Rais Samia: Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka

Rais Samia: Wakuu wa wilaya hamfanyi kazi, mnasubiri mkeka

Ukisoma post moja baada ya nyingine zote zimejaa upumbavu , utegemezi, udumavu wa akili na umaskini, hivi kuna mtu alizaliwa DC au kutokuwa DC utakufa? mbona vijana watanzania ni wajinga kiasi hiki..nchi hii ina future kweli kwa aina ya watu wanaofikiri kwa kiwango hiki? Hili halikupaswa kabisa kuwa kitu cha kudiscuss, mteuzi ana uhuru wa kufanya kadiri anavyoona inafaa..kama tumefanya uongozi ni ulaji, basi tuna taifa halina future!
 
Kweliiiiii Mama, yaani Mh. Rais ana macho makali sana aiseee. Ma DC wako wako tu siku hz, hawafanyi kazi ipasavyo, Mh. Rais wapige chini najua unawajua wote wanao kaa kaa, barabara mitaani mbovuuuu hasa Dar, matatizo ya wananchi kibaoo hata Ma DC kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zao hakuna, utafikiri Wilaya haina DC wala Mkurugenzi, wanasubiria hadi Mh. Rais aje ndio aongee na wananchi na kutatua kero zao.

Waambie kabisa wasikae maofisini kazi vikao kila siku visivyo isha ili kupata posho za vikao tu, unakuta mtu ana vikao 2 au 3 kwa siku, watoke maofisini wakatatue kero za wananchi wanyonge mitaani na vijijini.
 
Wafanye kaz gan wakat hamna cha kufanya? Hivi vyeo vya rc na dc havina mana yan mkoa mmoja unakuta una wabunge zaid ya wa3, dc,rc,ras,das na wote wanalipwa kupitia kodi na tozo za wananch
Nakubaliana nawe!
 
Back
Top Bottom