Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

 
Mama usicheke na kima, fukuza wote ujenge heshima na kuaminiwa zaidi na Watanzania.
Huyo hata afukuze wote mpaka mumewe hamna mwenye akili atamuelewa.

Kiongozi mkuu wa nchi kusimama hadharani na kuelekeza walio chini yake namna wanapaswa kula (kuiba) ulikuwa udhaifu mkubwa sana kiutendaji na kupitia udhaifu huo nchi itaumia sana.
 
Maana yake Invoice imejidouble 🤣🤣🤣

Ongezeko la $ 49 Million. Zaidi ya Billion 112 za Kitanzania.

Kuwaondoa kazini ni kuwapa nafasi ya kuzitumia hela zao kwa uwazi na uhuru. Hakuna mtumishi wa Umma atastaafu na ukwasi wa walau Billion 3.

Kama Mh Rais ana nia basi waondolewe na moja kwa moja mahakamani.
 
Mzee alimwachia watendaji wazuri, yeye akawafukuza, hao watamla hela mpaka basi, kufikia 2025, kapu halina kitu.
Rais atafanya mabadiliko ya msingi kwenye mfumo wa Usimamizi wa Mali.

Mwendazake na kufura watu walioiga za kutosha sembuse saizi..

Hapa inatakiwa mfumo wa Usimamizi uhusishe wengine bila kusubiria Central government walau inaweza saidia..
 
Alafu kuna takataka humu zimekomaa na plea bagain ya bilion 3
 
Rais aliwapa ruksa wale kwa urefu wa kamba yao ila wasivimbiwe. Sasa analalamika nini wakati wamefata maagizo kutoka juu??
 
Huyo hata afukuze wote mpaka mumewe hamna mwenye akili atamuelewa.

Kiongozi mkuu wa nchi kusimama hadharani na kuelekeza walio chini yake namna wanapaswa kula (kuiba) ulikuwa udhaifu mkubwa sana kiutendaji na kupitia udhaifu huo nchi itaumia sana.
Mbona kama mna akili ndogo sana ,hivi kula Kwa urefu wa kamba Yako Kuna shida kwenye hiyo Kauli?

Kwamba Ile methali ya Kila mbuzi hula Kwa urefu wa kamba yake Ina walakini?

Wewe Ukiwa muajikiwa hujui urefu wa kamba Yako? Kuiba si ndio kuvuka kamba? Hapo Kuna tatizo gani mbona mna shida mahala kwenye uwezo wenu wa kufikiri?
 
USITUZINGUE. Wizi na CCM unawezaje kuvitenganisha??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…