Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Rais Samia: Waliopokea ongezeko la gharama za ununuzi wa ndege ya mizigo waachie nafasi zao watupishe

Leo kaongea kwa hasira sana na matusi kibao hhaaa wabongo bila nguvu hawaeleweki

USSR
Nyie Machawa na Viroboto wa CCM tangu enzi ya Mwendazake mmekuwa watetezi wakubwa wa wezi wa mali za umma. Unscruplous individuals within CCM circles are the best Swindlers and Embezzlers of Public Funds for personal financial gains. Yet you treat them as Heros. Phweeeeh
 
Naona Rais anaanza kuelewa kwamba Watanzania bila kupelekea kama punda Huwa hawaelewi ni wezi kuliko unavyodhani..
Nani kati yenu anajua bei za zile Ndege za awali? Bei zake zilikuwa confidential utadhani ni siri za usalama wa nchi. Hongera Rai's SSH kwa kuwa muwazi, walau tunaendelea kuthibitisha awamu ile ilichezea hela ya wananchi kwa manunuzi ya ajabuajabu kwa maslahi ya wachache.
 
Highly unlikely wakati Radar tu ilipigiwa hela. Huo ununuzi sio wa nyanya mzee. Thats billions of money ambazo ni USD millions karibia 50. Mzungu gani hataki kuwa sehemu ya hio pesa 🤣?
Sakata la Radar sio wizi per se wa kwenye invoice.

Issue ilikuwa kuna watu walitoa hongo ili kuiuzia nchi RADAR mbovu kitu ambacho wanadhani sio sahihi kwa nchi maskini na ilikuwa aikihitaji.

Kutoa hongo kupata contract is common practice, hasa kwenye maswala ya ununuzi wa silaha za kivita; hiyo ni BAE system culture.

Lakini uwezi toza invoice ya $82 million halafu uandike anything else kwenye ledger it doesn’t work that way, besides hiyo hela utalipa kwenye account ya Boeing itafanyiwa conciliation na department nyingine. Huo mfumo una watu wengi wa kuchunguza ni vigumu hiyo hela kuitoa ikishaingia kwenye system yao kama income.

Hiko kitu ni highly unlikely system zao of control ni imara hao watu, sio Tanzania kila kitu possible.
 
Mbona kama mna akili ndogo sana ,hivi kula Kwa urefu wa kamba Yako Kuna shida kwenye hiyo Kauli?

Kwamba Ile methali ya Kila mbuzi hula Kwa urefu wa kamba yake Ina walakini?

Wewe Ukiwa muajikiwa hujui urefu wa kamba Yako? Kuiba si ndio kuvuka kamba? Hapo Kuna tatizo gani mbona mna shida mahala kwenye uwezo wenu wa kufikiri?
Usitufanye sisi wajinga, kauli ya kwanza alisema anajua kwamba wanakula lakini akahoji mbona wanakula sana? Watavimbiwa.
Sahizi unataka u edit kauli za mtu ambaye video zake zipo.
 
Wewe jifanye unakijua sana Kiswahili wenzako huko wanapiga,mama yenu aliwasisitiza kabisa "kuleni (ibeni) lakini msiibe mpaka mkavimbiwa (mkastukiwa)" na hao wameiba mpaka wakavimbiwa ndo maana wamestukiwa.

Na aliyewashauri waibe hana cha kuwafanya hizo mbwembwe tu.
Hahahahah jamaa anatuona wendawazimu🤣
 
Kuna watu wameongezeka 110% kwenye gharama za Ununuzi wa Ndege ya Mizigo. Nadhani Sasa Mh. Rais ameanza kuwafahamu Watanzania. Hawa watu msiishie kuwafuta kazi waende mahakamani.

Hii Nchi watu Kuiba ni sehemu ya maisha Yao so kuwasimamia Kwa kuwabembeleza watakutafuna Hadi ukome. Watanzania wanatakiwa kuendeshwa kama punda ndio wanaleta.

Mwisho waboresheeni maslahi Yao pia vinginevyo Kuna syndicate kubwa sana ya wizi.

