Kweliiiiii Mama, yaani Mh. Rais ana macho makali sana aiseee. Ma DC wako wako tu siku hz, hawafanyi kazi ipasavyo, Mh. Rais wapige chini najua unawajua wote wanao kaa kaa, barabara mitaani mbovuuuu hasa Dar, matatizo ya wananchi kibaoo hata Ma DC kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zao hakuna, utafikiri Wilaya haina DC wala Mkurugenzi, wanasubiria hadi Mh. Rais aje ndio aongee na wananchi na kutatua kero zao.
Waambie kabisa wasikae maofisini kazi vikao kila siku visivyo isha ili kupata posho za vikao tu, unakuta mtu ana vikao 2 au 3 kwa siku, watoke maofisini wakatatue kero za wananchi wanyonge mitaani na vijijini.