kama kawa!

Huelewi unachochangia alipoondolewa RDD kikaundwa cheo cha RAS.
Mimi binafsi sioni umuhimu wowote wa kuwa na cheo cha RC na sekretariet yote ya mkoa, Kuwe na ma DED tu. PCCB na TIS waachiwe kazi ya kusimamia uwajibikaji
Hawa ma RC na Ma DC wanasiasisha utendaji ( politicising the public administration)
 
Vyeo hivi vilichakatuliwa ili wale watakao kuwa wanakosa pahara pengine, wapachikwe huko ili waendelee kutukuza.
 
Back
Top Bottom