==============

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kuchukizwa na kitendo cha ongezeko la fedha za manunuzi ya Ndege mpya ya mizigo kinyume na fedha ambazo zilikuwepo kwenye mkataba wa awali huku akiwataka Watumishi wa Serikali waliokubali ongezeko hilo bila kuhoji waachie nafasi zao kwakuwa hawana uchungu na fedha za Watanzania.

“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji”

“Baada ya kuhoji akasema nilipokea hivi, nimeambiwa hivi lakini bado nimeoka tufanye hivi, huyu unamuelewa lakini Mtu anapokea kwa raha zake tu analeta Serikali ‘Kuna hiyo invoice imekuja, vifaa vimeongezeka baada ya covid, pumbavu haiwezekani….. Mawaziri tusaidieni over-invoicing zipo nyingi sana” ——— Rais Samia.

Wakuu nujuzeni, nani anasemwa hapo?
 
Mbona kama mna akili ndogo sana ,hivi kula Kwa urefu wa kamba Yako Kuna shida kwenye hiyo Kauli?

Kwamba Ile methali ya Kila mbuzi hula Kwa urefu wa kamba yake Ina walakini?

Wewe Ukiwa muajikiwa hujui urefu wa kamba Yako? Kuiba si ndio kuvuka kamba? Hapo Kuna tatizo gani mbona mna shida mahala kwenye uwezo wenu wa kufikiri?
We ni mandazi kweli kweli.
 
Hivi kutoka dola milion 37 mpaka dola milion 86 ni 10% ? Haya tuoneni wajinga tu.
 
Ndugu ununuzi wa ndege mpya auna tofauti sana na construction contract. Unalipa kwa hatua kadri kazi inavyofanyika ni matakwa pia ya IFRS 15 in recognition of revenue.

Hatua ya kazi ikiisha ujalipa on time kuna penalties and fines; ukichelewa kulipa na interest juu.

Kingine hakuna kampuni ya kigeni inafanya biashara ya muda mrefu bila ya discounting factor hiyo ni automatic inflation mitigation risk, pamoja na hayo contractor wa ujenzi makini anatuambia prices might go way beyond their expectation na hayo mambo yatakuwa kama sehemu ya ‘variable consideration’.

Ni hivi sitetei au sipingi, busara ni kusikiliza upande wa pili. Boeing siyo hizi kampuni zetu eti waongeze bei kwenye receipt upewe cha juu. That is highly unlikely, management inafanya kazi kwa niaba ya shareholders. Any income itakuwa correctly recorded in their books na wanakuwa audited thoroughly. So sioni how mtanzania anaweza faidika hapo, it’s close to zero possibilities ya mtu kupata mgao hapo.
Usitetee wizi, hiyo siyo ndege ya kwanza kuundwa duniani.
Kuna zilizotengenezwa kama hizo in thousands.
 
Sasa akifukuza wote si mtasema Mama nae ni Dikteta Kama Mwendazake!!? Watanzania mnatuchanganya sana,na hata sijui mnataka nini!? Mkipewa Jua mnataka Mvua, na mkipewa Mvua mnataka Jua!! Mnatuvuruga kabisa!!
Watanzania naona wafeerwe tu maana hakuna namna ingine. Ni wanafiki wa kiwango cha kutukuka.
 
Ndio maana wengine Mungu hakupenda tuwe Viongozi...hakika kwa mtu kama mimi Leo kungekuwa na Maturubai sehemu nyingi sana.
[emoji23][emoji23][emoji23]ungefanya nn mkuu?
 
Kwenye Hotuba yote ya mheshimiwa Rais naweza kusema alikuwa anasema kwa moyo wa dhati na wenye lengo la kuwataka watendaji walisaidie taifa.

Lakini hadi kufika eneo hili kwenye clip hii hapa chini, mama alikasirika sana yaani sana hadi kutoa lugha inayoonyesha alikerwa hasa.

View attachment 2570051
Mtu kapiga 115 billions halafu commander in chief anasema anaomba lifanyiwe kazi dah
 
Back
Top Bottom